Cytochrome p450
JF-Expert Member
- Mar 19, 2019
- 5,638
- 15,044
Leo Arsenal imetolewa rasmi kwenye michuano ya kombe la Europa League baada ya kupigwa nyumbani kwake mabao 1-2, mechi ikienda hadi kwenye dakika za nyongeza na mwishowe tukishuhudia Arsenal ikitolewa kwa aggregate ya magoli (2-2)
Binafsi kama mpenzi wa soka la ulaya, yafuatayo ni machache kati ya mengi niliyoyaona kwenye timu ya washika bunduki (The Gunners)
1. Lacazette hafai kuwepo kwenye timu ya Arsenal
Wakati anakuja alifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri ambacho mimi kama mdau wa soka la kulipwa nilikikubali kwa asilimia nyingi. Wengi walikuwa wakimuita Fighter kwa jinsi alivyokuwa akijiyoa kwa ajili ya timu. Ila ukweli uliopo sasa ni kwamba jamaa kabakia NDEVU tu, hatishi tena.
2. Pepe sio mchezaji wa kiwango cha Arsenal
Nilikuwa mgumu sana kukataa hili ila sasa naliona nikiniumbua moyoni. Niliamini sababu ya mazingira mapya ndio iliyomfanya mpaka asiperform vizuri, ila sasa kwa mbaali namuona kama Gervinho anakuja hivii! Mara anakataa!!
3. Mustafi ni mchezaji wa timu ndogo
Sijui Arteta kapata ushujaa gani wa kumuamini yule jamaa. Kwanza hajiamini hata kidogo. Naona watu wanamsifia siku hizi, ila kwangu mimi nikimuona nazuta picha ya dumu la petrol tu. Muda wowote.
4. Timu yote ni ya kubadili isipokuwa wachezaji wawili (2) tu
Hao ni kipa, Leno pamoja na Auba. Waliobaki wote sio hadhi ya Arsenal.
Nihitimishe tu kwa kusema, Arsenal kwa stage iliyofikia haitakiwi kushiriki mashindani makubwa yeyote ie. UEFA Champions League/Europa League. Kwa sasa ni bora wazingatie kwenye kuboresha timu zaidi. Nafikiri itakuwa na ushindani zaidi baada ya misimu miwili au mitatu.
Nawaza itawezaje kupata World Class Players kama haitoshiriki mashindano makubwa kama UEFA? Jibu sipati.
Timu kama Liverpool nayo ilipitia vipindi vigumu kama hivi, lakini wakapata kujijenga na sasa imerudi kwenye game.
Tunaona hakuna wachezaji mizigo tena kwenye timu kama Liverpool.
Tumpe muda Mikel, labda anaweza akaleta mabadiliko.
Mimi sio mwandishi mzuri, ila kwa hapo nilipojitahidi nadhani ujumbe umefika.