Wacha nami niwanyoroshe kama Mfipa
Rais Magufuli amesema hayo leo April 27, 2018 wakati akifungua barabara ya lami kutoka Dodoma hadi Babati, Manyara yenye urefu wa kilometa 251 ambayo imegharimu Tsh. Bilioni 378.
“Siwezi kuhangaika kutafuta fedha za kujenga barabara, kununua ndege, viwanja, alafu bado nitafute na fedha za kuwanunulia chakula cha bure. Nasema, hakuna chakula cha bure, ambaye hatalima, atakufa njaa,”
“Mvua imeenyeesha miezi yote halafu ije itokee mwezi wa ngapi mseme tunaomba chakula kuna njaa tutakufa nitasema tu kufa. Nawaambia Watanzania wote kuanzia Kongwa mpaka Chato hakuna chakula kitakachogaiwa mwaka huu,” amesisitiza.