A
Anonymous
Guest
Niishi Geita, nilisoma katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Mafinga (Mafinga College of Health and Allied Sciences – MACHAS), ambacho awali kilijulikana kama Clinical Officer Training Centre Mafinga (COTC).
Nilijiunga na chuo hicho kusomea Astashahada ya Utabibu (Certificate in Clinical Medicine) na nilifanikiwa kusoma kwa miaka miwili hadi mwaka 2021, nikiwa na namba ya usajili NS 182/0039/2017. Hata hivyo, nilishindwa kuendelea na masomo ya Diploma ya Utabibu kutokana na changamoto za kifedha, hivyo nikaomba kutunukiwa cheti cha ngazi ya astashahada kulingana na utaratibu wa chuo.
Nilifuata taratibu zote zilizohitajika na kuwasilisha maombi yangu chuoni, lakini hadi sasa zimepita takribani miaka mitano bila kupata cheti changu. Nimekuwa nikifuatilia mara kadhaa chuoni na hata kuwasiliana na mamlaka husika serikalini, lakini nimeendelea kuelekezwa kurudi chuoni ambako napata majibu yasiyo na uhakika.
Nina transcript yangu ambayo nilipata muda mrefu uliopita, lakini bado sijafanikiwa kupata cheti. Kutokana na kukosa cheti hicho, nimeshindwa kutumia taaluma yangu kupata ajira na kulitumikia taifa, licha ya kuwa nina uwezo na ujuzi wa kufanya kazi.
Mimi ni kijana kutoka familia yenye hali ya chini, na familia yangu inanitegemea. Kupata cheti hiki kutanipa fursa ya kuomba ajira, kujitegemea na kuweza kusaidia familia yangu pamoja na kutoa huduma kwa jamii.
Naomba msaada wenu ili haki yangu ipatikane.