Machawa wa Mwigulu na Januari Makamba waliokuwa mitandaoni 2015 wako wapi leo?

Machawa wa Mwigulu na Januari Makamba waliokuwa mitandaoni 2015 wako wapi leo?

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Mwaka 2015 watia nia ya urais kupitia CCM Mwigulu Nchemba na Januari Makamba walikuwa na timu kubwa sana za vijana wa kuwashangilia mitandaoni ili kuuhadaa umma kwamba ni viongozi wanaokubalika sana na jamii na wanafaa kushika madaraka makubwa ya nchi.

Najiuliza leo Mwaka 2022 Makamba na Mwigulu ndio kipindi ambacho wanamiliki pesa nyingi zaidi kuliko kipindi hicho cha 2015 lakini hatuoni mitandaoni zile timu za kuwashangilia kama ilivyokuwa 2015

Nini kimetokea hadi makundi hayo ya vijana yaliyokuwa yamefadhiliwa fedha nyingi na vitendea kazi kama simu na laptop kwa kazi hiyo leo wako wapi .

Tunaona viongozi hao wanashambuliwa sana mitandaoni ilihali sasa wote wana pesa nyingi sana mfano Makamba ana TANESCO ambayo anaweza kuwapa Mameneja wa Mikoa maelekezo yoyote kuwalipa watu fulani wa kumpigania.

Mwigulu ndio usiseme mikopo yote anasaini yeye hana njaa hata kidogo ya pesa kwanini vile vikundi havifanyi ile kazi ya 2015 hali iliyosababisha makada hao wawili Mwigulu na Januari kuburuza mkia kwenye uchaguzi wa NEC.

1903043_1080164505344277_1053305056_n.jpg

J26A6362.jpg
 
Wengi wako bize,kujiimarisha kisiasa,mfano Nicodemus,ni katibu tawala wa wilaya ya Lushoto,hivyo yuko bize,hawezi kushinda mitandaoni akimpigania Mwigulu.
 
mimi nilikuwa chawa januari umenikumbusha kabla ajawa february
 
Back
Top Bottom