Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Baada ya kifo cha Milambo, hakukuwapo na mtemi mwingine mwenye jina hilo kwenye eneo lote la Unyanyembe.sawa sijaweka mimi nimepewa hivyo hivyo tusaidiane kuirekebisha. Ila ila inaelekea Mkwawa na Mirambo walipata warithi na walitumia majina yale yale yaani Mkwawa na Mirambo wale wa kwenye Historia. Sababu mpaka leo Mrithi waMkwawa yupo
Milambo mwenyewe alirithiwa na mwanawe wa pekee aliyekuwa kiitwa Nyungu-ya-Mawe ambaye naye alikufa mwaka huo huo wa 1884 ndipo utemi wa Unyanyembe ulipovunjika kukawa na temi ndogogondogo kadhaa ambapo mtemi Katu-ka-Moto na alitawala eneo la Urambo na sehemu nyingine kubwa ikawa chini ya mtemi Isike. Hata hivyo wajerumani wawaua mtemi Isike na mtemi Katu-kaMoto na kuweka mtemi wao wa kike aliyekuwa akiitwa Bibi Nyaso kuwa mtemi wa Unyanyembe yote. Wakati waingereza wanaaza kutawala nchi hii, utemi wa unyanyembe ulikuwa umshegawanyika na kuwa dhaifu sana wala hakukuwa na trace zozote za mtemi Milambo tena. Chief wa Unanyembe aliyekuja kupatikana baada ya utawala wa waingereza alikuwa Chief Fundikira.