Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kwa mfano anatoka Makamu Mwenyekiti wa (Chanzo Cha Matatizo) CCM kwenea Ntwara, akifika huko anasimikwa uchifu, akija mwenyekiti wa hicho kijiwe naye anasimikwa uchifu.
Mara utasikia wazee na machifu wa Songwe wamemsimika uchifu mkuu wa mafisadi huku wakimpa sifa kem kem.
Numejiuliza, taratibu za kupata mkuu wa machifu ama mkuu wa kabila fulani zimekuwa holela namna hii? Tunajua ili mtu awe chifu, kwanza lazima awe mzaliwa wa kabila ama ukoo husika, pili ajue mila, desturi na taratibu za kabila husika hususan miiko na maadili ya jamii husika.
Anapaswa kuwa na nguvu ya ziada inayounganisha imani na matumaini ya jamii hiyo.
Sasa hawa machifu waliojisimika kwa hila wamekuwa wanagawa gawa uchifu kama zawadi kwa wanasiasa wakiamini watafaidika kiukwasi na hulka hiyo. Wengi wa hawa machifu waliingia kwa hila during German colonialism, waliingizwa uchifu ili kuwabomoa na kuwafuta machifu wa kweli na haki kwa jamii husika. Wale wote walioisaliti jamii na kabila zao kwa kuwauza machifu waliokuwa wanapambana kutotawaliwa, walizawadiwa uchifu.
Tukubali kwamba, usaliti dhidi ya jamii huzalisha maafa kwa jamii husika.
Toka lini Mkojani akatawala ziwani? Toka lini wa Ziwani akatawala milimani?
Gete gete, tugende baghosha