Mkuu arusha siyo mkoani ,Arusha ni nchi huru iliyo ndani ya Tanzania na inajulikana kwa jina letu kuu U.S.A- United State of Arusha a.k.a Chugga na watu wa huku ni wa chugastani au wadudu ukipenda hivyo
Nah uku hatuitani majina zaidi ya kuitana machaliii na wanawake wetu ni la mama /manzi/ demu wa msela
Na ukiwa unataka utelezi huku kijanja tunaita ""nyauuu"" mwambie la mama naomba hiyo nyauu kiroho safi na usijifanye mjuaji utapewa.
Hivyo ukija huku angalia usichukue demu wa msela . Siyo kila mwanamke utakaye muona Mrina Bar / Shivazi ukazani anajiuza wengine ni demu wa msela wanapitapita mitaani. Soma code kijanja sana utajua demu wa msela na dada poa
Ukijichanganya Chugga utakua chakula cha wadudu na hakika tutakukula bila maji.
Tahadhari hii iwafikie WANAUME WOTE WA DAR maana wakija huku wanajiona wajanja mbele ya madem zetu hakika mtaumia kuweni makini .
Nchi yetu ya Arusha ni nzuri na ya kistaarabu sana na tunapenda wageni , ukikutana na kijana/ Mzee ndani ya nchi yetu salamu nyepesi ni 'oi, niaje, inakuaje""
majibu yake ni "haina noma ,poa arifu, haina kwere au barida tuu"
Ewe mwanaume /mdada / mzazi kusalimiwa na manzi wa huku kihuni usiwaze ndiyo salamu za huku.
Salama za kumpa demu ni "mambo" au "niaje la mama" Wako pisi manzi zetu japo wababe hivyo unatakiwa ukaze kiume na usirushe nako maana masela hatupendi fedhea au upige manzi zetu, demu kama hakuwezi anakujazia "nzi ". Na hakika tutakutafuna bila maji.
ONYO uwapo ndani ya nchi ya Arusha usimwambie Mwanaume au jinsia ya kiume "mambo" unaweza kukatwa pasipo nakujua kosa lako ni nini.
KARIBUNI SANA ARUSHA , KARIBUNI NDANI YA NCHI YETU YA ARUSHA YENYE HALI NZURI YA HEWA NA SEHEMU NYINGI ZA UTALII