Machinga Dodoma mjini wapewa masharti ya kijani

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
2,181
Reaction score
1,493
Baada ya bomoa bomoa ya maeneo ya JAMATINI,SARAFINA NA STAND YA MKOA maeneo ambayo yanamilikiwa na Shirika la Reli Tanzania na Wajasiliamali kupitia umoja wao wameomba eneo la kufanyiabiashara kwa muda wakati wanajipanga kuisoma namba huku wakijiandaa kwa maamuzi magumu 2020.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma ameibika na kuwapa eneo kwenye D-center ya Makole hapa hapa Mjini lakini amewapa masharti kama yafuatayo:-

1.Wajenge vibanda vya muda huku wakisubiri mpango wa Jiji ndo wapewe sehemu za kudumu.

2.Vibanda vyote watakavyojenga lazima viwe na RANGI YA KIJANI KILICHOIVA.

3.............

Nikajiuliza binafsi kwanini iwe rangi ya Kijani au wanasisitiza usitawishaji Makao Makuu??au ndo UCCM wa wazi mchana kweupe?



 
We jamaa si ni mkereketwa wa kijani,leo imekuwaje?
Umewahi gombea hata umeya kwa tiketi ya kijani, na mara ya mwisho ulikuwa unampigia debe mgombea udiwani wa kata ya Chipogolo kupitia CCM.
Leo kwa wamachinga kimekusibu nini?
Wasaidie tu kupaka rangi ya kijani,ila kaa ukijua kuwa upinzani ni ideas na ambazo zipo kichwani mwa wananchi hata wakilazimishwa kuwa na muenekano wa kijani ila nafsi zao ni upinzani tu.
 
M
Mkuu kuna mahali umechanganya ni kweli nashiriki sana Siasa lakini sijawahi kuwa CCM na hata Chipogolo nilikuwa namnadi mgombea wa Chadema anaitwa Jafary Jumanne Simba [emoji111]
 
M

Mkuu kuna mahali umechanganya ni kweli nashiriki sana Siasa lakini sijawahi kuwa CCM na hata Chipogolo nilikuwa namnadi mgombea wa Chadema anaitwa Jafary Jumanne Simba [emoji111]
Mkuu naomba tuweke mambo sawa, Inamaana humuungi mkono Rais Magufuli ? Yani huamini anayoyapigania ndio wapinzani mlikuwa mkiyapigania?
Maana nyie wanasiasa ni ngumu kuwaelewa siku hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…