Machinga Mkoani Iringa wagoma kuhamia maeneo elekezi

Machinga Mkoani Iringa wagoma kuhamia maeneo elekezi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
WAFANYABIASHARA wadogo wadogo (MACHINGA) mkoani Iringa wameugomea uongozi wa manispaa ya Iringa kuhama katika eneo la mashine tatu na miomboni ambalo wanafanyia biashara zao hivi sasa.

Akizungumza na waandishi wa Habari katibu wa MACHINGA mkoa wa Iringa Joseph Kilienyi alisema kuwa uongozi wa manispaa ya Iringa wamewapangia eneo ambalo sio Rafiki kwa biashara ambazo wanazifanya hivyo wameamua kugoma kuondoka katika maeneo ambayo wanafanyia biashara hivi sasa.

Alisema kuwa serikali ya manispaa ya Iringa imewapangia wahamie katika eneo la welfare ambalo wanadai ni dogo halafu sio Rafiki kwa baishara ambazo wanafanya kwa kuwa ni vigumu wateje kuwafikia katika eneo hilo.

Kilienyi alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliwaangazi viongozi wa wilaya,halmashauri na mikoa kuwapanga MACHINGA katika maeneo ambayo Rafiki kwa biashara zao kwa kushirikiana na viongo wa wafanya biashara hao ila jambo hilo kwa manispaa ya Iringa Limekuwa kinyume na maagizo hayo.

Alisema wataendelea kugoma hadi mwisho kuondoka katika maeneo ya miomboni na mashine tatu hadi pale serikali ya manispaa ya Iringa itakapo watafutia eneo Rafiki kwa biashara zao ambapo wao wanategemea sana wateja wapita njia.

Kwa upande wake mwenyekiti wa MACHINGA mkoa wa Iringa Yahaya Mpelembwa alisema kuwa eneo ambalo linawafa wafanyabiashara hao ni eneo la makaburi ya Mlande ambapo kuna eneo kubwa na Rafiki kwa wafanyabiashara hao kufanya biashara zao.

Alisema eneo pekee ambalo watakubali kwenda kufanya biashara zao ni eneo la makaburi ya Mlandege kwa kuwa kuna eneo kubwa na Rafiki kwa bishara zao kinyume cha hapo hawapo tayari kuhama katika maeneo yam ashine tatu na miomboni ambyo kwa sasa ndio wanafanya shughuli zao za biashara.

Mpelembwa alisema kuwa eneo la welfare ambalo wamepangiwa na serikali ya Manispaa ya Iringa hawawezi kwenda kwa sababu eneo ni dogo hala halina mzunguko wa watu wengi ambao wangeweza kununua bidhaa zao.

Zeche Zabron aliyekuwa mwenyekiti wa MACHINGA mkoa wa Iringa alisema kuwa wafanyabisha hao wanatakiwa kwenda katika makaburi ya Mlandege tu na sio sehemu nyingine kwa kuwa makaburi hayo yanaweza kuondolewa kwa kuwa yamekaa miaka mingi ambayo kisheria yanatakiwa kuondolewa kwa kufuata tu utaratibu husika.

Alisema hakuna sheria inayokatakaza makaburi kuhamishwa hivyo ameutaka uongozi wa manispaa ya Iringa kuhakikisha wanayaoondoa makaburi hayo kwa mujibu wa sheria za nchi kama ambavyo inatakiwa la sio watalazimika kwenye mahakani kwa hoja ya kuyaondoa makaburi hayo.

Zeche alisema kuwa uongozi wa manispaa ya Iringa unafanya mambo ambayo wanaamua bila kuwashirkisha viongozi wao waliopo madarakani kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alivyowaagiza.

Akijibia kero hizo Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa kila hatua wanayoifanya ya kuwahamisha MACHINGA katika manispaa hiyo wamekuwa wakiwashirikisha viongozi wao mara kwa mara anashangaa kuona wameanza kuyageuka majadiliano yao.

Alisema kuwa walikubaliana na viongo wa umoja huo kuwa eneo Rafiki kwa biashara yao ni eneo la welfare na serikali ikawekeza fedha nyingi ambazo zimetumika kujenga mabanda ya kufanyia biashara na yamekamika sasa anashangaa kuona kumeanza maneno mengine ambayo hayana afya kwa maendeleo ya manispaa ya Iringa.

Ngwada alisema kuwa viongozi wa MACHINGA wamekuwa wakilitaka eneo la makaburi ya Mlandenge jambo ambalo ni gumu kufanyika kutokana na historia ya makaburi hayo.

Alisema kuwa makaburi hayo bado hayajafikiwa muda wa kuyaondoa kwa kuwa bado kuna makaburi ya miaka 40 toka mtu wa mwisho azikwe pili kutakiwa kutafuta sehemu nyingine ya kuhamishia miili ya marehemu waliozikwa katika makaburi hayo.
1643722595616.png


Ngwada alisema kuwa ili kuyaondoa makaburi hayo ni lazima kuwashirkisha wananchi,viongozi wa dini wizara husika na kutathimini gharama halisi ya makaburi hayo na kuingalia sheria inasema na vyote hivyo havijafanyika na viongozi wa MACHINGA Iringa wanataka tu yaondoke wapewe eneo hilo wafanyie biashara.

Alisema kuwa watu waliozikwa katika eneo hilo wanathimini kwa mchango wa kimaendeleo walioufanya hadi kuifikisha manispaa ya Iringa ilipofika hivyo sio japo jepesi kiasi hicho cha kuyaondoa makabuli hayo.

Ngwada alisema kuwa kuna maeneo mengi ambayo MACHINGA wa Manispaa ya Iringa wanatakiwa kufanyia biashara sio eneo ambalo holo wanalolihitaji kwa kutumia mashinikizo bila kujali wataalam wanasema nini.

Nao wazee wa Manispaa ya Iringa wamelaani kitendo cha MACHINGA wa Iringa kutaka kuyaondoa makaburi hayo kwa kuwa hawajui historia ya makaburi hayo na mchango ulifanywa na watu waliozikwa kwenye makaburi hayo ya Mlandege.

Walisema kuwa asilimia kubwa ya wananchi waliokuwa wanapigania maendeleo ya mkoa wa Iringa walizikwa pale ilikuwa kwa kunyongwa na wakoloni kutokana na kutafuta uhuru na kuleta maendeleo ya Iringa.

Waliwataka viongozi wa machinga Iringa kukaa pamoja na serikali ya manispaa ya Iringa na kutafuta eneo linguine la kufanyia biashara hizo kwa kuwa bado kuna maeneo mengi yapo wazi kwa ajili ya biashara zao.

Wazee hao walitoa ovyo kwa mtu yeyote yule atakae husika kuyaondoa makaburi hayo kwa maslai yake binafsi atapata laana kutoka kwa mashujaa hao ambao wamezikwa hapo.

1643722581879.png


Michuzi Blog
 
Upumbavu kabisa
Eti 'wazee wa iringa' wanalaani makaburi yasiondolewe,like serious?
Yaani watu weusi bado tuna safari ,hasa makaburi ya nn? Kwamba mtu atafufuka au nn?

And at the same time ,mnataka maendeleo? Duh jmn kuwa kiongozi kazi aisee[emoji119]
 
Upumbavu kabisa
Eti 'wazee wa iringa' wanalaani makaburi yasiondolewe,like serious?
Yaani watu weusi bado tuna safari ,hasa makaburi ya nn? Kwamba mtu atafufuka au nn?

And at the same time ,mnataka maendeleo? Duh jmn kuwa kiongozi kazi aisee[emoji119]
Mamb ya maendeleo afrika yanakwama Kwa Imani mkuu hta Kwaokoland, kunene. Namibia mambo yalkwama Kwa sabb ya makabur
 
Upumbavu kabisa
Eti 'wazee wa iringa' wanalaani makaburi yasiondolewe,like serious?
Yaani watu weusi bado tuna safari ,hasa makaburi ya nn? Kwamba mtu atafufuka au nn?

And at the same time ,mnataka maendeleo? Duh jmn kuwa kiongozi kazi aisee[emoji119]
Kaburi la Yesu bado lipo la mtume bado lipo,hawa machinga tusiwape bichwa sana,yaani umfukue babu yangu kisa muuza sox za buku buku
 
Welfare ni eneo dogo sana hata wamachinga waliopo pale hawatoshi

Makuburi ya mlandeg yatolewe tu kwanza yamebki machache baada ya wenye nayo kuanza kuyatoa

Mlandege saizi ni makazi ya vibaka usiku na ni guest bubu

Anyway machinga iringa ni changamoto wanatumka mno kisiasa ngoja wapambane na hali zao
 
Welfare ni eneo dogo sana hata wamachinga waliopo pale hawatoshi

Makuburi ya mlandeg yatolewe tu kwanza yamebki machache baada ya wenye nayo kuanza kuyatoa

Mlandege saizi ni makazi ya vibaka usiku na ni guest bubu

Anyway machinga iringa ni changamoto wanatumka mno kisiasa ngoja wapambane na hali zao
Basi wakakae magari mabovu kule....

Pale mashine tatu pilika zimekuwa nyingi mno so ni vyema pia waiache ile barabara ifanye shughuli zingine za kijamii
 
Zaidi ya welfare na viwanja vya mwembetogwa hakuna sehemu nyingine ambayo machinga watapelekwa na kuridhika. Hata hapo makabur ya samora wakipelekwa baadae watarudi tu katikati yamji. Jifunzeni kwenye hilo soko la gharama lililojengwa mlandege kwa gharama ukiingia ndani lipo tupu kama hall la harusi hakuna wafanyabiashara zaidi ya wale waliopo nje wenye maduka tu
 
Wacha wakutane na Flames... Ubishi wa kijinga..
🤔🤔🤷🤷😭
 
Mji wa Iringa inabidi upangwe kwakweli,nimehamia karibuni sijawahi kuona mji mgumu kuendesha gari kama huu,wamachinga kila mahali,inabidi upaki mbali ili uweze kupata huduma,wamachinga wako barabarani mjini hakupitiki kirahisi.Kwakweli serikali ifanye haraka kwenye hili!
 
Mji wa Iringa inabidi upangwe kwakweli,nimehamia karibuni sijawahi kuona mji mgumu kuendesha gari kama huu,wamachinga kila mahali,inabidi upaki mbali ili uweze kupata huduma,wamachinga wako barabarani mjini hakupitiki kirahisi.Kwakweli serikali ifanye haraka kwenye hili!
labda mashine tatu ila sehem nyingin kunapitika poa tu
 
Back
Top Bottom