Machinga ni watu wenye mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa lolote

Machinga ni watu wenye mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa lolote

kahembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Posts
227
Reaction score
310
Machinga ni watu Wenye mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa lolote , hakuna Taifa liloendelea kiuchumi bila kuwa na informal sectors, mfano mzuri ni nchi ya China kwenye miaka ya 1990s Mji wa Beijing ulikuwa na Machinga guys wengi ndo hao baadae wakakua kiuchumi Waka transform kuwa wafanya biashara wakubwa na wakanza kumiliki makampuni makubwa makubwa, Sasa Leo hii kwetu machinga wanaonekana Kama sikanka kwenye miji.

Mimi sipingi kuondolewa kwa wamachinga hata kidogo Ila swali langu je wameandaliwa mazingira rafiki ya kwenda kufanya shughuli zao?

SABABU ZA KUWEPO NA MACHINGA
1. Kutokuwepo kwa ajira katika Formal Sectors, kwa Sasa nchini Tz Kuna uhaba wa ajira kwa vijana wengi wenye fani mbalimbali mfono, kuanzia 2015 serikali imepunguzwa Sana kiwango Cha kutoa ajira kwa vijana wanaotoka vyuo mbalimbali hivyo wanaona suluhisho ni kujiajiri katika biashara ndogo ndogo.

2.Mfumo mbovu wa elimu yetu haumuiandai mtu/ muhitimu kuja kuitumia ile elimu aliyoipata kujiingizia kipato mfano katika fani nyingi vijana wetu wanazozipata mashuleni na vyuoni hakikosa kuajiriwa katika Taasisi either government or private hawezi kutumia hiyo Fani yake kujiajiri kwenye hiyo Fani, kwa mfano Mtu amesomea ualimu wa chuoni huyu akikosa kuajira hatafanya Nini? Au mtu kasomeaa librian, au Ugavi Utasikia eti kaanzishe tution centre.

MADHARA YA KUWAONDOA MACHINGA BILA KUANDALIA MAZINGIRA RAFIKI
1.Watayumba kiuchumi na kufilisika kwani walio wengi mitaji wao imeanza kuharibika.Fikiria wanao uza matunda, mama lishe na baba lishe.

2.Kutaibuka migogoro na kesi nyingi Kati ya Hawa wajasiliamali na Taasisi za kifedha kwani walio wengi mitaji yao wanaipata kwa mikopo toka kwenye hizo Taasisi za kifedha, itafika wakati watashindwa kupata marejesho.

3.Kuibuka na kuongezeka kwa makundi korofi mitaani , Kama vile vibaka, vijana kuanzia kutumia madawa ya kulevya, madada kuanzia kujiuza.

4. Kuongezeka chuki baina ya wananchi na serikali au viongozi wao.
Mwisho. Watawala waliangalie kwa umakini Jambo ili kwani linaweza kutatuliwa kwa njia iliyo sahihi bila kuumiza watu, kwani serikali yoyote ipo kwa ajili ya watu wake.
 
Hawataweza kuendelea kukaa kiholela ukategemea transformation, cha muhimu pangwa na dai mazingira bora na lipa kodi yako kadri ya kipato upatacho
 
Machinga hawalipi kodi, umeme, maji, pango, ulinzi, mwenge, sijui nini? acha waondolewe ili waijue vizuri CCM
 
Wamachinga bado wapo hawajaondolewa, wamewekwa kwenye maeneo sahihi kibiashara. Usituaminishe kuwa kufanya biashara katikati ya barabara kunamuwezesha mmachinga kupata wateja. Mmachinga anachouza kimetoka China, hauzi bidhaa kubwa kubwa zinazotengenezwa nchini hivyo hakuzi viwanda vyetu, huyo mchina uliyemtaja anauza bidhaa zao za China. Utoapo mfano kuwa makini.
Mmachinga amelichafua jiji na halipi kodi ya maendeleo kwa ajili ya usafi.
 
Back
Top Bottom