kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Utangulizi
Nimetembelea Kariakoo Mara nyingi ninapopata fursa ya kufika Dar es salaam. Nimefanya tafiti kwanini bidhaa inayouzwa na machinga iwe nafuu kuliko bidhaa hiyohiyo eneo like inayouzwa dukani? Ukweli ni kwamba Kariakoo na masoko makubwa nchini hakuna machinga Bali Kuna kundi la watu lililoajiriwa na wafanyabiashara wakubwa kuwasaidia kuuza bidhaa zao bila kulipa tozo mbalimbali na kupunguza msururu wa Kodi
Machinga wanapataje bidhaa?
Wanaoitwa machinga kwa mfano Kariakoo ni vijana wengi walioletwa mjini na ndugu zao wenye maduka makubwa kwa lengo lakuwatoa kijijini lakini pia kuwasaidia wapate angalau fedha yakuanzia maisha na kuhudumia familia. Msukumo mkubwa unaopelekea watu Hawa kuongezeka nikutokana na ukweli kwamba gharama yakufanya biashara rasmi nchini nikubwa Sana. Tumeleta efd machine bila kushauriana na wafanyabiashara, tulijikita sana kukamata makontena ya watu yenye bidhaa halali zilizolipiwa kodi kihalali na kuzitangaza bidhaa hizo Kama bidhaa zilizofichwa na zinazohusoshwa na uhujumu uchumi. Wafanyabiashara wakaona isiwe tabu, wasihifadhi bidhaa kwenye makontena wazihifadhi kwa machinga. Sasa hivi mfumo huu umepamba Moto na Sasa bidhaa zinasambazwa nchi nzima kidogokidogo na wamachinga kukusanya fedha baada ya kuuza mzigo na kulipa deni.
Nini chanzo cha kukua kwa wanaoitwa machinga?
Kwanza, chanzo kikubwa ni serikali. Serikali imechangia tatizo ili kwa kuongeza Kodi, tozo na kibaya zaidi kukuza mfumo usio na taaluma ya Kodi wakubambikkia watu kesi. Mfanyabiashara alikuwa anaogopa kukaa na mzigo kwenye makontena kwa sababu akikutwa n huo mzigo hata kama ataonyesha risiti zote mamlaka za serikali zilikuwa zinatamka anahujumu uchumi.
Pili, kukua kwa technology,bidhaa hizi kwa Sasa zinatangazwa online na watu wanapata bidhaa bila hata kufika sokoni hivyo wafanyabiashara Hawa hata Kama utapambana na machinga lakini mzigo unaweza kufika popote machinga alipo kwa kuzingatia uaminifu uliopo Kati ya machinga na wafanyabiashara.
Tatu, serikali kuruhusu raia wa kigeni kufanya shughuli za machinga nchini. Ni kawaida kukutana na waarabu wakisambaza bidhaa mitaani,wachina wanasamabaza bidhaa mitaani na mataifa mengine. Je, tunapaswa kupambana na machinga au tupambane na wageni wanaofanya umachinga? Kwanini wageni waruhusiwe kusambaza bidhaa mtaani na majumbani then tukapambane na machinga waliopanga barabarani?
Wageni wanagonga milango na mageti yetu kinyume kabisa na taratibu na serikali imekaa kimya then tunataka kuwatoa machinga walalahoi? Au kwa sababu wageni Hawa wanatetewa na nchi zao? Uzalendo wa kwanza ulikuwa kupambana na aina mpya ya umachinga.
Nini kifanyike?
1. Serikali lazima iangalie upya mfumo wa Kodi
2. Serikali itenge maeneo ya wafanyabiashara wadogo na tozo au Kodi zinazoligawa
3. Tusiwaze kuwanyonya wamachinga
4. Serikali ipige marufuku raia wa kigeni kusambaza bidhaa majumbani na mitaani, jukumu lakusamabaza bidhaa liwe la Watanzania aidha waajiriwa na wageni au wauziwe bidhaa
5. Serikali iweke halama maeneo yote inayodhani si salama kufanya biashara na waweke kiwango Cha faini kwa watakaokutwa maeneo hayo. Hakuna haja yakutumia jeshi tutumie busara.
Hitimisho
Tatizo la wamachinga kuongezeka litapungua pale wafanyabiashara wakubwa watakapolindwa na serikali na kwamba maeneo yao rasmi na bidhaa zao hazitabughuziwa kinyume Cha sheria.

Upvote
2