JAYJAY
JF-Expert Member
- Oct 31, 2008
- 8,191
- 8,490
Najua jana katika kulazimisha wapate fedha za kufungia mwaka askari manispaa walivunja godown mnakohifadhi mali zenu na kupora na kuharibu mali na kutaifisha.
Kwa kuwa wakati wa tukio mali zilikuwa hazijatolewa wala kupangwa sehemu wanazokatalia msifanye biashara hasa jioni, ni vyema kwa mliopata hasara mutafute haki yenu iliyodhulumiwa.
Tafuteni usaidizi wa kisheria mdai fidia ya uharibifu na upotevu wa mali zenu maana hakuna sheria inayowaruhusu kufanya walichofanya ingawa najua wengine mliwapoza kwa virushwa na kupata mali zenu. Ambao mali zenu zimepotea msikubali kufa kikondoo.
Cha kumalizia mchawi wetu mkuu mnamjua hao wala rushwa uchwara wanatumwa tu.