Machinga waanza kumlilia Hayati Magufuli

Machinga waanza kumlilia Hayati Magufuli

Hawa jamaaa wamezidi aiseee hadi barabaran wnaapanga vitu. Hapa mbagala ni purukushani tupu.. Bado na hawa boda boda ni vurugu nyingine hiii.... Nchi kama haina mtu wa kutoa amri...... Watamzania tunaishi kwa kuogopana sana kwa kigezo cha kunyimwa kura.
 
Hatimaye kilio cha machinga kumlilia JPM, chaanza kusikika, baada ya gari la matangazo kupita mitaa ya tandika na kuwaambia kuwa mwisho wa kupanga bidhaa zao, pembeni mwa barabara, mbele ya maduka, na kwenye hifadhi za barabara mwisho ni 18.10.2021.

Hivyo wanatakiwa kuondoka mapema na kwenda sehemu walizopangiwa, baada ya muda huo, wasije kuilaumu serikali.

Ndipo wakaanza kuimba "tunakukumbuka jpm mtetezi wa wanyonge sasa haupo tumeanza kunyanyaswa" Sasa naona serikali imeamua kweli, ni jambo zuri sana kwani ilikuwa ni kero tupu.
Hakuna cha mtetezi wa wanyonge machinga ktk barabara ni sawa na uchafu kama ulivyo uchafu mwingine.
Jpm nae alikua hatumii ubongo wake vizuri kama aliweza kubomoa nyumba za watu kimara bila fidia huku akiwaacha machinga wazagae kila kona basi ni ufyatu
 
Road reserve wameharibu sanaaa nimeliona baadhi ya maeneo walikotolewa, wamechimba, wameweka zege ni hatari tupu
Sijui hata wanaowatetea kwa nini? Mpaka Kariakoo centre. Nenda Mbezi mwisho pale vurugu tupu.
 
Hatimaye kilio cha machinga kumlilia JPM, chaanza kusikika, baada ya gari la matangazo kupita mitaa ya tandika na kuwaambia kuwa mwisho wa kupanga bidhaa zao, pembeni mwa barabara, mbele ya maduka, na kwenye hifadhi za barabara mwisho ni 18.10.2021.

Hivyo wanatakiwa kuondoka mapema na kwenda sehemu walizopangiwa, baada ya muda huo, wasije kuilaumu serikali.

Ndipo wakaanza kuimba "tunakukumbuka jpm mtetezi wa wanyonge sasa haupo tumeanza kunyanyaswa" Sasa naona serikali imeamua kweli, ni jambo zuri sana kwani ilikuwa ni kero tupu.

Kwanini wasimfuate huko alipo kuzimuni. Lazima tukubali kuishi kwa kuzingatia taratibu.
 
Naona dalili za sisiemu kupoteza uchaguzi ujao.
Kwa hiyo upinzani ikishinda uchaguzi itawaruhusu machinga kupanga bidhaa barabarani?

Unapotekeleza jambo kwa maslahi ya maendeleo ya taifa usiangalie mambo ya uchaguzi; huwezi kumridhisha kila mtu. Wamachinga watambue kuwa zama zimebadilika, wafuate utaratibu bora uliowekwa wa kufanya BIASHARA.
 
Hakunankitu kama hicho mkuu, kwani ushindi wa CCM, wala hautegemei kura za wananchi, wao wana fomula zao, ambazo hazionyeshi njia bali ni jawabu tu.
Wakati upinzani wakitumia formula ya BODMAS chama cha majizi wanatumia formulas za CALICULAS!
 
Back
Top Bottom