kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Machinga sio kikundi cha watu ambao ukishawasikiliza wao na kuwatekelezea kilio chao basi umemaliza, hapana. Watu wanaweza kudhani kuwa machinga ni vijana tu, hapana, ndani ya machinga kuna watoto, vijana, watu wazima na wazee. Mbaya zaidi wadau wa machinga wamo watu wenye wenye ajira zao na wasio na ajira kabisa, wamo raia na wako askari wa majeshi mbalimbali, wamo wanasiasa na viongozi wa serikali mabibi na mabwana ambao idadi yao ni kubwa sana iliyotawanyika nchi nzima mijini hadi vijijini, wanaongezeka kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka. Kundi hili la machinga limezalishwa na mifumo mibovu ya uchumi, elimu, na siasa kitaifa na kimataifa.
Bahati mbaya sana kundi hili la wasiokuwa na kitu mifukoni ndilo wanasiasa wanalolitegemea kupata kura wakati wa chaguzi za kisiasa kwa kutumia gharama kidogo sana na ahadi wasioweza kuzitimiza kwao. Hivyo kabla na baada ya uchaguzi kundi hili linalipwa uholela wa kufanya mambo yao hasa baada ya wanasiasa kushindwa kutekeleza ahadi zao kwao za ajira, mikopo, kupandishwa mishahara, mazingira bora ya kazi, matibabu bora, elimu bora, pembejeo za kilimo, maji, umeme, na masoko ya bidhaa zao kwao. Hivyo hakuna mwanasiasa ambae haliogopi hili kundi, maana ni kundi la watu wasiokuwa na cha kupoteza na wameahidiwa sana kwa miaka 60.
Hivyo basi, Kama kuna mtu anataka kuwahangaikia hawa watu ni lazima kwanza atunge Sera kuhusu hawa watu badala ya kutatua kwa utashi, zimamoto na matamko ya hapa na pale. Sera hii ni lazima iseme wazi kuwa machinga ni nani, ana umri gani, anaishi wapi, ana haki na wajibu gani na lini na namna gani atakoma kuwa machinga.
Mfano, kwenye lile jengo la machinga complex pale Ilala waliopata nafasi ya kufanya biashara kwenye lile jengo ni watu wenye pesa, ajira na vyeo vyao ambao wameajiri vijana wa kuwafanyia biashara zao. Hata ukijenga masoko ya machinga pale jangwani ni kazi bure kama hakuna sera ya machinga, na badala yake utazidi kuongeza malalamiko kwa machinga halisi watakaokosa nafasi ya vizimba. Lakini hata hao wanaoitwa machinga idadi yao inazidi kuongezeka kila siku, utawajengea wapi na wapi ili watoshe wote?
Nionavyo mimi ili kutatua shida za machinga ni kuwatungia sera maalum ili kuwatambua rasmi, na kuwawezesha kupata elimu na mikopo maalum ya riba nafuu kabisa na kuwaacha wenyewe watafute/wachague aina ya biashara/kazi ya kufanya popote nchini kwa kufuata kanuni na taratibu za biashara/kazi husika zilizopo badala ya kuwaahidi kuwajengea majengo, kuwapa mtaa na sijui nini. Kufanya hivyo ni kuzidi kulipalilia tatizo na kuliahirisha kwa kuficha kichwa kwenye mchanga ili awamu ipite salama na anaekuja baada yako atajuana nao yeye mwenyewe.