Machinga wapata neema Dodoma

Machinga wapata neema Dodoma

Mwaka mmoja uliopita agizo la kuwapanga Machinga lilitolewa. Mwaka mmoja baadaye soko la kisasa Dodoma limekamilika limegharimu Tsh Bilioni 9 na sasa limeanza kutumika.

Lengo la soko hilo ni kuwaepusha Machinga na ajali zilizotokana na kufanya biashara pembezoni mwa barabara pia wanarasimishwa, na wataweza kupata huduma za kifedha na kuwa sehemu salama zaidi.

Rais Samia Suluhu amewajali wamachinga.
Nimeliona pale kumbe ndio B tisa zimetumika pale 🤔🤔🤔
 
Sasa yajengwe majengo mengi kama hayo miji iepukane na utitiri wa watu wasio na sehemu maalumu za kifanya biashara...
 
Like ndo solo la 9bills [emoji28][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hata million 1000 hazifiki pale
Tumeshapigwa pale Yani wamesimamisha nguzo wakapiga kenchi na bati ndio 9bilions
 
Wamachinga sasa wanakua wafanya biashara rasmi watakopesheka kama wafanyabiashara wengi sasa hapo shida iko wapi bro Rais Samia Suluhu anaendelea kuupiga mwingi
Inawezekana ukijumuisha na hayo Magali yanayoonekana pamoja na hizo nyumba pemben
 
Aisee huu utawala kweli kuna watu wanalamba asali, yaani ujenzi ule wa soko la machinga ndio sawa na BILIONI 9????.
Hivi kwanini mnamdharau sana sa100 lakini.
Hapo ukute kijumba cha mlizi ni milini 300
 
Soko kubwa ila sio kwa bil 9,
Bil 9 nyingi sana
Wanasahau kuwa kila mwaka wanazaliwa wamachinga wapya, na soko lililojengwa halitoshi hata waliopo.Bilioni 9 bora wangejenga VETA.Sidhani kama kuna kijana anaweza kuwa anamafunzo ya veta akatamani kuwa machinga au bodaboda
 
Acholile Kachola
Tumepigwa Ndugu Ndugu Zangu
 
Mwaka mmoja uliopita agizo la kuwapanga Machinga lilitolewa. Mwaka mmoja baadaye soko la kisasa Dodoma limekamilika limegharimu Tsh Bilioni 9 na sasa limeanza kutumika.

Lengo la soko hilo ni kuwaepusha Machinga na ajali zilizotokana na kufanya biashara pembezoni mwa barabara pia wanarasimishwa, na wataweza kupata huduma za kifedha na kuwa sehemu salama zaidi.

Rais Samia Suluhu amewajali wamachinga.
Siku UPUNGUANI wakuabudu watu ukiwaisha ndio Nchi itapata maendeleo Ila mpaka wajinga mko wengi sana
 
Kuna vumbi sana pale,waweke hata paving blocks,hakafu mle ndani kuna baa na saluni,Je na hao ni wamachinga?
 
Back
Top Bottom