Machinga warejea upya Mwenge

Machinga warejea upya Mwenge

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2016
Posts
6,974
Reaction score
8,750
Pamoja na Kampeni iliyogharimu pesa nyingi ya kuhamisha machinga sehemu maalum. Kwa Sasa wamerudi upya wakiupiga mwingi

newslite1631946850689.jpg
 
Machinga inatokana na neno mutching guy , ni mchuuzi anaetembea kufuata wateja walipo, hasa ukimjengea soko atauza tu kibanda aendelee kutembea ndio maana leo yuko mwanza, kesho kaitwa na wenzake chunya kabeba vitu kariakoo kalianzisha na keshokutwa yuko mwenge au karume ndio maisha yake
 
Sawa na gharama kubwa iliyotumika kujenga stand za mabasi wewe basi linapita halikai muda mrefu weka vyoo vya kutosha na mabafu, jengo la abiria simple, weka garden za kupendeza kwa abiria watakaokaa kidogo hapo na kula na kunywa, imarisha usafi weka fence simple, yanakopaki na kupita magari weka zege au paving imara kesi kwisha maofisi wawekee vikontena na kituo cha polisi simple mabilioni ya kujenga magorofa ya nini?
 
Sawa na majengo ya masoko ya ghorofa utamaduni wa mtanzania hapendi kupanda magorofani anaona usumbufu kwanza hivo masoko yanageuka kua magofu tu
 
Machinga inatokana na neno mutching guy , ni mchuuzi anaetembea kufuata wateja walipo, hasa ukimjengea soko atauza tu kibanda aendelee kutembea ndio maana leo yuko mwanza, kesho kaitwa na wenzake chunya kabeba vitu kariakoo kalianzisha na keshokutwa yuko mwenge au karume ndio maisha yake
Mutching? Hilo neno ndio mara yangu ya kwanza kulisikia na sidhani kama ni neno la english.

Hebu check tena vizuri
 
Wewe kinakuuma nini? Mwanaume mzima unakuwa mbeya mbeya. Sasa hivi tunawaza vita vya Ukraine na bei ya mafuta wewe unawaza umbeya tu. Acha watu watafute maisha. Unataka wawe panya road.
 
Back
Top Bottom