KERO Machinjio ya Manispaa ya Moshi hayana hadhi kiafya kwa Mifugo na Wakazi maeneo yanayoizunguka

KERO Machinjio ya Manispaa ya Moshi hayana hadhi kiafya kwa Mifugo na Wakazi maeneo yanayoizunguka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Muda mwingi mifugo wanakaa juani. Hakuna kivuli cha kuwakinga na jua, ama eneo maalumu la kulishia.

Wanakaa pamoja na kuficha vichwa kwa kujikusanya pamoja, kukwepa makali ya jua.

Pia, mfereji wa maji taka toka machinjioni umeziba na upo wazi kwa miaka na miaka. Eneo la kuchinjia halina uzio, watu huweza kukatisha eneo hilo kama vile kwenye uwanja wa mpira.

Hakuna sehemu maalumu ya kukaushia ngozi, bali hutandazwa chini, ambapo nzi hujazana na kunguru.

Manispaa iboreshe eneo husika kwa faida ya afya za watu na za mifugo.
 
Back
Top Bottom