Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Eneo la Machinjio ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mkoani Songwe kuna Daktari wa Mifugo ambaye jukumu lake ni kukagua nyama baada ya ng’ombe kuchinjwa, katika ukaguzi wake amekuwa akiondoa sehemu anazodai kuwa hazifai kuliwa na binadamu.
Anaondoa kwa malengo ya kuteketeza lakini badala yake anaingiza kwenye chumba kingine hizo nyama na kuwauzia Wafanyabiashara wa migahawa badala ya kuziteketeza.
Daktari huyo inadaiwa kuwa hana sifa za kazi anayoitumikia amewekwa kwa urafiki na wakubwa fulani, lakini anashindwa kuutumia urafiki uliomfikisha hapo kufanya kazi kwa weledi.
Jambo lingine ni usafi wa mazingira ya eneo husika ni kama hauzingatiwi na watu wanaona ni jambo la kawaida wakati hicho ni chakula ambacho kinaliwa na mamilioni ya watu.
Ufafanuzi wa Serikali ~ DED: Nimeunda timu kuchunguza madai ya michezo michafu katika Machinjio ya Halmashauri ya Tunduma