Ndugu wana jamii Forums waslaam!
nimekuwa na tatizo la macho ambapo hadi sasa ninalazimika kutumia miwani ili kuona mbali kwani baada ya kupima nilibaini jicho moja la kushoto kuwa na uoni hafifu, hivyo nilishauriwa kutumia miwani ili kulinda hili moja la kulia.
Lakini ninashangazwa na macho kutengeneza kama kovu au rangi ya kahawia kwa macho yote mawili ninaomba msaada wenu tafadhali maana ninahisi dalili za muwasho hasa kwenye kope za chini na kupelekea kuyapikicha sana macho.