Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,379
- 41,294
Habari za mchana nyote.
Natumai mmeshapata mlo wa mchana na kama bado basi niwatakie mlo mwema mtakapopata nafasi wa kuubwia.
Naomba nisimulie kile macho yangu yanaona na ubongo unanipa taarifa. Likizo imesha na kazi ndogo ndogo za kuuchangamsha mwaka zimeshaanza. Bado niko ofisi ndoo sijarudi makao.
Hapa ofisini kuna kijana mtanashati tuu mwenye fani yake (nikisema fani namaanisha amebobea kwenye taaluma flani aka certified). Sasa huyo kijana tangu mwaka jana alipofika ofisini alikuwa ananisemesha kwa macho.
Kijana mwenyewe mpolee tuu ila nikipita anavonitazama (nikijikuta nami namtizama kama napita kwenda ofii nyingine) unaona macho yake yanaongea.....
Tangu jumatatu nilivyoripoti kazini, akifika tuu kanakuja kunisalimia, ila haniambiaa shkamoo. Utasikia dada habari ya asubuhi.... sasa mie nasoma macho yake yanavyonianglia akiwa ananitizama......
Sijamwambia mtu yeyote kuhusu hili nikisema hapa basi kinakuwa kimeishia hapa maana kwanza ni mdogo kwangu kiumri sanaa tuu. (hii waliokuja PM na umri kasoro bahari watathibitisha vile niko allergic na umri mdogo aka Ben10.
Ila huwa namjibu na kumuongelesha kawaida tuu akihitaji msaada kama vile sijaona na sifahamu maneno anayoniongelesha kwa macho yake. Nakumbuka wakati niko likizo kuna kazi alikuwa anafanya akahitaji msaada wangu, akaomba namba ya simu akanipigia..... sijui .... lakini nahisi sauti ilimletea shida (usiniulize shida gani).
Nakutana na watu wengi tuu mtaani wanakuongelesha kwa macho ila unapiga ukope unaendelea na safari. Kilichonifanya nilete huu uzi hapa ni kuwa, huyu kijana leo kajitutumua ameomba tutoke wote kwenda kula mlo wa mchana. Nikajikaza nikamjibu kistaarabu kabisa, mdogo wangu leo nna majukumu mengi nisamehe sitoweza na hii ni hadi mwezi uishe siwezi kukuahidi mwezi ujao.
Masikini akasema sawa dada, pole na kazi na kazi njema.
Hivi na nyie huwa mnakutana na watu wanaowasemesha kwa macho??!!
Kasinde