Allah's Slave
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 562
- 46
Asalam Alaykum Waungwana, Naombeni mnisaidie mawazo yenu ili niweze kumrudisha mke wangu aliyeondoka nyumbani yapata mwezi sasa. Tumejaliwa watoto wa wili na ndoa yetu ina miaka 6 sasa. Tulikorofishana nyumbani akaondoka. Mke alikuwa mama wa nyumbani hivo sina hata house girl. Kupika sijui so nawalisha hoteli na junk food wakati wote. Kuwatayarisha waende shule asubui naona kazi nadhani na leo hawatoenda shule. Nahangaika bila mama yao na nimeshajaribu kumfuata kuongea naye imeshindikana. Ramadhani ndo imeshafika hivyo sijui nitafturu wapi. Nimemkumbuka sanaaaaaaa Mke wangu.