MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
NAOMBA UNIJIBU:-
1. Kwanini CCM hawakununua bajaji 200 kupeleka wilayani kwa ajili ya kampeni badala yake tena wakanunua mikonga 200 ? kumbuka mkonga mmoja ni 80 milioni soi kama ccm wangeamua kununua bajaji basi kwenye kila mkonga moja wangepata bajaj 20 kwa bai ya 4ml kwa bajaji, kwahiyo kwenye mikonga 200 wangepata bajaji 4000 na naamini kila balozi angekuwa na yake?
2. Je serekali na ccm ni nani mwenye huwezo, huoni kuwa kama CCM wanaweza kununua mikonga 200, srekali inaweza kununua ambulance 2,000 = (200 x 10 ) na zaidi ikitaka?
vipaumbele ni muhimu katika kutoa maamuzi sidhani kama vipaumbele hivyo vinapangwa hapa JF.
vipaumbele ni muhimu katika kutoa maamuzi sidhani kama vipaumbele hivyo vinapangwa hapa JF.
Mwenye contacts za Dr Slaa na meneja wa kampeni wa Chadema awapelekee haraka hii habari ya mama mjamzito kulia kwenye daladala sababu ya uchungu na hasira ya kuambiwa na Kikwete eti wajawazito watanunuliwa Bajaji. Hii hoja itawaongezea Chadema kura kibao. Huu ujumbe usisitizwe kila kampeni ya Chadema kuanzia dakika hii hadi mwisho wa kampeni. Ujumbe ukishamfikia Dr. Slaa na Baregu na Chadema kwa ujumla tujulishwe jamvini. Ni hayo tu.
mama huyo alikuwa na lake jambo asisingizie ahadi ya usafiri wa bajaj kwa wajawazito.
mama yangu mdogo ni mjamzito na yule kijijini kuna siku nilimpigia simu swali lake la kwanza aliniuliza nasikia Rais katukumbuka wajawazito katika kampeni zake kwa ahadi ya bajaj. mama mdogo ana imani na Rais na kaahidi kumpa kura yake.
Asanteni kwa maoni yenu,hiki ni kisa cha UKWELI kimetokea mbele ya macho yangu,sina sababu ya kukulazimisha uamini na ndio mana hii story sijampa rafiki yangu(mwandishi wa habari)ili aitoa kwenye gazeti,mana wengi mngesema imetungwa.Nina story ya AHADI YA KUNUNLIWA MELI WAKAZI WA ZIWA VICTORIA njinsi walivyoipokea,je wajua kuwa ahadi hii itamnyima kikwete kura kanda ya ziwa?,mana baba mmoja aliyepoteza famila yake (mke na watoto 4) aliniambia "walikuwa wapi miaka 15 yote"?,"mpaka tuwape kura ndio wanunue meli"?,"hana ata huruma na aibu kusema hiyo ahadi wakati huu wa kuomba kura"?,"mi naona anataka KULA sio kura","kwanini wameua reli"?"au wanafikiri hatujui kama wana BOTI na mabasi ya abiria ya kufanya biashara hapa"?,ni stori ya kweli ya kusikitisha jiandae.
Unafaa kuwa mhariri wa magazeti ya udaku, story ya kutunga kuna wengine wataamini. Umejitahidi kuisuma hadi imekaa kama kweli vile.