BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Wapo waliotembea kwa miguu, baadhi yao walitumia baiskeli, wengine walitumia bodaboda, wachache walitumia Ubber na taxi huku wengi walitumia daladala. Lakini wote walishangaa wakitekwa nyara na kupelekwa ambako hawakutarajia kufika! Watoto wao wanahangaika, wake, waume pamoja na wenzi wao wanapatwa na sonona kwa kuwakosa huku mashamba yao, kazi zao, ofisi zao, maduka yao, biashara zao vikivurugika. Madeni waliyokopa Benki na kwenye taasisi mbalimbali za Fedha yanazidi kutunisha riba kwa kukosa marejesho.
Je, unajua aina ya Usafiri walioutumia na hatimaye kufikia hatua ya kutekwa nyara? Nitakueleza! Tulia nikujuze! Wapo waliokuwa wanatetea Wagombea wao wasienguliwe na Wasimamizi wa Uchaguzi, wapo ambao walikuwa wanadhibiti kura za Wagombea wao zisiporwe, wapo walioonyesha upinzani mkali katika majukwaa ya kisiasa, wapo waliokuwa wakiendesha vikao vya kimkakati ili Wagombea wao washinde, wapo waliokuwa wakitoa misaada au kuchangia gharama za kuendesha siasa za upinzani, wapo waliokataa kuwachangia wanasiasa wa CCM, wapo waliokataa kuchangia harakati za CCM, nk.
Malengo na mikakati yao vikatekwa nyara. Wapo waliouawa na wapo waliopotea au kupotezwa wasionekane hadi leo. Wengine wakawindwa kama ndege na kukamatwa na kusokomezwa mahabusu. Wapo waliokamatwa usiku, wako waliovamiwa mashambani na wapo waliokamatwa njiani. Walipewa tuhuma zimazotofautiana kulingana na matakwa ya wakamataji. Wapo waliounganishwa katika tuhuma za mauaji ya kisiasa, wapo waliopewa tuhuma za madawa ya kulevya, wapo waliopewa tuhuma za uchochezi, wapo waliopewa tuhuma za kuhujumu uchumi na kutakatisha fedha, wapo waliopewa tuhuma za kufanya fujo, nk.
Hao ndio mamia ya mahabusu ambao wamejaa katika magereza kama mahabusu kila kona ya nchi. Wachache au kiduchu miongoni mwao wameachiwa kwa dhamana huku wengi wao wakiendelea kusota mahabusu pasipo huruma. Haya yote yanatendeka katika nchi ambayo siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili mamilioni ya watu wake wakiwemo viongozi hufurika katika nyumba za ibada kumuomba Mungu.
Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unafanywa katika nchi ambayo viongozi wake huapa kwa kushika vitabu vya dini. Wakishapoteza watu, wakishaua watu, wakishapora ushindi, wakishawarundika watu mahabusu, huenda kuapa kuwa watasimamia haki katika nchi huku wakishika vitabu vya dini wakishuhudiwa na viongozi wa dini ambao hawawezi hata kufunua vinywa vyao kuwaonya wala kuwakemea achilia mbali kuwatetea wanaonyanyaswa, wanaoteswa na kuporwa haki.
Tunaandika haya ili kuwakumbusha na kuwaonya wenye mamlaka katika uso wa nchi kwamba wasipowaachia huru watu waliosingiziwa, basi hasira ya Mungu itawaka juu ya uso wa nchi. Wanaweza kusoma kitabu cha Nabii Amosi ili kuelewa kwa undani ujumbe huu wa Askofu kwa watawala pamoja na washauri wao.
Mimi nimekwisha kutimiza wajibu wangu (Ezekieli 33:1-20).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki