Machozi ya Baba Askofu Mwamakula kwa Watawala wa Tanzania

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Wapo waliotembea kwa miguu, baadhi yao walitumia baiskeli, wengine walitumia bodaboda, wachache walitumia Ubber na taxi huku wengi walitumia daladala. Lakini wote walishangaa wakitekwa nyara na kupelekwa ambako hawakutarajia kufika! Watoto wao wanahangaika, wake, waume pamoja na wenzi wao wanapatwa na sonona kwa kuwakosa huku mashamba yao, kazi zao, ofisi zao, maduka yao, biashara zao vikivurugika. Madeni waliyokopa Benki na kwenye taasisi mbalimbali za Fedha yanazidi kutunisha riba kwa kukosa marejesho.

Je, unajua aina ya Usafiri walioutumia na hatimaye kufikia hatua ya kutekwa nyara? Nitakueleza! Tulia nikujuze! Wapo waliokuwa wanatetea Wagombea wao wasienguliwe na Wasimamizi wa Uchaguzi, wapo ambao walikuwa wanadhibiti kura za Wagombea wao zisiporwe, wapo walioonyesha upinzani mkali katika majukwaa ya kisiasa, wapo waliokuwa wakiendesha vikao vya kimkakati ili Wagombea wao washinde, wapo waliokuwa wakitoa misaada au kuchangia gharama za kuendesha siasa za upinzani, wapo waliokataa kuwachangia wanasiasa wa CCM, wapo waliokataa kuchangia harakati za CCM, nk.

Malengo na mikakati yao vikatekwa nyara. Wapo waliouawa na wapo waliopotea au kupotezwa wasionekane hadi leo. Wengine wakawindwa kama ndege na kukamatwa na kusokomezwa mahabusu. Wapo waliokamatwa usiku, wako waliovamiwa mashambani na wapo waliokamatwa njiani. Walipewa tuhuma zimazotofautiana kulingana na matakwa ya wakamataji. Wapo waliounganishwa katika tuhuma za mauaji ya kisiasa, wapo waliopewa tuhuma za madawa ya kulevya, wapo waliopewa tuhuma za uchochezi, wapo waliopewa tuhuma za kuhujumu uchumi na kutakatisha fedha, wapo waliopewa tuhuma za kufanya fujo, nk.

Hao ndio mamia ya mahabusu ambao wamejaa katika magereza kama mahabusu kila kona ya nchi. Wachache au kiduchu miongoni mwao wameachiwa kwa dhamana huku wengi wao wakiendelea kusota mahabusu pasipo huruma. Haya yote yanatendeka katika nchi ambayo siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili mamilioni ya watu wake wakiwemo viongozi hufurika katika nyumba za ibada kumuomba Mungu.

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unafanywa katika nchi ambayo viongozi wake huapa kwa kushika vitabu vya dini. Wakishapoteza watu, wakishaua watu, wakishapora ushindi, wakishawarundika watu mahabusu, huenda kuapa kuwa watasimamia haki katika nchi huku wakishika vitabu vya dini wakishuhudiwa na viongozi wa dini ambao hawawezi hata kufunua vinywa vyao kuwaonya wala kuwakemea achilia mbali kuwatetea wanaonyanyaswa, wanaoteswa na kuporwa haki.

Tunaandika haya ili kuwakumbusha na kuwaonya wenye mamlaka katika uso wa nchi kwamba wasipowaachia huru watu waliosingiziwa, basi hasira ya Mungu itawaka juu ya uso wa nchi. Wanaweza kusoma kitabu cha Nabii Amosi ili kuelewa kwa undani ujumbe huu wa Askofu kwa watawala pamoja na washauri wao.

Mimi nimekwisha kutimiza wajibu wangu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Tusishangae tukisikia anatishiwa uhai wake pia kama Baba Askofu Bagonza. Natamani tungekuwa na viongozi wa dini wengi wenye UJASIRI kama hawa wawili pamoja na yule Sheikh Ponda.
Hakika Mwana Kondoo Ameshinda Tumfuate..

Asante Baba Askofu maneno kuntu kwa watawala wetu wenye viburi na vichwa vigumu kama jiwe.
 
Wewe nani humu mpaka uandike upuuzi kama huu? Mbona mmiliki wa Jamii Forums hajalalamika kuhusu haya mabandiko? Kafungue forum yako huko utaweza kuamua nini kiwe posted au kisiwe posted acha kujikweza
Huyu mleta mada ndo mtumishi feki mwenyewe. Hizi story zinaanziaga kwake, na akipotea wiki au mwezi nazo zinapotea.
 
Hata Bhokasa alifanya zaidi ya haya na sasa hivi hana uwezo wa kuyafanya tena.
 
Reactions: BAK
Usingekua fake ungetumia verified user name. Huna haki ya Kuwait’s wengine fake.
Vyote ni feki, mada feki, huyo askofu feki,mleta mada feki hata mimi ni feki. Kama sio feki uliwahi kuona waraka zake popote verified Kama gazetini!? Huwa zinaletwa JF tu na mtu yuleyule feki.
 
Anatumia uhuru wake wa kikatiba kutoa maoni yake. Na huo pia mtaupindisha kama mlivyopindisha katiba kwingine kote!
 
Sasa kama mada ni fake kwanini upo kwenye huu uzi MPUUZI wewe? Tafuta mada ambazo si fake ili uachane na hii mada fake.
Vyote ni feki, mada feki, huyo askofu feki,mleta mada feki hata mimi ni feki. Kama sio feki uliwahi kuona waraka zake popote verified Kama gazetini!??, Huwa zinaletwa JF tu na mtu yuleyule feki.
 
Rais, wabunge na madiwani wote feki, bunge feki serikali fake.
Sawa, Ila hilo haliondoi ufeki wa huyu mtumishi hewa. Hanaga impact yoyote zaidi ya kuleta maandiko Jamii Forums tena usiku usiku. Ana misemo yake ya kujipa matumaini, eti mwanakondoo ameshinda. Ukimuuliza hajui hata anamuongelea mwanakondoo gani!?
 
Sawa, Ila hilo haliondoi ufeki wa huyu mtumishi hewa. Hanaga impact yoyote zaidi ya kuleta maandiko Jamii Forums tena usiku usiku. Ana misemo yake ya kujipa matumaini, eti mwanakondoo ameshinda. Ukimuuliza hajui hata anamuongelea mwanakondoo gani!?
Tatueni matatizo yenu ya pesa kwanza. Beberu amekataa kuitambua serikali fake na haleti misaada. Hivi karibuni mtaweka kodi ya oxygen kila raia alipie.
 
Reactions: BAK
Ungekuwa na robo tu ya reasoning capacity yangu usingekuwa mpumbavu kiasi hiki.
Wewe reasoning capacity yako ipo chini sana. Ndo maana unaleta maandiko feki.
 
Wewe unayetaka watu wasijadili kuhusu Nchi yao au wahame nchi au kunywa sumu ndiyo unaijua katiba. MPUUZI mkubwa.
Mustakabali wa nchi unaujua wewe!?.. Katiba unaijua!?.. narudia tena, upeo wako mdogo sana. Haya elezea maana ya mwanakondoo ameshinda unayowekaga kwenye maandiko yako ya dini feki!?
 
Ungekuwa na robo tu ya reasoning capacity yangu usingekuwa mpumbavu kiasi hiki.
Kama kawaida yako umeanza kuleta tu video twako. Hii style inatumiwaga na watu wasioweza kujitegemea kiakili mpaka atumie video za wengine. We ni mjinga tu.
 
Tusishangae tukisikia anatishiwa uhai wake pia kama Baba Askofu Bagonza. Natamani tungekuwa na viongozi wa dini wengi wenye UJASIRI kama hawa wawili pamoja na yule Sheikh Ponda.
Huwezi kushindana na dola popote duniani. Soma taarifa za Kenya namna mauaji ya viongozi waandamizi yanavyofanyika ndo utajua Tanzania ina demokrasia japo kidogo.
 
Hujui umuhimu wa hiyo video katika hali halisi ya Nchi hivi sasa na hii inasababishwa na UFINYU wa akili yako. Siku ukitia akili kichwani utaelewa tu.

Kama kawaida yako umeanza kuleta tu video twako. Hii style inatumiwaga na watu wasioweza kujitegemea kiakili mpaka atumie video za wengine. We ni mjinga tu.
 
Wewe unayetaka watu wasijadili kuhusu Nchi yao au wahame nchi au kunywa sumu ndiyo unaijua katiba. MPUUZI mkubwa.
Ndo maana nakwambia we mjinga, tangu uanze kujadili au kuleta maandiko yako feki ya dini usiku usiku umewahi kubadili nini kwenye Jamii!?, We ni pingapinga wa kila kitu unajulikana Ila awamu hii tunawakomesha kweli kweli mpaka mpate akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…