1
Amani kwenu Nyote,Na Utukufu kwa Muumba
Yeye Aloumba Vyote,Na Kuvipatia Unyumba
Kwake Vyarudi Vyote,Hata visivyo unyumba
Machozi ya Mkizi,Huoshwa na Bahari
2
Maisha Masikitiko,Mtiririko wa Matatizo
Wakati mwingine Vituko,Utafikiri ni Maigizo
Popote pale Uliko,Uitafutapo tuzo
Machozi ya Mkizi,Huoshwa na Bahari
3
Kili mja ni chake,Imemganda Huzuni
Atafuta kilicho chake.Aondokane na Uduni
Kila mtu na wa kwake,Aso wake wa huzuni
Machozi ya Mkizi,Huoshwa na Bahari