Mack D yuko wapi?

Mack D yuko wapi?

We mungu wangu.. Mja wako.. Nakushukuru Mja wako..

Jamaa namkubali sana.
Jamaa mshkaji sana. Ana roho safi mno. Mkifahamiana hawezi kukupita bila kukusalimia.
 
Unaishi vipi Dizllee!!
Nimezungukwa na wachawi,lakini mkongwe bado sipagawi
Africa natamba,nashine Big Brother kama mwisho mwampamba.
 
Huyu jamaa nilimuuzia audio CD siku moja hapa Posta DSM miaka kama mitatu iliyopita. Mja Wako ni ngoma poa kutoka kwake.
 
Yupo bana na anaonekana yupo vizur tu! Mara nying anapita maeneo ya apa ofcn kwangu karbu kila day
 
Nilimuonaga mitaa ya Ulongoni.ana kampuni ya kuclear mahari bandarini.jamaa ana roho ya kipekee.niliomba lift,alinipita na gari nikiwa na mimba ya miez saba kisha mbele kidogo akasimama akanipa lifti.kipindi hiko ni kama miaka minne iliopita. Sitamsahau yule jamaa.sijui yuko wapi sasa
Kumbe ndio wewe, nipm nikuunganishe naye umpe shukrani hata kwa kuagiza kavitz kupitia kampuni yake.
 
Huyu jamaa yupo anafanya kazi clearing and forwarding, pia ana baa yake nafikiri maeneo ya Kiwalani. Haujapita mwaka niliona alifanya interview kwenye kipindi kimoja cha tv.
Safi sana sio kama wale wanaokula unga kama nyoka
 
Mack D ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop waliokuwa "underrated" sana. Ana mistari ya hatari na anajua kusimulia hadithi kwa kutumia nyimbo. Nimefurahi kusikia anaendelea vyema na maisha nje ya muziki.
 
kuna wimbo alitoa 2011 mwishoni, ulikuwa ni wimbo mkali kwa kweli aliwashirikisha AY na FA, na video ilikuwa nzuri sana pia, sijui kwanini baadhi ya wasanii hata wakitoa nyimbo nzuri hawatambi!
Tatizo nyota, siyo wasanii tu, hata kazi nyingine wewe utajitahidi kila njia lakini kazi bure, wenzio kidogo tu wanatusuwa.

Acha kabisa ukiona maduka yanayouza vifaa vya kurogea hayafungwi basi ujuwe wateja wapo.
 
Back
Top Bottom