Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Hivi ni vitu vitakavyowafanya nyote muone mmepata muda mzuri na kujuana. Mada hizi zitakusaidia kuepuka mada ambazo zitapunguza kasi ya mwanamke kukupenda. Mfano, kumuambia kuwa unampenda mapema sana hata kabla hujamjua vizuri tabia yake na kuamua kama unaweza kuishi naye. Na kwa wale wanaojiona wanadharauliwa na mwanamke mwenye pesa/ aliyefanikiwa itakusaidia akuone wa thamani. Uzuri wa hizi mada unaweza kutumia ukitaka kumjua mtu yoyote kiundani.
Anapenda kufanya nini. Kitu gani kinampa motisha ya kufanya vitu? Kitu gani anapenda kufanya ukiachana na kazi yake? (kwa mimi anayesema anapenda kulala huyo najua hanifai). Pia na wewe umwambie kwa upande wako. Hapo utajua kama huyo mwanamke mtaendana au la, usiangalie uzuri wa mwili ukapuuzia mambo ya muhimu. Lazima uwe na viwango.
Ana malengo gani kimaisha. Angependa awe sehemu gani baada ya miaka mitano? Anajiona nani baada ya miaka mitano? Je, akipata anachokitaka atakua na tabia gani?. Na wewe unampa kwa uchache juu ya malengo yako.
Kitu gani kinamvutia au nani anayemvutia na kumpa motisha. Muulize kuhusu watu wanaomvutia na kwanini au nchi/mkoa unaomvutia na kwanini au hata kitu kinachompa motisha ya kuamka asubuhi na kwenda kazini. Pia na wewe unampa vya upande wako.
Anaogopa nini kwenye maisha. Kuna mwanamke nilikua naye, yeye aliniambia anaogopa na anaona hastili kupendwa. Nikajua kabisa sitoweza kuwa naye, siwezi kuwa mwokozi wake wa anachokiogopa, na nikajua hatoweza kujitoa 100% kwenye penzi letu kama anaona hastahili. Na wewe unaweza kumwambia kwa uchache kuhusu unavyoviogopa.
Ila usikae kuuliza tu maswali, utajibiwa kiufupi. Njia nzuri ni kutangulia kutoa stori fupi inayoelezea kile unachotaka kuzungumzia kisha muulize na yeye. Mfano, kama unataka kuwa dokta mkubwa, tafuta stori fupi inayoelezea furaha uliyonayo kusaidia watu, au kama unavutiwa na CR7, tafuta stori inayokuhusu wewe jinsi CR7 anavyokupa motisha kwenye maisha yako na kwanini au unakisema unachokiogopa katika stori na sio moja kwa moja kuwa unaogopa kusemwa na watu vibaya. Hapo utajua mwanamke uliyenaye ana kitu zaidi ya uzuri wake au yupoyupo tu na kama anafikia viwango ulivyojiwekea ili uweze kujenga naye maisha.