Mada: Fahamu mambo mbalimbali kuhusu gari aina ya Subaru Forester

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
3,930
Reaction score
4,912

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU GARI HII
Wakuu rafiki yangu mmoja yupo interested na hizi gari aina ya Subaru Forester lakini kabla hajaingiza maamuzi mzima mzima alitaka kujua yote ya husuyo hizi aina za haya magari.

Stability zake, upatikanaji wa spare na mengine yote ambayo mtu yeyote angependa kuyajua.Huyu jamaa yupo mkoani na amejaribu kuangalia aina hizo hazipo na yeye yupo interested nayo kwa kuwa ni 4DW kulingana na maeneo anayoishi anahitaji mkoko wa namna hiyo.

Kwa kuwa JF inakila aina ya uelewa kwa niaba yake naomba niwasilishe ili apate la kumsaidia kwenye hii issue nzima.
---

UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAU
---
---
---
---
---
---
 
Ana kiasi gani? Kunayo moja if interested PM me.

issue siyo kiwango mkuu yeye anachotaka kujua is the secrecy behind that kwamba ina ubora gani basi na mara nyingi huwa insumbua nini kama tunavyokuwa tunasikia kuhusu Surf;Mitsubish10i, Saloon car kwenye kunywa mafuta inaongoza nk
 
issue siyo kiwango mkuu yeye anachotaka kujua is the secrecy behind that kwamba ina ubora gani basi na mara nyingi huwa insumbua nini kama tunavyokuwa tunasikia kuhusu Surf;Mitsubish10i, Saloon car kwenye kunywa mafuta inaongoza nk

Haya tembelea link hii kupata specifications
 
issue siyo kiwango mkuu yeye anachotaka kujua is the secrecy behind that kwamba ina ubora gani basi na mara nyingi huwa insumbua nini kama tunavyokuwa tunasikia kuhusu Surf;Mitsubish10i, Saloon car kwenye kunywa mafuta inaongoza nk

Subaru forester SF5 engine edition, 2000cc; niliagiza moja mwaka jana from Japan nikaitumia for 6 months; ni gari nzuri sana kama bado iko mpya, ni imara na haisumbui sana; tofauti moja niliyo-note ni katika acceleration system yake (iko tofauti kidogo na toyota makes), pia inapoanza kuchoka au ukichelewa kuifanyia service huwa inachelewa kupokea mafuta kwa sekunde kadhaa wakati wa kuondoka, baada ya hapo huwa inakuwa shwari. Pia ikichoka huwa ina matatizo ya kupokea moto (kuna kitu nilitajiwa nimesahau jina lake) ila hili ni tatizo dogo. Matatizo mengine ni ya kawaida kama gari nyingine yeyote ile (ball joints, tyroid ends - kama unatembelea kwenye rough roads). This car is Full Time 4WD na engine yake ina nguvu sana sana ukilinganisha na RAV4 au HONDA SRV!!

Spare zake kwa sasa ziko nyingi sana hapo mtaa wa Msimbazi (duka moja lipo karibu na Diamond Trust Bank hiyo ya Wahindi) ila ni genuine na za gharama sana kwa kweli (ulinganisha na toyota) hivyo mwambie jamaa ajiandae kwa hilo!! Wa-Kenya wana uzoefu nazo sana manake kwao zimejaa sana ... na almosts parts zote zapatika Nairobi na Dubai (na sasa Dar) ... actually nasikia kenya subaru cars ni nyingi kuliko toyota.

This car was my favourite kwa kweli nilipotaka ku-enjoy barabara na kutunishiana misuli na magari makubwa like Toyota VX, Nissan Patrols kwani Subaru Forester zinachanganya haraka sana na zinachomoka balaaa! At one instant nilitumia less than 1 minute kufika 140km/hr. Usipokuwa mwangalifu ni rahisi sana kuuonja umauti!!!!

Karibu ujaribu kitu tofauti.
 
Subaru forester SF5 engine edition, 2000cc; niliagiza moja mwaka jana from Japan nikaitumia for 6 months; ni gari nzuri sana kama bado iko mpya..

Mkuu nashukuru kwa ushauri ambao kwa kweli umeelezea uzoefu wako najua gharama za spare zake zitakuwa sawa na za Suzuki kama baadhi ya watu wasemavyo.

Mkuu kwa nini uliamua kuuiza baada ya miezi sita?
 

Mkuu nimecheka sana. Kuna siku nilikua naelekea Iringa nikitokea dar niko na Rav4. jamaa alikua na hii gari (subaru forester) nilijaribu kumtunishia misuli. Nilibaki kusoma No. tu.
Nimeukubali kweli inatembea mkuu
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri ambao kwa kweli umeelezea uzoefu wako najua gharama za spare zake zitakuwa sawa na za Suzuki kama baadhi ya watu wasemavyo.

Mkuu kwa nini uliamua kuuiza baada ya miezi sita?

Rafiki yangu mmoja wa mkoani aliipenda sana sana ... nikaamua kumuuzia. Lakini ukweli pia ni kwamba nina kaugonjwa ka-magari ... huwa sipendi kukaa na gari muda mrefu ... nikikaa nayo sana ni miezi 12 tu!!
 

Subaru's are for people who love cars, people who understand the beauty of perfomance.may be the reason kenyans buy more subarus than we do here in TZ-kenyans are ahead of us education wise and development wise.

I suggest you buy that car and you will never be dissapointed!kuna watu wako tayari kununua Toyota kwa sababu spea bei rahisi,what is the use of a cheap spare part if you need to change it every 3 months?

kwa wanamahesabu,ipi rahisi over time?15,000tshs spare that u will buy 4 times a year or a 35,000tshs that you will buy only once a year?go figure.

anyways,watanzania wachache sana wanapiga hesabu in long term figures,no wonder tuko tayari kununua saa feki 10 kila mwaka for 20,000 lakini ukimwambia mtu atumie 200,000 kununua saa original atakayokaa nayo miaka 10 unakuwa ugomvi.
 
wana jamii wenzangu mimi ni mpenzi sana wa gari inaitwa subaru nataka kununua sasa nataka kujua kama spea zinapatikana hapa tanzania maana kila unaye muuliza anakuambia sio gari nzuri,au spea hakuna,utakufa nayo na mambo kama hayo naombeni msaada,SUBARU LEGACY TX<cc 2000 ENGINE BH 5
 
subaru ni gari nzuri sana,imara na unaweza kutumia ktk motor sports etc.
1-Disadvantage zipo chache sana in East Africa,hivyo basi spares zinaletwa kidogo na bei inakuwa kubwa.
2-Mafundi wa subaru wako wachache ,sababu ni kama hapo juu
3-jiandae kuwa mteja special ktk maduka ya spare na mafundi

ni hayo tu
 
kaka kama unataka kununua subaru..nunua..usiwasiklize sana wabongo watakukatisha tamaa..shida ni kuwa wameshazoea toyota kwa hiyo wengi akili zao zimeganda.

ukishakuwa na subaru akili yako itachangamka na bila shaka utajua ni wapi na kivipi upate spare za bei nafuu!

all the best mkuu..niko nyuma yako lakini mimi napenda zaidi subaru forrester, 4WD with turbo engine
 
Mimi namiliki subaru forester, mwaka wa nne sasa haijanisumbua, kwa sasa spare zipo nyingi, unaweza kuzipata msimbazi street kuna duka lipo opposite na msimbazi eyes center na pembeni yake kuna akiba commercial bank au used spare kuna duka ilala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…