Mada: Fahamu mambo mbalimbali kuhusu gari aina ya Subaru Forester

All in all Subaru ni gari makini sana. Haitaki mafuta ya kuunga unga. Ni gari ambayo kama kweli we ni mpenzi wa magari unapaswa kuwa nayo. Handle with care and it will NEVER disappoint you. Kuna jimbo moja Marekani (nimelisahau) polisi wake wanatumia Subaru kukimbizia wahalifu wa barabarani.

Hiyo gari ni makini sana. Ukitembelea kwenye page ya subaru you tube utakuta wameelezea kwa uhalisia technicalities zao kwa nini wanatumia technology wanayotumia na faida zake. Boxer engine is their one among many tech wanazotumia na ni engine bora sana kwa sasa kwenye ulimwengu wa magari
 

Hapo nakuunga mkono asilimia 100. watanzania wengi wanaangalia gharama ya mwanzo, na bila kujali gharama zitakazokuja baada yake.

Nakumbuka mwaka jana niliagiza Carina Ti, niliendesha miezi miwili nikaenda kubadilisha tyrod na ball joints, tangu siku hio nikasema sitanunua toyota tena. Toyota kwa tanzania ni ugonjwa wa moyo, kila unapopark unakuwa roho juu, mpaka watu wanaishia kujaza maribit, na mavyuma kibao kuzuia wezi.

Nilikuwa na Mazda MPV, nalipark popote na hata vioo sikuandika namba....Nilitumia mwaka mzima, sikuwahi kubadili hata kifaa kimoja... Same applies to Nissan Cars...Kubadili spare ni historia.

Speaking of Saa za bei ghali, mwaka 2006 Nilinunua ESPRIT watch kwa bei ya ajabu, lakini hadi leo ninayo hiyo saa na haina scratch hata moja na nimebadili battery mara moja tu almost miaka mitatu iliyopita...
CHEAP IS EXPENSIVE.
 
Habari zenu wana JF. Nina dream za kununua gari aina ya Subaru Forester nimetokea kuipenda sana gari hii.

Msaada wa ushauri toka kwenu ni kwamba nahitaji kujua gari inatumia Lita 1/how many Kms, spare parts zinapatikana kiurahisi, Nini umadhubuti wake, ni vipuri gani huwa vinasumbua mara kwa mara na vinapatikana?

Kwa heshima na taadhima naomba msaada wenu ndg zangu
 
Gari nzuri kama huwazi km/l, spea ni gali kama umezoea kunua za corola, kama mtu wa tungi achana nayo kwani "used parts" zake ni gali.
 
CYBERTEQ OLESAIDIMU Kaizer MANI mnahitajika huku...
 
Last edited by a moderator:
Ka gari hiyo inabidi asiwaze mafuta maana sio economy kwa watu wa hali ya chini..sema ina turbo charger na maspeed ya kufa mtu so barabarani huonewi. Spare parts zipo za kumwaga na ukifunga ndo unasahau sio kama corolla ila pia ni bei ghali kidogo.

Kiufupi kwa mtu mwenye kipato cha kueleweka haimsumbui. RRONDO nimekuja kiongozi
 
Last edited by a moderator:

asante kaka nilijua mkija hapa mwenzetu huyu atapata ushauri makini,kazi kwake.
 
Asante brother kaizer ushauri nimeupenda sana
 
Last edited by a moderator:
Ni gari zuri nimetumia sasa mwaka WA tatu.ni very durable haliaribiki hovyo kama magari ya Toyota spea kwa sasa zipo nyingi Tu na speed kiboko
 
RRONDO nimekusikia kaka!!!!

Mengi yamesemwa na wadau tayari, ni gari haswa kama "anaiweza" spea kwa sasa ni nyingi sana na mafundi wapo!!!!!

Kama nakumbuka vizuri kwenye facebook wana group ya subaru fans kama sio owners so huko anaweza kupata mengi zaid kwa experience ya waliozitumia!!!!!

Ila najua perfomance yake ni baab kubwa sababu nimeshakutana nazo road na kwa kweli nilikubali mziki wake!!!!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu i have this car kwa muda wa wiki tatu sasa ni very comfy, na spare zipo tu hata mwenge pale eg. Oil filter yake nimenunua 8000/- na vitu vingine sio ghali kiivo! Pia mafuta sio mbaya sana though yangu ni non turbo charger! From dar to iringa around 500km nimetumia less that 45ltrs! Jus try it its real comfidence in motion


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Poa kaka hiyo ni model ya 2005 ila hata 2004 si mbaya


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…