Mada fikirishi kuhusu ndoa

A Peculiar people

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
612
Reaction score
773
Natumai mnaendelea vyema wadau.

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu. Uzi huu unahusu sawa zima la ndoa.

Kwa miaka mingi ndoa imekuwa ni kitu cha kuheshimika au heshimana wengi wetu tunaona ndoa kama ndio msingi wa familia.

Lakini ni wapi kwa kizazi hiki tumekosea kiasi kwamba kumekuwa na maumivu mengi, malalamiko na hadi wengine kufikia uamuzi wa kuto kama kama na kuolewa. Ili hali tunaona ndoa ambayo inatengeneza familia ndio chanzo cha malezi bora kwa watoto.

Ni wapi haswa tunapokosea?

Je, ni sahihi kuendelea kuandaa kizazi cha watoto ambao wengi wao ni wanalelewa na single mother au single father?

Nawasiliasha ndugu zangu.
 
Mi Binafsi yangu, naona ungekua Bora Kila mtu angejitimizia mahitajia yake.
Maana Wanawake wanajiona ni wamaana sana, Kila Kitu wao wanajua na wao ndo Wana akili ya Kila Jambo, kwa mtazamo wangu ndo Bora isingekuepo.
Kila mtu ashike mambo yake na Akutimizie mahitaji yake.
 
Ndoa kweli ni kitu cha kuheshimika
makosa ni pale tunapoacha msingi unaojenga ndoa, msingi huo ni Mungu ambaye ni mwazilishi wa ndoa ili tuzae tuongezekee.
Na akaweka mambo mawili yanayowahusu wanandoa
1. MUME - Kumpenda mkewe
2. MKE - KUMTII muwewe

Kila mmoja akisimama katika nafasi yake vizuri haya tunayoyaona na kuyasikia yasingekuwepo.

Wazazi wetu wakati wanaolewa walikuwa wanalia wemgine hata vichwa kuinua hawakuweza walifunzwa na kujua wanachokiendea lakini ni tofauti sana na sasa
 
Ndoa ni mkataba wa maisha ambao ushapitwa na wakati. Haiwezekani taasisi ya familia ika-survive kwenye gender liberalism tunayoiishi sasa hivi kwa sababu familia kwa asili yake ni conservative institute
 
Oa mkuu acha janjajanja na visingizio.

Mkuu sababu zipo nyingi sana na sio kila sababu ipo kila ndoa au kila mtu. Huyu ana hili huyu anali ili mradi.

Sasa hivi mimi nina imani moja tu kuhusu ndoa. “Ukitapata gubegube lako la kusogeza nalo siku mkisubiri mauti oa au olewa nalo ili mradi tu litaweza kukuvumilia mapungufu yako na wewe uweze kuvumilia ya kwake”

Kwa dunia ya sasa ni kupata mtu atakae match mifumo yenu ta maisha na imani zenu juu ya uendeshahi wa taasisi ya ndoa hata kwa asilimia 50 inatisha. Mengine mtakua napigana mnasameheana mnasogeza siku
 
Huko tuendako hali ni ngumu zaidi si kwa wanawake si kwa wanaume
 
Vijana wakiachana na mawazo ya kupata mwenza wa kusaidiana maisha na ku-stick kutafuta mama walezi wa watoto wao taasisi itarudi ktk ubora wake.

Tafuta leo aliyeoa mama wa nyumbani na aliyeoa mfanyakazi utaelewa nachomaanisha hapa.
 
Vijana wakiachana na mawazo ya kupata mwenza wa kusaidiana maisha na ku-stick kutafuta mama walezi wa watoto wao taasisi itarudi ktk ubora wake.

Tafuta leo aliyeoa mama wa nyumbani na aliyeoa mfanyakazi utaelewa nachomaanisha hapa.
Hao wakina mama wa nyumbani nao wanaangalia tv uko wanaowaona wakina joyce kirya. Wana mashoga zao mtaani ishu ndogo tu utasikia achana nae mgawane mali ufanye maisha yako mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…