Mada Fikirishi: Unamchukulia vipi mtu ambaye hataki ufanikiwe?

Mada Fikirishi: Unamchukulia vipi mtu ambaye hataki ufanikiwe?

plan z

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
1,394
Reaction score
1,434
Kama kichwa kinavyojieleza, huyu anaweza akawa mfanyakazi mwenzako, ndugu yako, mzazi wako au mtu wako yeyote wa karibu ambaye hata ukimkwepa na kumpuuza bado yupo tu kwenye life lako hivyo inakuwa hakuna namna.

Wakati mwingine hata mke au mme n.k n.k

Ukiweka plans zako ukaanza kuzitekeleza unakuta unawekewa pingamizi na watu wa namna hiyo, unaamua kukeep going no matter what, still raia waivyo ndo wanazidi kukuwekea vikwazo au fijisu mbalimbali kwa namna yeyote ile usisonge, muhuni unaamua kukomaa hivyohivyo kibishi, bado raia zinazidi kukaza uzi, raia zingine zinaamua kukuloga, hapo muhuni unaamua kuokoka na kuanza maombi au kwenda kuzindikwa, still raia nao wanazidi. Wanataka uishi maisha ya chini ili wakucheke, wakuseme au wakufanye mtumwa wao, ndiyo raha yao.

Yani hawa raia wakiona tu unaelekea kutoboa wanakuwa kama wachawi vile utafikiri ndugu zake shetani. Wasione tu unapata mpenyo.

Nadhani mshaielewa hii situation. Sasa wadau mada hii napendekeza itumike kushusha nondo tushirikishane mbinu mbalimbali za kudeal na hao raia, maana kuwauwa haifai tutafungwa jela.

 
Nafikiri mafanikio yanaanzia ndani yako, ukiwa na bidii tena mwenye nidhamu hakika lazima utafikia malengo yako.
Kushindwa kunaanzia kwenye mawazo yako.
 
sina muda na mtu anayechukia / hataki maendeleo yangu, nikiamua langu nafanya langu na moyo wangu haijalishi unachukia hajalishi unataka au hautaki. jambo langu ni langu

shinda mechi zako.
 
Wakuu shusheni nondo, shusheni nondo.
 
Back
Top Bottom