Mada: Je, mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari unaendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi?

Mada: Je, mchakato wa kuhakiki taarifa kwenye vyombo vya habari unaendana na kasi ya kuenea kwa taarifa potoshi?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
706
Reaction score
1,230
Wakuu,

MJADALA (3).jpg


Dunia ya sasa ipo kiganjani mwako, lakini je, kila unachokisoma au kusikia ni cha kweli?

Shiriki nasi katika Mjadala wa "Mchakato wa Kuhakiki Taarifa Kwenye Vyombo vya Habari, Unaendana na Kasi ya Kuenea kwa Taarifa Potoshi" kupitia Instagram Live ya JamiiForums.

Mjadala huu utaongozwa na mwandishi wa habari, Imani Luvanga, wazungumzaji ni Nuzulack Dausen wa Nukta Africa pamoja na Mpoki Thompson, Mhariri Mkuu Mwananchi Communication.

Usikose kujiunga nasi Machi 30, 2026, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku

Karibu!

=====

Karibuni kwenye mjadala, muda ndio umewadia, Tutakuwa Live Instagram, kupitia kurasa rasmi ya JamiiCheck, Instagram, na kupitia Jukwaa hili, kila kitu utakipa.

Karibuni sana tushiriki mjadala pamoja.


TUPO LIVE KUPITIA JAMIICHECK!!! 🔥📌🔨

Jiunge nasi kupitia Instagram Live ya JamiiCheck kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku katika mjadala wa “Mchakato wa Uhakiki wa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari unaendana na kasi ya kuenea kwa Taarifa Potofu?” ambapo tutajadili nafasi ya teknolojia, changamoto pamoja na mbinu zinazotumiwa na vyombo vya habari katika kupambana na taarifa potoshi.

Kushiri Bofya Instagram

----------

Mpoki Thomson - Mhariri Mkuu, Mwananchi :
Kuhakiki Taarifa ni pale ambapo unatakiwa kuhakikisha taarifa unayoipeleka kwa umma au walaji ni sahihi na haina upotoshaji wa aina yoyote.

Taarifa Potofu, kwa ujumla wake inaweza kutumika kwa njia hasi zaidi, kwa tasnia ya Habari ni pale ambapo mtu anaandika taarifa au anachapisha taarifa ambayo haijahakikiwa na inaweza kupotosha umma.

Kuhusu kuhakiki taarifa naweza kusema kuwa Mchakato wa Kuhakiki taarifa katika Dunia ya sasa ya Kidigitali kwenye Vyumba vya Habari hauendani na mazingira ya ‘Media’ zetu. Mambo yanaenda kwa haraka sana sasa, hali hiyo inakuja na mabadiliko yake pia, ndiyo maana kuna mambo mengi yanaenda kwa umma kisha baadaye ndiyo yanakuja kufanyiwa uhakiki.

1774887597741.png
Uhakiki wa Taarifa unatakiwa kufanyika kabla ya Habari au taarifa yenyewe kwenda kwa umma, kwa sasa mara nyingi imekuwa tofauti na ndio maana watu wengi wamekuwa wakijutia kwani taarifa zinaenda kwa umma kisha baadaye ndiyo zinahakikiwa.


Nuzulack Dausen - CEO Nukta Africa:

Vypmbo vya habari vimenuifa na mabadiliko ya kidijitali na vimeathirika hivyo hivyo, hasa kwa nyakati hizi ambazo kuna uandishi wa habari wa kiraia ambapo mtu mmoja anaweza kuwa anamiliki chombo na kufanya kila kitu chenyewe hali inayofanya kuwa dhaifu kimfumo na kufanya kuwe na tatizo la kuhakiki taarifa

Kila chombo kinataka kuwa cha kwanza kuweka habari na hii imeshuka mpaka kwa wananchi ili kupata views kwa hiyo kabla ya kuhakiki mtu anakwenda tu,

1774887519062.png

Kwa sasa kuna kuenelea kwa sababu vyombo vingi vimekuwa na chuma cha kuhakiki habari,

Baadhi ya vyombo vya habari vya mtandaoni (Jeshi la mtu mmoja) kuna muda wanaamua tu kutwst kichwa cha habari tunaita click belt, kwa ajili ya maokoto, unaweza sikiliza video usikute hata hicho kitu kwenye habari ila sababau ya maokoto anaweza pata labda dola 200

Mambo mengine yanayochangia usambaaji wa taarifa potoshi ni mazingira ya Uchumi, mfano kukosa watu sahihi wa kufanya uhakiki wa taarifa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuajiriau kulipa timu ya kufanya majukumu tofauti-tofauti.

Kasi ya kusambaza taarifa haitakiwi kuvunja ukweli, bora tuwe wa mwisho kwenye kutoa habari halafu ikawa kweli kuliko tukawa wa kwanza halafu tukapotosha.

Siku hizi kwa sababu ya mtandao, hata habari za nje tunaweza kuhakiki, mfano kuna habari kwenye haya mataifa ya nje tuliwatumia email, baada ya masaa sita wakawa wametujibu. Taarifa unaweza kuiona ni ndogo ila madhara yake kwa umma ni makubwa sana, Stori unaweza kuiona ni ndogo lakini ikienda upande fulani ni kubwa na ina umuhimu mkubwa kwa Mtu au Watu wengine. Unaweza kumuharibia Mtu biashara au maisha kwa sababu tu umechapisha ukiamini ni taarifa ndogo na kwamba unataka kuwahi usiwe wa mwisho.

Mpoki Thomson - Mhariri Mkuu, Mwananchi :

Mchakato wetu wa kuzalisha maudhui umekuwa ukibadilika kutokana na ukuaji wa chombo, Sisi tangu 2006 tulikuwa na digital fast, kama una stori ambayo ina maslahi kwa umma basi inaenda kwenye mitandao yetu ya kiamii, sasa hii ilikuja na pressure yake kwa kuwa ilitakiwa kuzingatia suala la uhakiki wa taarifa husika

Mwandishi anapoleta stori kwetu lazima azingatie misingi ya taasisi na ile ya Uandishi wa Habari. Inapotokea kuna mabadiliko lazima yafanyike kulingana na aina ya kile ambacho kinatakiwa kwenda kwa umma, anachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwa Mhariri au Mtu wake wa Juu kumuelezea alichokutana nacho ili mwisho wake ipatikane taarifa sahihi kwa umma.

Chumba cha Uandishi ndani ya Mwananchi lazima tuwe na ‘Mhariri Mkufunzi’ ambaye anakuwa na kazi ya kuwakumbusha Waandishi wa Habari kuhusu Sera, lengo ni kuwakumbusha umuhimu wa kuwa na taarifa sahihi na zenye ‘impact’ kwa umma.

Wakufunzi hao wanakuwa ni Daraja la kuwafundisha Wanahabari wapya kutoka taasisi za elimu kuhusu umuhimu wa kuwa na taarifa sahihi, kwani Uhakiki wa Taarifa unaendana na takwa la Kisheria, ambapo hapo napo Watu wetu wa Sheria nao wanaingia kusaidia masuala ya Kisheria. Uhakiki wa taarifa unaenda kabisa na matakwa ya sheria, kwa sababu ukipotosha unaweza kufunguliwa kesi, hivyo uhakiki wa taarifa ni muhimu sana

Tunazingatia Vigezo gani hadi Mtu kuwa Mhariri? Itambulike taasisi yetu ni ya Kibiashara, uwezo wa mtu kufanya kazi unaweza kuchangia nafasi yake kwa kuwa kulegeza kamba inamaanisha unaweza kushuka kibiashara pia.

Namna gani mtu anafanya kazi, anawezaje kuongoza timu, anaweza kuinyanyua taasisi, ni sehemu ya mambo ambayo yanazingatiwa pamoja na jinsi ambavyo anaweza kuendana na wakati kwa kuzingatia Sera ya Taasisi.

Ni nadra kukuta bidhaa yoyote ambayo ipo chini ya Mwananchi inakuwa na makosa, hiyo ni kwa kuwa uwekezaji wa kufanya kazi kupitia mifumo ya kuhakikisha taarifa sahihi zinapatikana inazingatiwa.

Jambo lingine la muhimu ni matumizi ya Teknolojia hasa kwa kuwa wakati kama huu kuna Akili Mnemba (AI) inatumika na imekuwa ikitumiwa na wengi kama chanzo cha kupindisha baadhi ya taarifa.


EDWARD CHAINA (Afisa JamiiCheck)
Idara ya JamiiCheck inahusika na mambo mbalimbali ikiwemo kuwajengena uwezo Wananchi katika kutambua taarifa potoshi. Pia, imekuwa ikiwajengea uwezo Watuw a makundi mbalimbali ikiwemo Wanafunzi, Wanahabari na wengineo kuhusu elimu na utambuzi wa taarifa potoshi.

Kuna wakati msimu wa mambo au matukio yamekuwa yakichangiua taarifa potoshi mfano wakati wa Uchaguzi Mkuu, wakati wa usajili au wakati wa mlipuko wa magonjwa. Hapo kumekuwa na matukio mengi ya taarifa zinazoposha. Teknolojia inavyokuwa na pia vyanzo vya upotoshaji navyo vimekuwa vikiongezeka.

Upotoshaji unaweza kutokea hata katika Vyombo vya Habari, hii inawezeka kutokea kwa Wapotoshaji kutumia taarifa za ‘Media’ kupishisha ukweli lakini pia hata Vyombo vyenyewe vinaweza kupotisha pasipo kukusudia.

Teknolojia inavyokuwa inarahisisha usambaaji na ufikiaji wa taarifa nyingi kwa Umma, ndiyo maana JamiiForums ikaleta Jukwaa la JamiiCheck kusaidia Wananchi na Umma wote kwa jumla kutambua kuhusu masuala ya Taarifa Potoshi na jinsi ya kupatra taarifa sahihi.

Kumekuwa na upotoshaji mwingi ambao JamiiCheck tumekutana nao katika sekta mbalimbali ikiwemo masuala ya Dini, Siasa na hata Afya. Mfano, Mtu au Watu wanaweza kuandaa graphics inayoonesha maelekezo ya chombo fulani yanesema hivi au vile wakati uhalisia siyo hiyo.

Upotoshaji kuhusu masuala ya Afya umekuwa ukitokea kwa kiwango kikubwa, na mhusika anapofanya hivyo mara nyingi ni kwamba anataka fedha au anakuwa na lengo lake lingine hasa ni kupata kitu kutoka kwako wewe anayekulenga.

1774889022706.png

Wapotoshaji wengi wanacheza na hisia za Watu, hivyo wanachokifanya mara nyingi wanalenga hisia ili kumfanya mlengwa afanye kile ambacho wanakitaka au amekidhamiria.

Unapopata changamoto zozote za kutokuwa na taarifa tembelea taasisi rasmi au unaweza kutumia majukwaa ya kuhakiki taarifa kama JamiiCheck kupata uhakika wa kile ambacho una mashaka nacho.


MPOKI THOMPSON (Mhariri Mkuu - Mwananchi)
Kila mtu anaweza kuwa ni mchapishaji kwenye Dunia ya Kidigitali, ili kukabiliana na changamoto za kusambaa kwa taarifa za upotoshaji lazima tufanye kazi na Wadau mbalimbali, tunafanya hivyo kwa kushirikiana nao katika mafunzo.

Sisi Mwananchi kuna ‘tools’ nyingi ambazo tunatumia katika kuhakiki taarifa.

Nitoe mfano, hata ilipoanzishwa JamiiCheck tuliona ilikuwa ni jambo nzuri na sisi tulijaribu kufanya japokuwa JamiiCheck wao wamefanya kwa ukubwa zaidi


NUZULACK DAUSEN (Mtendaji Mkuu - Nukta Africa)

Kuna wakati unaweza kupata taarifa kutoka kwa chanzo cha uhakika lakini kumbe chanzo nacho chenyewe kilipotosha katika mazingira ambayo hakikujua kama kimepotosha.

Ni jambo la busara kuomba radhi hata kama hakuna malalamiko kwa kuwa hata kama hakuna malalamiko kuna mtu au Watu wanaweza kuitumia taarifa hiyo katika utafiti, hivyo kuomba radhi kunasaidia marekebisho kwa upande mwingine, japokuwa hilo ni jambo gumu kwa Vyombo vya Habari kuomba radhi.

Una baadhi ya Vyombo vya Habari vimekuwa na Mhariri wa kuangalia kasi (Speed Editor) ambaye kazi yake ni kuangalia nani amekuwa wa kwanza kuchapisha kuliko wao.

Kuajiri mtu kama huyo kunahitaji uwe unajiweza, hiyo inamaanisha kama huwezi kuwa na mtu au watu wa aina hiyo ni vema kufanya kazi kwa kile ambacho unakiweza, nikimaanisha usichapishe taarifa ambayo unajua huna uwezo wa kuihakiki.

Unapochukua taarifa kutoka katika chombo unachokiamini unatakiwa kuhakikisha kabla ya kuchapisha wewe pia jiridhishe usahihi, kwani ikitokea huko ulipochukua taarifa wakabainika kupotosha hata wewe pia utaingia matatizoni. Haijalishi unakiamini chombo kiasi gani, jiridhishe kuwa upo sahihi katika taarifa unayotaka kuichapisha.

Pamoja na changamoto zozote za eneo la tukio siyo kigezo cha kushindwa kuhakiki taarifa, siyo tiketi ya kuchapisha taarifa potofu.


NUZULACK DAUSEN (Mtendaji Mkuu - Nukta Africa)

Tunaona sasa hivi kuna Wanahabari wengi ambao unakuta hajui watu wanaostahili kuwajua katika sekta zao, mfano kujua Katibu Mkuu wa chama fulani au Mwenyekiti wa taasisi fulani, mazingira kama hayo ni rahisi kupotosha pia unapotoa taarifa. Baadhi ya taarifa zinazopotoshwa zinatokana na ombwe la taarifa, ni vema mamlaka zikawa na nafasi ya kutoa taarifa kwa wakati.

Unaweza kukuta taarifa potoshi inatoka sasa hivi inasambaa na Mamlaka zinao uwezo wa kuweka sawa, lakini haifanyi hivyo, inaweza kupita saa kadhaa au siku kadhaa matokeo yake ile taarifa ya awali inasambaa na kuaminiwa na watu.

Mamlaka zinaweka Sheria kukabiliana na mambo yanayoenda kinyume na utaratibu, lakini siyo kila sehemu kunatakiwa kutumia Sheria, kabla ya kufanya hivyo, elimu itolewe.

Serikali iwekeze katika kutoa elimu ili kuwa na mwamko wa watu kutambua jinsi gani watabaini taarifa potoshi na nini cha kufanya, zipo taasisi kadhaa zinazofanya hivyo kama sisi (Nukta Africa) na kuna JamiiCheck.
 
Kuna huyu ndigili Echolima1 alikuwa kutwa kuleta mijengeo ya AI na kwa alivyo mporipori anasisitiza ni taarifa ya kweli utadhani yuko kijijini kwao anawapanga walugaluga wenzake
 
Kuna huyu ndigili Echolima1 alikuwa kutwa kuleta mijengeo ya AI na kwa alivyo mporipori anasisitiza ni taarifa ya kweli utadhani yuko kijijini kwao anawapanga walugaluga wenzake
Ulivyo mjinga na mpumbavu Warabu-koko wenzako huwezi kuwatakia maana wenyewe fake-News mnazijua sana na sasa mmeamua kufichiana Siri lakini sisi tu Naona Post zenu zinazounga mkono ugaidi!!
 
wapo waandishi wa habari hawachuji habari wanaipandisha hewani vile vile alivyoipokea au kuisikia pasipo kuchuja na kusababisha athari kubwa.lazima tasnia iwe na watu wenyee weredi ili kuipasha jamii habari zilizokua na ukweli
 
Vyombo vya habari vya umma ndo vinaongoza kwenye mambo ya upotoshaji, uongo na propaganda, mfano: TBC
 
Wakuu,

View attachment 3563062

Dunia ya sasa ipo kiganjani mwako, lakini je, kila unachokisoma au kusikia ni cha kweli?

Shiriki nasi katika Mjadala wa "Mchakato wa Kuhakiki Taarifa Kwenye Vyombo vya

Usikose kujiunga nasi Machi 30, 2026, kuanzia Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku

Karibu!
Najiunga bando la kutosha kabisa sasa hivi ili 12 net niwe kwenye mjadala, nipate elimu na nichangie mawazo yangu mjadala muhimu kabisa huu
 
Mimi, kwa maoni yangu, ninaona kuwa kuna vikundi vinavyofanya kazi ya kupotosha taarifa kwa makusudi, vikilenga kushawishi mitazamo ya umma na kuunda simulizi fulani za kisiasa. Ndiyo maana, ukifuatilia mwenendo wa matumizi ya majukwaa ya kidijitali, baada ya kufungiwa kwa X, inaonekana baadhi ya vikundi hivyo vimehamishia shughuli zao zaidi kwenye Facebook, ambako kuna wigo mpana wa watumiaji na usambazaji wa taarifa kwa haraka.

Katika suala jingine ambalo ni gumu katika mchakato wa uthibitishaji wa taarifa kwenye vyombo vya habari, ni pale ambapo kunakuwepo taarifa sahihi zenye ushahidi, lakini taasisi au vyombo vya serikali vinazikanusha na kuzitaja kuwa ni za uongo au potofu. Hali hii husababisha changamoto kubwa kwa wanahabari na umma kwa ujumla, kwani huleta mkanganyiko kuhusu ipi taarifa sahihi na ipi si sahihi.
 
Back
Top Bottom