Mada kuu: Matambiko

Mada kuu: Matambiko

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
MADA KUU: MATAMBIKO
1737494079890.jpg

Mada ndogo: KUTEMBELEA MAKABURI.

Somo linaendelea . . .

Makaburi ni makao ya roho za mababu (mizimu) ambao hawajazaliwa tena kwenye miili mipya (reincarnate) na ambao nafsi na roho zao (spirit-soul body) hazijaachana au hazijatengana.

Kwa kawaida, mtu ni roho yenye nafsi vinavyokaa ndani ya umbo liitwalo mwili.

Kwa hiyo, kitendo cha kufa, mwili utengana au huachana na roho yenye nafsi papo hapo.
Pale tunaposema fulani kafariki, maana yake mwili wake ndio umekufa, sio nafsi yake wala roho yake (ambavyo ndiye yeye mwenyewe)

Nafsi ya mtu ni mkusanyiko wa fikra, mawazo, uzoefu na akili zake.
Hivyo mtu akifa, akili yake, fikra, zake, utambuzi wake na uzoefu wake katika mambo mbalimbali, huwa havifi, huwa vinaendelea kuishi, vikiwa vimeshikamana na roho yake.
Huu mshikamano ndio huitwa 'spirit-soul consciusness' ambapo mtu amekufa, lakini bado anaendelea kuona, kuelewa, kutambua kila kitu kinachoendelea kwenye jamii yake.
Hali hiyo huendelea hata pale mwili wake unapozikwa kaburini.
Sasa hiyo 'spirit-soul consciusness' ambayo ndiyo tunaweza kuita 'ghost' au mzimu; katika hali ya rohoni, kwa wale wanaoweza kuona rohoni, uwa wanaona Mzimu huo ukiwa katika hali uliyokuwa nayo kipindi ulipokuwa bado 'umevaa' mwili wake.
Unaweza kuwa mwili wa ujana, utu uzima au uzee.
Kama mtu alikufa akiwa bado kijana basi mzimu wake unaweza kuonekana akiwa katika hali hiyo ya ujana au akiwa mtoto mdogo.
Kama mtu alikufa akiwa mtu mzima, sio kijana tena, basi Mzimu wake unaweza kuonekana akiwa mtoto, kijana au hivyo hivyo alivyokuwa kabla hajafa.
Akifa akiwa mzee anaweza kuonekana katika umbo lake hilo la uzee au ujana au utoto kutegemeana na utashi wa alivyotaka kujifunua kwa watu wa jamii yake.
Mara zote huyu 'marehemu' hujitokeza au hujifununua na kujidhihirisha kwa 'watu wake' katika hali ya ndoto au maono.
Kama sio ndotoni au kwenye maono, basi anaweza kujitokeza mahali popote kwa 'watu wake' akiwa kwenye umbo la kiumbe kingine, kama vile mnyama fulani, mdudu au hata ndege fulani ambaye kwa jamii ya watu wake ni rahisi kumuelewa.
Mathalani, kuna mizimu isipojitokeza kwenye ndoto kama binadamu au mnyama wa kufugwa (hususani ng'ombe, mbuzi, mbwa, kuku nk), basi inaweza kujitokeza waziwazi katika umbo la Nyoka au mdudu fulani nk.
Mizimu mingi sana ya kiafrika hujitokeza mara nyingi kwa watu wake kama wanyama pori; Fisi, Chui, Simba, Ngedere nk. au kama wadudu mfano nyoka, konokono, siafu, mjusi nk.

Kwa hiyo, ni muhimu tuelewe kwamba pale mtu anapokufa na mwili wake kuzikwa, huwa haendi popote isipokuwa kwenye eneo la kaburi alikozikwa, ambapo kaburi lake hutumika kama nyumba yake, ingawa uwa ana uhuru wa kuzunguka zunguka kwenda mahali popote atakapo, sana sana kutembelea ndugu, jamaa na watu wake wa karibu; lakini makao yake makuu ni kwenye kaburi lake.
Ndio maana makaburini, ni mahali pa kiroho, ambapo roho za wafu huishi pale.
Watu wanaokwenda 'kuhiji' kwenye makaburi ya watakatifu wao (wazee wao), uwa wanaenda kuwasalimia na hata kujipatia baraka zao.

Wayahudi kutembelea makaburi ya wazee wao; makaburi ya kina Ibrahim, Isaka na Yakobo na wengineo; au Waislamu kutembelea kaburi la Mtume Muhamad (S.A.W) na 'maswahaba' wa mtume, au Wakristo kutembelea kaburi la Yesu, sio kwamba uwa wanaenda kucheza au kutalii tu, bali wanaenda kuzungumza na wazee wao ili kujipatia baraka; ingawa ukweli ni kwamba, roho za wafu hubaki makaburini, kati ya miaka 4 hadi 600 ambapo 'Spirit - Soul Consciusness' utengana katika kile kinachoitwa 'mind decomposition'.

Mind decomposition ni pale roho ya mtu inapotengana na nafsi yake milele, ili aweze kuendelea na safari kuelekea kwenye chanzo chake (asili yake) au kuzaliwa upya (reincarnation au rebirth)

Mtu aliyekuwa mwadilifu kwenye jamii, akitenda mema kwa watu wengine na kwa viumbe vingine, lakini akafa, katika mazingira tata au ya kuonewa, yaani kabla ya wakati wake, huzaliwa upya ili kulipwa mema na hiyo ndiyo huitwa 'rebirth'
Ndio maana kuna watu (sio wengi sana) huzaliwa katika mazingira mazuri, huishi hata kufa wakiwa kwenye maisha mazuri; wanakuwa hawana historia ya kupitia magumu. Ni kwa sababu wanalipwa malipo ya matendo yao mema waliyotenda walipokuwa katika mwili (before rebirth)
Mtu mwovu, mbaya, aliyekufa bila kulipwa mabaya kama alivyopaswa, huzaliwa tena ili kulipwa haki yake na hii ndiyo huitwa 'karmic reincarnation'

General reincarnation ni kule kuzaliwa tena ili ukamilishe kusudi ambalo ulikufa bila kukamilisha ulipokuwa duniani, yaani kuwa vile maumbile yalivyokutaka uwe.
Hii mada ya REINCARNATION & REBIRTH ni mada pana, tutajifunza kwa kirefu huko mbeleni.

Kwa hiyo unapotembelea makaburi ya watu wako, ujue unaenda kusalimia wazee, watakatifu wako, ili wakupe baraka zao.
Ndio maana yafaa huende na zawadi ambazo ni chakula ambacho wao walikipenda pale walipokuwa hai (walipokuwa kwenye mwili) sana sana ni vyakula vya mazingira waliyoishi, vingi vikiwa vyakula vya asili ya marehemu (mzimu)
Mfano, kama marehemu alikuwa Muhaya, basi atapelekewa vyakula kama ndizi, samaki, nyama, 'ntura', msusa, mnafu, maziwa, senene, kahawa, 'rubisi' na vyakula vingine vya jamii ya Wahaya, alivyopendelea yeye kula, wakati alipokuwa hai.
(Nimeshafundisha jinsi ya kutoa hivyo vyakula kama sadaka, kwenye masomo yaliyopita)
Hiki kitendo cha kutembelea makaburi ya watakatifu wako, ukaongea nao, ukawatolea sadaka na kuwaomba wakusaidie, pia huitwa tambiko.

Kwa hiyo kuna matambiko ya kufanyia madhabahuni kama nilivyokwisha eleza huko nyuma na matambiko ya kufanyia makaburini.

Somo litaendelea . . .

Dr. Magical power (PhD),
Mtafiti na Mkufunzi wa masuala ya kiroho.

NB: Mada hii ya MATAMBIKO inaendelea kwenye madarasa yetu maalum ya Utambuzi, inafundishwa huko 'Enlightenment Class 2' kwa malipo/ ada maalum.
Unaweza kujiunga kwa kuniandikia ujumbe DM
 
MADHABAHU KWA AJILI YA MATAMBIKO.

✍️Kwa wale TU ambao sio Wakristo au Waislam!
(Hadhira izingatiwe)

Tunapoendelea kujifunza kuhusu suala zima la matambiko kwa miungu, wazee, mizimu au watakatifu wetu, kwenye mada ya MATAMBIKO (RITUALS) ili kurejesha mahusiano yetu pamoja nao yaliyovunjika; ni muhimu sana tufahamu kuhusu madhabahu!

Madhabahu ni nini?

Neno madhabahu, limetoholewa moja kwa moja kutoka kwenye neno la Kiebrania 'mizbeah' (;eBzim), likimaanisha "kuchinja."
Kwa kilatini, neno hilo hilo, madhabahu ni 'altārium' likimaanisha "mahali pa dhabihu."
Waswahili huita madhabahu 'altare' wakimaanisha mahali pa kufanyia ibada. Wametohoa mpaka na Kirumi!

Vyovyote iwavyo, madhabahu ni eneo au sehemu au mahali palipowekwa wakfu, yaani kuandaliwa rasmi kwa ajili ya kufanyia matambiko (au ibada) kwa miungu au mizimu ya mababu.

Niwakumbushe tu kwamba hata hizi dini zetu kubwa zinazotambulisha mizimu yao kama miungu iliyoumba dunia, mfano Yehova, Yesu, Allah nk, ukweli ni kwamba hao miungu pia ni watu waliowahi kuishi zamani huko kwenye jamii zao.

Yehova au Yahwe ni wa Kiyahudi, unaomtokea Ibrahim na kujitambulisha kwake kama MUNGU.
Ndio maana hata leo huu mzimu unaitwa Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.

Allah ni mzimu wa jamii ya Waarabu na Yesu ni jina la kisiasa linalowakilisha muungano wa mizimu ya watu wa Ulaya Magharibi.

Hata hivyo, kama nilivyokwisha tangulia kusema huko nyuma, neno mzimu sio tusi, linamaanisha (Ghost) yaani Roho na kila mzimu ni Roho!

Kuna mizimu mizuri (Roho Takatifu) na mizimu mibaya (roho chafu)

Usipojisikia kutumia neno mzimu, unaweza kutumia neno Mungu, ili mradi upate amani tunapoendelea kujifunza mengi kwenye somo hili.
Pengine badala ya kusema Mzimu wa Rugambwa, tumia neno Mungu wa Rugambwa, mantiki inabaki tu ile ile.

Tuendelee . . .

Madhabahu ni mahali pa wewe kukutana au kuwa na faragha na Mungu (Mzimu) wako ambapo unatakiwa kufika mara kwa mara na kumfanyia tambiko (ibada)

Matambiko yanayofanyika madhabahuni, uhusisha sadaka au matoleo ya damu sana sana, lakini pia nafaka, maziwa, kinywaji, uvumba na yanayofanana na hayo.
Kwa wayahudi wao wana mpaka sadaka za chumvi, sadaka za unga, asali, mafuta hata ubani !

Leviticus 2:11-16

"SADAKA YA UNGA iwayo yote itakayosongezwa kwa BWANA isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala ASALI iwayo yote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto."

"Vitu hivyo mtavisongeza kwa BWANA kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.
Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.
Nawe kwamba wamtolea BWANA sadaka ya unga ya malimbuko, utatoa hiyo ngano katika masuke yake iliyochomwa motoni, ngano iliyopondwa ya masuke mabichi, ndiyo utakayoleta kuwa sadaka ya unga ya malimbuko yako.
Nawe utatia MAFUTA juu yake, na kuweka ubani juu yake; ni sadaka ya unga.
Huyo kuhani atauteketeza ukumbusho wake, yaani, sehemu ya ngano iliyopondwa ya hiyo sadaka, na sehemu ya mafuta yake, pamoja na ule UBANI wake wote; ni kafara ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto."

Kwa nini tunatoa sadaka za damu hasa damu za wanyama?

Ni kwa sababu roho zote hupenda harufu ya damu.
Mara nyingi kwenye madhabahu za kiukoo na kikabila, damu ya wanyama hususani ya kondoo, mbuzi au ng'ombe utolewa kwa sababu hapo zamani, wazee hao (mizimu/ miungu) walipokuwa katika miili yao walikuwa wakipenda kula nyama ya wanyama hao, hivyo kuchinja kondoo, mbuzi au ng'ombe, wakati mwingine kuku, ile damu inapomwagika hao wazee katika roho huhisi harufu yake, huhisi uwepo wa nyama, kwa sababu kila kiumbe uhai wake humo kwenye damu yake.
Kuchinja mnyama ni kuutoa uhai wake.
Damu ya mnyama ni uhai wa mnyama husika.
Ukichinja kondoo kama sadaka (dhabihu) basi ile damu yake inakuwa chakula cha Mungu wako na hii ni kwa kila miungu, iwe ya Mashariki, Magharibi au ya kikushi.
Unapotoa sadaka ya nafaka, mfano dengu, kwenye madhabahu basi Mungu hufurahia ile harufu yake.

Ni hivi, miungu yote ni roho (ghosts/ spirits) na haionekani kwa macho ya damu na nyama kama ambavyo hewa, mathalani ya Oksijeni, isivyoonekana kwa macho ya damu na nyama; hivyo kila unachotoa ni vizuri kiwe na harufu kwani wao hula na kunywa kwa njia ya kuhisi harufu!
Ndio maana kila unapokwenda madhabahuni na kutoa dhabihu (sadaka) basi hakikisha iwe katika hali ya 'kunusika'.
Ndio maana ya kuchoma uvumba, ubani au kuchoma nyama ya mnyama (sadaka ya kuteketezwa) nakadhalika.

Unapoenda madhabahuni na sadaka ya kinywaji kwa mfano, basi uwa unatakiwa kumimina ile sadaka (kama ni maziwa labda) ili huyo Mungu wako asikie (ahisi) radha ya harufu ya maziwa hayo.

Miungu/ mizimu uwa inahisi njaa sawa sawa na sisi tunavyohisi njaa, ingawa yenyewe haihitaji kula mara tatu kama sisi.
Lakini, inafaa kulisha mizimu yako angalau kila baada ya muda fulani, walau mara moja kila baada ya miezi mitatu, sita au mwaka mmoja.
Ndio maana zamani watu wa ukoo au jamii fulani walikuwa na desturi ya kukutanika kila mwisho wa mwaka au hata katikati ya mwaka kwa ajili ya kuchinja.
Lengo halikuwa kuchinja, bali kutoa dhabihu ili kulisha miungu/ mizimu!
Hata Wayahudi mpaka leo wanachinja kila mwaka (mwaka wa Abibu) na hiyo kafara ya kuchinja kinachoitwa sadaka za kuteketezwa, ni tambiko maalum kwa Mungu wao YEHOVA!
Waarabu nao wana sherehe zao za kuchinja (Eid el addhā, Eid el fitrí) na lengo la hizo zinazoitwa sikukuu ni kwa ajili ya Mungu wao ALLAH!

Wakristo wao hawachinji, kwa sababu dini yao ni ya kisiasa, wao huchinja 'kiroho' na ndio maana huenda kwa Mungu wao kwa 'damu ya Yesu' lakini ukilinganisha matokeo wanayoyapata wao na wale wanaochinja kiuhalisia ni vitu viwili tofauti.

Assignment:
1. Je, wewe unachinja mara ngapi kwa mwaka na je, unachinjia kwenye madhabahu ipi?
2. Usipokuwa na utamaduni wa kutoa kafara kwa Mungu wako au Mzimu wako, ni wazi hata sasa huyo Mungu (huo mzimu) ana njaa (starvation).
Je, unafanyaje kutuliza ghadhabu yake ambayo ni matokeo ya wewe kumnyima chakula?

3. Orodhesha vyakula muhimu 10 (na vinywaji) ambavyo vinafaa kutolewa kwenye madhabahu ya miungu ya kabila au jamii yenu wakati wa matambiko.
4.
Somo litaendelea . . .

Dr. Magical power
1737493921226.jpg
(PhD)
Mtafiti na Mkufunzi wa masuala ya kiroho!

MADA HII INAENDELEA KWENYE DARASA LETU LA 'Enlightenment Class 2'

Niandikie DM kama unataka kuwa mwanafunzi wangu kwenye madarasa yangu maalum ya ELIMU YA UTAMBUZI.
 
Isaya 26:13-14
Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

Uyu bwana n nani?
 
Kunaendelea kuwa kwa moto.

Huyu anajifanya hamjui muumba wa hayo anayoandika na huyu anataka jamaa aokoke ehehehe 🤣!.
 
Muumba wako

Zekaria 14:9
Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
Mimi Sina bwana mkuu?

Unajua Mungu ni Nan na yupo wapi?
Tuanzie apo kwanza
 
Yaani ulivyosema tu wakristo dini yao ni ya kisiasa,tayari nimeshakuona mtoa mada ni mganga wa kienyeji tu na uzi wako sio wa kuutilia maanani tena,una malengo yako ya kishweitani
 
Ukifa; umekufa. Habari zako zinaishia hapo.
Mwili ni kama jengo, na roho ni kama mwenye mji. Ukiondoka unaacha pagare. Ndiyo maana pale Kinondoni makaburini watu wanashenyentana na wanasepa bila tabu.

Hakuna cha mizimu. Ni mapepo hutumia hiyo njia kuhadaa ili wawatumikishe watu.
Unapokufa unaenda mahakamani ni kujibu kesi. Hakuna dhamana ya kusema urejee duniani ili usumbue raia wanaishi kwa raha na tabu.
 
Mimi Sina bwana mkuu?

Unajua Mungu ni Nan na yupo wapi?
Tuanzie apo kwanza
Mungu wapo wengi ,kuna mizimu ni Mungu,kuna watu ni mungu,kuna wanyama ni mungu ila Muumba ni mmoja na hakuwa huko wengi wanadhan yupo.
 
MADA KUU: MATAMBIKO
View attachment 3209397
Mada ndogo: KUTEMBELEA MAKABURI.

Somo linaendelea . . .

Makaburi ni makao ya roho za mababu (mizimu) ambao hawajazaliwa tena kwenye miili mipya (reincarnate) na ambao nafsi na roho zao (spirit-soul body) hazijaachana au hazijatengana.

Kwa kawaida, mtu ni roho yenye nafsi vinavyokaa ndani ya umbo liitwalo mwili.

Kwa hiyo, kitendo cha kufa, mwili utengana au huachana na roho yenye nafsi papo hapo.
Pale tunaposema fulani kafariki, maana yake mwili wake ndio umekufa, sio nafsi yake wala roho yake (ambavyo ndiye yeye mwenyewe)

Nafsi ya mtu ni mkusanyiko wa fikra, mawazo, uzoefu na akili zake.
Hivyo mtu akifa, akili yake, fikra, zake, utambuzi wake na uzoefu wake katika mambo mbalimbali, huwa havifi, huwa vinaendelea kuishi, vikiwa vimeshikamana na roho yake.
Huu mshikamano ndio huitwa 'spirit-soul consciusness' ambapo mtu amekufa, lakini bado anaendelea kuona, kuelewa, kutambua kila kitu kinachoendelea kwenye jamii yake.
Hali hiyo huendelea hata pale mwili wake unapozikwa kaburini.
Sasa hiyo 'spirit-soul consciusness' ambayo ndiyo tunaweza kuita 'ghost' au mzimu; katika hali ya rohoni, kwa wale wanaoweza kuona rohoni, uwa wanaona Mzimu huo ukiwa katika hali uliyokuwa nayo kipindi ulipokuwa bado 'umevaa' mwili wake.
Unaweza kuwa mwili wa ujana, utu uzima au uzee.
Kama mtu alikufa akiwa bado kijana basi mzimu wake unaweza kuonekana akiwa katika hali hiyo ya ujana au akiwa mtoto mdogo.
Kama mtu alikufa akiwa mtu mzima, sio kijana tena, basi Mzimu wake unaweza kuonekana akiwa mtoto, kijana au hivyo hivyo alivyokuwa kabla hajafa.
Akifa akiwa mzee anaweza kuonekana katika umbo lake hilo la uzee au ujana au utoto kutegemeana na utashi wa alivyotaka kujifunua kwa watu wa jamii yake.
Mara zote huyu 'marehemu' hujitokeza au hujifununua na kujidhihirisha kwa 'watu wake' katika hali ya ndoto au maono.
Kama sio ndotoni au kwenye maono, basi anaweza kujitokeza mahali popote kwa 'watu wake' akiwa kwenye umbo la kiumbe kingine, kama vile mnyama fulani, mdudu au hata ndege fulani ambaye kwa jamii ya watu wake ni rahisi kumuelewa.
Mathalani, kuna mizimu isipojitokeza kwenye ndoto kama binadamu au mnyama wa kufugwa (hususani ng'ombe, mbuzi, mbwa, kuku nk), basi inaweza kujitokeza waziwazi katika umbo la Nyoka au mdudu fulani nk.
Mizimu mingi sana ya kiafrika hujitokeza mara nyingi kwa watu wake kama wanyama pori; Fisi, Chui, Simba, Ngedere nk. au kama wadudu mfano nyoka, konokono, siafu, mjusi nk.

Kwa hiyo, ni muhimu tuelewe kwamba pale mtu anapokufa na mwili wake kuzikwa, huwa haendi popote isipokuwa kwenye eneo la kaburi alikozikwa, ambapo kaburi lake hutumika kama nyumba yake, ingawa uwa ana uhuru wa kuzunguka zunguka kwenda mahali popote atakapo, sana sana kutembelea ndugu, jamaa na watu wake wa karibu; lakini makao yake makuu ni kwenye kaburi lake.
Ndio maana makaburini, ni mahali pa kiroho, ambapo roho za wafu huishi pale.
Watu wanaokwenda 'kuhiji' kwenye makaburi ya watakatifu wao (wazee wao), uwa wanaenda kuwasalimia na hata kujipatia baraka zao.

Wayahudi kutembelea makaburi ya wazee wao; makaburi ya kina Ibrahim, Isaka na Yakobo na wengineo; au Waislamu kutembelea kaburi la Mtume Muhamad (S.A.W) na 'maswahaba' wa mtume, au Wakristo kutembelea kaburi la Yesu, sio kwamba uwa wanaenda kucheza au kutalii tu, bali wanaenda kuzungumza na wazee wao ili kujipatia baraka; ingawa ukweli ni kwamba, roho za wafu hubaki makaburini, kati ya miaka 4 hadi 600 ambapo 'Spirit - Soul Consciusness' utengana katika kile kinachoitwa 'mind decomposition'.

Mind decomposition ni pale roho ya mtu inapotengana na nafsi yake milele, ili aweze kuendelea na safari kuelekea kwenye chanzo chake (asili yake) au kuzaliwa upya (reincarnation au rebirth)

Mtu aliyekuwa mwadilifu kwenye jamii, akitenda mema kwa watu wengine na kwa viumbe vingine, lakini akafa, katika mazingira tata au ya kuonewa, yaani kabla ya wakati wake, huzaliwa upya ili kulipwa mema na hiyo ndiyo huitwa 'rebirth'
Ndio maana kuna watu (sio wengi sana) huzaliwa katika mazingira mazuri, huishi hata kufa wakiwa kwenye maisha mazuri; wanakuwa hawana historia ya kupitia magumu. Ni kwa sababu wanalipwa malipo ya matendo yao mema waliyotenda walipokuwa katika mwili (before rebirth)
Mtu mwovu, mbaya, aliyekufa bila kulipwa mabaya kama alivyopaswa, huzaliwa tena ili kulipwa haki yake na hii ndiyo huitwa 'karmic reincarnation'

General reincarnation ni kule kuzaliwa tena ili ukamilishe kusudi ambalo ulikufa bila kukamilisha ulipokuwa duniani, yaani kuwa vile maumbile yalivyokutaka uwe.
Hii mada ya REINCARNATION & REBIRTH ni mada pana, tutajifunza kwa kirefu huko mbeleni.

Kwa hiyo unapotembelea makaburi ya watu wako, ujue unaenda kusalimia wazee, watakatifu wako, ili wakupe baraka zao.
Ndio maana yafaa huende na zawadi ambazo ni chakula ambacho wao walikipenda pale walipokuwa hai (walipokuwa kwenye mwili) sana sana ni vyakula vya mazingira waliyoishi, vingi vikiwa vyakula vya asili ya marehemu (mzimu)
Mfano, kama marehemu alikuwa Muhaya, basi atapelekewa vyakula kama ndizi, samaki, nyama, 'ntura', msusa, mnafu, maziwa, senene, kahawa, 'rubisi' na vyakula vingine vya jamii ya Wahaya, alivyopendelea yeye kula, wakati alipokuwa hai.
(Nimeshafundisha jinsi ya kutoa hivyo vyakula kama sadaka, kwenye masomo yaliyopita)
Hiki kitendo cha kutembelea makaburi ya watakatifu wako, ukaongea nao, ukawatolea sadaka na kuwaomba wakusaidie, pia huitwa tambiko.

Kwa hiyo kuna matambiko ya kufanyia madhabahuni kama nilivyokwisha eleza huko nyuma na matambiko ya kufanyia makaburini.

Somo litaendelea . . .

Dr. Magical power (PhD),
Mtafiti na Mkufunzi wa masuala ya kiroho.

NB: Mada hii ya MATAMBIKO inaendelea kwenye madarasa yetu maalum ya Utambuzi, inafundishwa huko 'Enlightenment Class 2' kwa malipo/ ada maalum.
Unaweza kujiunga kwa kuniandikia ujumbe DM
NIMEPATA MASWALI MENGI SANA.
ILA INASIKITISHA SANA MADA HIZI.
 
Umeandika mengi mazuri, mengi ya ukweli, na machache au mengi ya uongo.

Truth mixed with untruths and half thruths, lakini si mbaya sana. Labda si kwa makusudi. Kwa ujumla nimependa andiko lako.

Mizimu kukaa makaburini si sawa sawa, kwanini wakae huko?? Labda kama marehemu yuko traumatized sana hataki kuuacha mwili wake, vinginevyo sioni ni kwanini mzimu ukae kaburini!

Pili wengi wanaokufa huwa wanakamatwa kijanja na kupewa miili mingine ili warudi duniani haraka haraka, kwahiyo ili mtu awe mzimu KUNA NAMNA hapo katikati.
 
Nguvu ya kujua...
 
Mungu wapo wengi ,kuna mizimu ni Mungu,kuna watu ni mungu,kuna wanyama ni mungu ila Muumba ni mmoja na hakuwa huko wengi wanadhan yupo.
Mbona Bado ujanijibu zaidi ya kutoa maelezo 🤷🏽‍♂️
 
Umeandika mengi mazuri, mengi ya ukweli, na machache au mengi ya uongo.

Truth mixed with untruths and half thruths, lakini si mbaya sana. Labda si kwa makusudi. Kwa ujumla nimependa andiko lako.

Mizimu kukaa makaburini si sawa sawa, kwanini wakae huko?? Labda kama marehemu yuko traumatized sana hataki kuuacha mwili wake, vinginevyo sioni ni kwanini mzimu ukae kaburini!

Pili wengi wanaokufa huwa wanakamatwa kijanja na kupewa miili mingine ili warudi duniani haraka haraka, kwahiyo ili mtu awe mzimu KUNA NAMNA hapo katikati.
Mkuu sisi uku ndo tumemezeshwa wapendwa wetu kuwaita mzimu ila wwnzetu rangi nyeuPe wapendwa wao wanawaita watakatifu
 
mkuu umesema kuna mizimu mizuri na mibaya..elezea kidogo hiyo mizimu mibaya ni ipi na mizimu mizuri ni ipi na utajuaje kwamba huu ni mzimu mbaya au mzuri na pia vp ukiwa unataka mambo mazuri lakini kwenye kuomba mizimu ukaomba mizimu mibaya je,matokeo yatakuwaje ? kwanza tujuze hiyo mizimu mibaya na mizuri kwa sifa zao na namna ya kuwaepuka na je,mzimu anaweza kuombwa kila kitu au chochote tu au utuomba kitu specific hasa kile alichokiishi yeye au alichofanikiwa nacho alipokuwa dunianai mfano mzimu alikuwa mfabiashara enzi zake lakini ww ukaenda kumuomba kuhusu shughuli zako za ufundi iwe uashi au mechanics utatoba kweli je,ni lazima unachokiomba kwa mzimu kiwe kiliwahi kuwa katika njia yake alippkuwa duniani.?
 
Yaani ulivyosema tu wakristo dini yao ni ya kisiasa,tayari nimeshakuona mtoa mada ni mganga wa kienyeji tu na uzi wako sio wa kuutilia maanani tena,una malengo yako ya kishweitani
lkn ukifatilia historia ya uanzishwaji wa dini ya kikristo naweza kukubaliana na mwandishi.
yesu alikuwa ni myahudi, je wanaomfuata yesu kwanini sio wayahudi kama yesu?

walianzisha dini inayoitwa ukristo wanadai wanaishi na kufuata miiko ya yesu, je kwanini hawafuati dini yake?

swala lingine linalofanya niamini ukristo ni dini ya kisiasa ni namna ilivyochipua. kihistoria urumi ndio ulikuwa ufalme wenye uchafu mwingi sana wa kimaadili, ki utu na kitamaduni, je kwanini waliamua kuitumia dini ya ukristo kuinusuru dola yao ambayo ilikuwa inakufa?

dini ya uyahudi na hinduisim ndio dini kongwe zaidi duniani, maandiko yake yapo toka enzi na enzi na hayabadiliki, je kwanini maandiko ya bibilia yamekuwa yakibadilika na kurekebishwa mara kadhaa? kwanini baadhi ya vitabu vya enzi katika biblia vimekuwa vikiondolewa katika mtililiko wa biblia?
 
Back
Top Bottom