Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
MADA KUU: MATAMBIKO
Mada ndogo: KUTEMBELEA MAKABURI.
Somo linaendelea . . .
Makaburi ni makao ya roho za mababu (mizimu) ambao hawajazaliwa tena kwenye miili mipya (reincarnate) na ambao nafsi na roho zao (spirit-soul body) hazijaachana au hazijatengana.
Kwa kawaida, mtu ni roho yenye nafsi vinavyokaa ndani ya umbo liitwalo mwili.
Kwa hiyo, kitendo cha kufa, mwili utengana au huachana na roho yenye nafsi papo hapo.
Pale tunaposema fulani kafariki, maana yake mwili wake ndio umekufa, sio nafsi yake wala roho yake (ambavyo ndiye yeye mwenyewe)
Nafsi ya mtu ni mkusanyiko wa fikra, mawazo, uzoefu na akili zake.
Hivyo mtu akifa, akili yake, fikra, zake, utambuzi wake na uzoefu wake katika mambo mbalimbali, huwa havifi, huwa vinaendelea kuishi, vikiwa vimeshikamana na roho yake.
Huu mshikamano ndio huitwa 'spirit-soul consciusness' ambapo mtu amekufa, lakini bado anaendelea kuona, kuelewa, kutambua kila kitu kinachoendelea kwenye jamii yake.
Hali hiyo huendelea hata pale mwili wake unapozikwa kaburini.
Sasa hiyo 'spirit-soul consciusness' ambayo ndiyo tunaweza kuita 'ghost' au mzimu; katika hali ya rohoni, kwa wale wanaoweza kuona rohoni, uwa wanaona Mzimu huo ukiwa katika hali uliyokuwa nayo kipindi ulipokuwa bado 'umevaa' mwili wake.
Unaweza kuwa mwili wa ujana, utu uzima au uzee.
Kama mtu alikufa akiwa bado kijana basi mzimu wake unaweza kuonekana akiwa katika hali hiyo ya ujana au akiwa mtoto mdogo.
Kama mtu alikufa akiwa mtu mzima, sio kijana tena, basi Mzimu wake unaweza kuonekana akiwa mtoto, kijana au hivyo hivyo alivyokuwa kabla hajafa.
Akifa akiwa mzee anaweza kuonekana katika umbo lake hilo la uzee au ujana au utoto kutegemeana na utashi wa alivyotaka kujifunua kwa watu wa jamii yake.
Mara zote huyu 'marehemu' hujitokeza au hujifununua na kujidhihirisha kwa 'watu wake' katika hali ya ndoto au maono.
Kama sio ndotoni au kwenye maono, basi anaweza kujitokeza mahali popote kwa 'watu wake' akiwa kwenye umbo la kiumbe kingine, kama vile mnyama fulani, mdudu au hata ndege fulani ambaye kwa jamii ya watu wake ni rahisi kumuelewa.
Mathalani, kuna mizimu isipojitokeza kwenye ndoto kama binadamu au mnyama wa kufugwa (hususani ng'ombe, mbuzi, mbwa, kuku nk), basi inaweza kujitokeza waziwazi katika umbo la Nyoka au mdudu fulani nk.
Mizimu mingi sana ya kiafrika hujitokeza mara nyingi kwa watu wake kama wanyama pori; Fisi, Chui, Simba, Ngedere nk. au kama wadudu mfano nyoka, konokono, siafu, mjusi nk.
Kwa hiyo, ni muhimu tuelewe kwamba pale mtu anapokufa na mwili wake kuzikwa, huwa haendi popote isipokuwa kwenye eneo la kaburi alikozikwa, ambapo kaburi lake hutumika kama nyumba yake, ingawa uwa ana uhuru wa kuzunguka zunguka kwenda mahali popote atakapo, sana sana kutembelea ndugu, jamaa na watu wake wa karibu; lakini makao yake makuu ni kwenye kaburi lake.
Ndio maana makaburini, ni mahali pa kiroho, ambapo roho za wafu huishi pale.
Watu wanaokwenda 'kuhiji' kwenye makaburi ya watakatifu wao (wazee wao), uwa wanaenda kuwasalimia na hata kujipatia baraka zao.
Wayahudi kutembelea makaburi ya wazee wao; makaburi ya kina Ibrahim, Isaka na Yakobo na wengineo; au Waislamu kutembelea kaburi la Mtume Muhamad (S.A.W) na 'maswahaba' wa mtume, au Wakristo kutembelea kaburi la Yesu, sio kwamba uwa wanaenda kucheza au kutalii tu, bali wanaenda kuzungumza na wazee wao ili kujipatia baraka; ingawa ukweli ni kwamba, roho za wafu hubaki makaburini, kati ya miaka 4 hadi 600 ambapo 'Spirit - Soul Consciusness' utengana katika kile kinachoitwa 'mind decomposition'.
Mind decomposition ni pale roho ya mtu inapotengana na nafsi yake milele, ili aweze kuendelea na safari kuelekea kwenye chanzo chake (asili yake) au kuzaliwa upya (reincarnation au rebirth)
Mtu aliyekuwa mwadilifu kwenye jamii, akitenda mema kwa watu wengine na kwa viumbe vingine, lakini akafa, katika mazingira tata au ya kuonewa, yaani kabla ya wakati wake, huzaliwa upya ili kulipwa mema na hiyo ndiyo huitwa 'rebirth'
Ndio maana kuna watu (sio wengi sana) huzaliwa katika mazingira mazuri, huishi hata kufa wakiwa kwenye maisha mazuri; wanakuwa hawana historia ya kupitia magumu. Ni kwa sababu wanalipwa malipo ya matendo yao mema waliyotenda walipokuwa katika mwili (before rebirth)
Mtu mwovu, mbaya, aliyekufa bila kulipwa mabaya kama alivyopaswa, huzaliwa tena ili kulipwa haki yake na hii ndiyo huitwa 'karmic reincarnation'
General reincarnation ni kule kuzaliwa tena ili ukamilishe kusudi ambalo ulikufa bila kukamilisha ulipokuwa duniani, yaani kuwa vile maumbile yalivyokutaka uwe.
Hii mada ya REINCARNATION & REBIRTH ni mada pana, tutajifunza kwa kirefu huko mbeleni.
Kwa hiyo unapotembelea makaburi ya watu wako, ujue unaenda kusalimia wazee, watakatifu wako, ili wakupe baraka zao.
Ndio maana yafaa huende na zawadi ambazo ni chakula ambacho wao walikipenda pale walipokuwa hai (walipokuwa kwenye mwili) sana sana ni vyakula vya mazingira waliyoishi, vingi vikiwa vyakula vya asili ya marehemu (mzimu)
Mfano, kama marehemu alikuwa Muhaya, basi atapelekewa vyakula kama ndizi, samaki, nyama, 'ntura', msusa, mnafu, maziwa, senene, kahawa, 'rubisi' na vyakula vingine vya jamii ya Wahaya, alivyopendelea yeye kula, wakati alipokuwa hai.
(Nimeshafundisha jinsi ya kutoa hivyo vyakula kama sadaka, kwenye masomo yaliyopita)
Hiki kitendo cha kutembelea makaburi ya watakatifu wako, ukaongea nao, ukawatolea sadaka na kuwaomba wakusaidie, pia huitwa tambiko.
Kwa hiyo kuna matambiko ya kufanyia madhabahuni kama nilivyokwisha eleza huko nyuma na matambiko ya kufanyia makaburini.
Somo litaendelea . . .
Dr. Magical power (PhD),
Mtafiti na Mkufunzi wa masuala ya kiroho.
NB: Mada hii ya MATAMBIKO inaendelea kwenye madarasa yetu maalum ya Utambuzi, inafundishwa huko 'Enlightenment Class 2' kwa malipo/ ada maalum.
Unaweza kujiunga kwa kuniandikia ujumbe DM