Mada: Kwanini tumefika hapa?

Mada: Kwanini tumefika hapa?

Utandawazi, + Unyumbulifu wa maadili +

Ndio mchawi mkuu, Utandawazi umekuja Africa wakati Ambao Jamii zetu zikiwa bado hazijajiandaa vyema kifikira dhidi ya mapokeo ya utawazi huo na kujua jinsi ya kuendana nao , Matokeo yake vijana wa sasa tumejikuta tuna fuata kila Aina ya mapokeo toka ktika Mataifa yenye nguvu ya ushawishi Basi kujali zuri ama baya , pasipo kutazama Nguvu zetu za kisaikojia Kama zinaweza kuhandle pressure ya Yale tunayo yaiga ,

Leo hii mahala tulipofika ktika vijana 10 ni vijana wawili tu ndio utakuta hawana picha za ngono za wapenzi wao ktika device zao ,

Dunia imefika pabaya Sana,
Sana Dunia imefika pabaya..kuna wakati ua nawaza dunia hii ya sasa na utandawazi huu, kizazi kijacho kitaikuta dunia katika hali gani?
Tutakua kweli mfano wa kuigwa kwa kizazi kijacho
 
Huko baadae ndio usiseme
 
Utandawazi, + Unyumbulifu wa maadili +

Ndio mchawi mkuu, Utandawazi umekuja Africa wakati Ambao Jamii zetu zikiwa bado hazijajiandaa vyema kifikira dhidi ya mapokeo ya utawazi huo na kujua jinsi ya kuendana nao , Matokeo yake vijana wa sasa tumejikuta tuna fuata kila Aina ya mapokeo toka ktika Mataifa yenye nguvu ya ushawishi Basi kujali zuri ama baya , pasipo kutazama Nguvu zetu za kisaikojia Kama zinaweza kuhandle pressure ya Yale tunayo yaiga ,

Leo hii mahala tulipofika ktika vijana 10 ni vijana wawili tu ndio utakuta hawana picha za ngono za wapenzi wao ktika device zao ,

Dunia imefika pabaya Sana,
Ni sahihi kabisa, lakini elimu ya msingi ya mahusiano na ndoa huwa inatolewa Kwa usahihi? Tukianza ngazi ya familia, na jamii na taifa kwa ujumla hali ikoje?
 
Inatolewa lakini imezidiwa nguvu na nguvu ya globalization, Yaani wakati elimu ya masuala ya ndoa inatolewa Basi ilipaswa na elimu ya namna ya kuhandle kasi ya globalization ingekuwa inatolewa vile vile ,, tena now days ndio kumekuwana balaaa ,, Kuna wanawake wengi Sana now days w
Katika wale unaowajua na usiowajua wana magroup ya WhatsApp huko Wana ongelea ngono tu kila kukicha miongoni mwao Kuna wake za watu na wasio wake za watu,

Yaani huko watu Wana danganyana ile mbaya , do you think mkeo akiwa ktik makundi Kama hayo aajifunza Nini !? Kama sio kuja kuleta mabalaa katika ndoa yenu
 
Na sijajua kwanini wanawake wakikaa peke yao wanaongeleaga zaidi wanaume na changamoto wanazopitia huko saluni, kwenye vijiwe vya ususi saizi Ndio imehamia kwenye makundi ya Whatsapp, elimu ilitakiwa itolewe zaidi kuwajenga hawa vijana hasa katika mahusiano kujua wajibu na haki zao katika mahusiano
 
Umofia kwenu!!!!!1

Kwanza kabisa niwatakie heri ya mwaka mpya 2022, ni muda mrefu kidogo nimekuwa ndugu mtazamaji lakini kwa leo naomba nilete hili kwenu.

Kwanza kabisa ijulikane taasisi ya mahusiano na ndoa ndio taasisi mama katika kuishape jamii, kumbuka taasisi hii ndiyo inayozalisha familia na familia ndio msingi wa maendeleo katika jamii yoyote, kupitia hii familia tunapata watu mashuhuri,viongozi wa dini,wanasiasa mashuhuri nk.

Lakini upepo unavyoenda hii taasisi imekubwa na dhoruba kuu, kutokana na changamoto zimewafanya vijana wengi wa kike na wa kiume kukata tamaa juu ya ndoa,ni kawaida tu kusikia "mimi nitafuta wa kuzaa naye tu basi, sitaki kuoa au kuoelewa kama mambo yenyewe ndio haya" Sasa kwanini tumefika hapa???....

1. Mahusiano yamegeuzwa ni sehemu ya ujasiliamali
Vijana wengi wa sasa wamegeuza mapenzi ni fursa ya kutoka, sio tena platform ya kuweza kutengeneza familia bora, vijana wakiume nao siku hizi wanatafuta mwanamke anayejiweza ukiwasikiliza wanasema maisha ni kusaidiana, hiyo kauli imewafanya wengi kupenda kitonga, mabinti nao ni hivyo hivyo unaweza kumpenda binti na kutimiza jukumu lako lakini ukaitwa danga na akawa na mahusiano na mtu mwingine kwa kigezo et huyu ndiye wa moyo, kama huyo ni wa moyo kwanini msiweke juhudi ya kutafuta vya mwili pamoja??

2. Mmong'onyoko wa maadili
Maadili yamepungua kabisa miaka ya nyuma mwanaume kutembea na mke wa mtu, suala lilikuwa halikubaliki yaani iweje utembee na mwanamke ambaye mwenzio amemgharamia na kujiwekea usingizi wake ndani wewe ukammendee ili hali wapo wanawake wengi wanahitaji kuhifadhiwa?? siku hizi imekuwa sifa na nyie ni mashahidi humu halafu inaanza kuonekana ni fahari kwa kijana kutembea na mke wa mtu, inaonekana ni ushujaa huku mwenye mke akionekana hajui mambo maarufu kama "kupeleka moto" Sasa kijana ambaye anatembea na mke wa mtu unafikiri ataoa?... hofu na mashaka ya kutafuniwa itamtafuna

3. Kuwa na Matarajio Makubwa
Vijana wengi wanapoingia kwenye mahusiano au ndoa huwa wanakuwa na matarajio makubwa kutoka kwa wenzi wao hii hutokana na ubinafsi, ule umimi, huyu hanifanyii hivi, mbona hafanyi hivi kama fulani, mwisho wa siku humpelekea mtu kutodumu katika mahusiano aliyoyaanzisha ama ndoa husika, inatakiwa ukumbuke wote ni binadamu na hakuna anayeweza kumtimizia mwenzake mahitaji yake kwa 100% hivyo tuwe wenye kutosheka na kuridhika.

4. Harakati za Haki sawa
Hiki ni kirusi kinachotafuna mahusiano na ndoa za wengine, dada yangu nikukumbushe tu kwenye suala la mahusiano hakuna kitu kinaitwa haki sawa, kwenye mahusiano mwanaume ni kiongozi na ili mahusiano yako yadumu lazima uzingatie hili "Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala" (mwanzo 3:15) . utii ndio kitu pekee na cha msingi sana wanawake wa kizazi hiki wamekosa, wanafikiri utii ni manyanyaso, ni ukatili na ndivyo linavyoweka kwa sura hiyo kitu ambacho si kweli.

5. Wanaume kutotaka kuwajibika katika mahusiano
Mahusiano ni zaidi ya tendo la ndoa ambalo wengi ndio hufikri ni mapenzi hayo, na ndio maana utaona wengi wakilalamika oooh mara ananinyima, oooh mara hafanyi sawa sawa, mahusiano ni zaidi ya hilo tendo hapa tukumbushane, baadhi ya wanaume wanasema kuoa mwanamke mwenye mtoto ni risk, ni kweli lakini huyo mtoto mwanamke anamtoa wapi?? usikute mwanaume umezalisha huko halafu unatembea kifua mbele kwamba sioi mwanamke mwenye mtoto, huyo uliyempa mtoto amuoe nani?? hao watoto/mtoto anatengenezewa sai8kolojia ya namna gani? muda mwingine akina dada mnasababisha hili mkihadaika kwamba pengine nikibeba mimba atanioaa, au anakuambia nizalie mtoto sitashindwa kumlea wakati unaona kabisa wewe mwenyewe mahitaji yako hupati sawa sawa, mwisho wa siku tunatengeneza watoto ambao hawana upendo wa kweli, watoto wanakuwa hawajali wala kuheshima

Tusipoliangalia hilop tukalichukulia kawaida basi tunatengeneza kizazi cha ajabu sana hapo baadaye, tutakao kuja kulaumiwa ni sisi, sasa hivi hali sio nzuri huwezi ukapita nyumba mbili tatu ukakosa binti aliyezalia nyumbani, itafika kipindi kumpata mwanamke ambaye hajazaa kabla ya ndoa itakuwa kama kusaka bikira, na litakuwa jambo la kufurahiwa sana kuliko kukutwa na bikra.

Samahani kwakuwachosha kwa thread ndefu najua mnapenda fupi fupi, mniwe radhi kwakweli, na hayo ni kulingana na mtazamo wangu na hali ya mazingira yaliyopo kwa sasa.
KARIBUNI KWA MJADALA​
safi sana kiongozi akili kubwa, busara na hekima, ukomavu na uongozi umesheheni, building a constructive society is our collective and mandatory responsibility. Sisi sote ni ndugu, umoja ni nguvu, pamoja tunaweza na shina lake ni taasisi iitwayo ndoa.

Mtarajiwa wa ndoa awaye yeyote zingatia ushauri huu wa mdau ipo neema ya kudumu ukizingatia.
 
Inatolewa lakini imezidiwa nguvu na nguvu ya globalization, Yaani wakati elimu ya masuala ya ndoa inatolewa Basi ilipaswa na elimu ya namna ya kuhandle kasi ya globalization ingekuwa inatolewa vile vile ,, tena now days ndio kumekuwana balaaa ,, Kuna wanawake wengi Sana now days w
Katika wale unaowajua na usiowajua wana magroup ya WhatsApp huko Wana ongelea ngono tu kila kukicha miongoni mwao Kuna wake za watu na wasio wake za watu,

Yaani huko watu Wana danganyana ile mbaya , do you think mkeo akiwa ktik makundi Kama hayo aajifunza Nini !? Kama sio kuja kuleta mabalaa katika ndoa yenu
Hii inapaswa kuwa mada za wanandoa kama life transition portfolio, do's and don't's kwenye maisha ya ndoa our brains organically knows all sorts of boundaries, dual education and sensitization among couples iwe endelevu plus religious platforms.
 
4. Harakati za Haki sawa
Hiki ni kirusi kinachotafuna mahusiano na ndoa za wengine, dada yangu nikukumbushe tu kwenye suala la mahusiano hakuna kitu kinaitwa haki sawa, kwenye mahusiano mwanaume ni kiongozi na ili mahusiano yako yadumu lazima uzingatie hili "Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala" (mwanzo 3:15) . utii ndio kitu pekee na cha msingi sana wanawake wa kizazi hiki wamekosa, wanafikiri utii ni manyanyaso, ni ukatili na ndivyo linavyoweka kwa sura hiyo kitu ambacho si kweli.
Jambo la msingi sana hili
 
safi sana kiongozi akili kubwa, busara na hekima, ukomavu na uongozi umesheheni, building a constructive society is our collective and mandatory responsibility. Sisi sote ni ndugu, umoja ni nguvu, pamoja tunaweza na shina lake ni taasisi iitwayo ndoa.

Mtarajiwa wa ndoa awaye yeyote zingatia ushauri huu wa mdau ipo neema ya kudumu ukizingatia.
Ubarikiwe
 
Jambo la msingi sana hili
Mahusiano mengi yanavunjika ukiangalia Kwa umakini kuna movement ya haki sawa yaani mwanamke anataka mwanaume akitoka na yeye atoke bila kuulizwa halafu hapo hapo anataka apendwe, athaminiwe na kuheshimiwa kitu ambacho hata ukienda Kwa mganga Kwa mwanaume Hilo haliwezekani mwanamke anatakiwa amtreat kama mfalme hapo atakuwa malkia bila shuruti
 
Na sijajua kwanini wanawake wakikaa peke yao wanaongeleaga zaidi wanaume na changamoto wanazopitia huko saluni, kwenye vijiwe vya ususi saizi Ndio imehamia kwenye makundi ya Whatsapp, elimu ilitakiwa itolewe zaidi kuwajenga hawa vijana hasa katika mahusiano kujua wajibu na haki zao katika mahusiano
Kwa kweli hata Mimi sijui
 
Hakika, umenena vyema...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Mada mzuri sana mkuu
Wewe unafikir tufanye Nini? Wimbi la vijana kujisifia juu ya kula wake za watu linaongezeka na imekuwa kafasheni wanajisifia kula wake za wenzao wakat huo Kuna mabint wamewazalisha hawaijui hata sabuni
 
Hakika, umenena vyema...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
Nimeangalia clip moja nimejikuta naumia sana vijana wakiume(mashoga) wanahojiwa vijana ambao ulitegemea watengeneze familia dah!! Inasikitisha angalia sababu yao et ni homoni zimezidi kwenye miili Yao ndio maana wamejikuta mashoga kizazi kitakachofuata sijui kutakuwa kizaz cha namna gani?
 
Inasikitisha sana, wengine wanasema wamejikuta tu wapo hivyo...

Huwezi kujikuta tu upo hivyo mazingira yanachangia sana kutengeneza tabia ya mtu...
 
Huwezi jikuta tuuu, eti nimeumbwa hivyo na Mungu, Mungu gani huyo angeumba angekataza? yaani eti na wao wanachama cha kusaidiana na walikuwa kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa mwenzao
 
Back
Top Bottom