Mada Maalum kwa wale tuliokutana na Watu wanaoongea sana

Mada Maalum kwa wale tuliokutana na Watu wanaoongea sana

kisokolokwinyo20

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2019
Posts
472
Reaction score
423
Kuna watu wamejaliiwa kuzungumza, yani mnaweza kukaa mahala akawa anaongea yeye tuu muda wote.

Kiukweli hawa watu wanaboa hasa ukutane na yule mjuaji na mbishi yani ukitaka kumuongelesha tuu utasiki 'sikiliza wewe mimi najua' ni hivi na hivi na vile.

Nyie waongeaji embu punguzeni kidogo na muwe na akiba ya maneno!
 
Kuna kamama jirani yangu huwa kaongeaji balaa. Nahisi hadi muda wa kupumua huwa kanakosa.

Mtu anaongea mada ya kwanza kabla hujapanua mdomo kuchangia kashamaliza mada ya pili yupo ya tatu. Basi unabaki kukubali kwa kichwa tu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]asee huyo ni noma

Anakosa muda wa kupumua yani anakufwa na kuamka tena anaongea tuu
 
Back
Top Bottom