Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Ni siku nyingine tena imepita, tumerudi salama majumbani mwetu, kuungana tena na wapendwa wetu, familia na watoto pia. Baadhi yetu hatujarejea, tuko mishe na viti virefu, baadhi tuna sababu za msingi na nyumbani wanafahamu na tumewapa taarifa, wanatusubiri watupokee kwa upendo, kwa furaha kwa bashasha kuu.
Baadhi hali ni tofauti, hatungependa kuchelewa nyumbani, tungependa tuwahi, tuungane na familia, tuimalize jioni kwa furaha kuu kabla hatujaungana kwa dinner na maombi ya usiku, lakini hali ni tofauti. Tunapoteza muda nje saa zisogee ili tukifika tu ni chakula kuoga na kulala, tunakimbia kero na malumbano yasiyoisha.
Ndoa haina furaha, ndoa haina amani, majuto ni mengi mno moyoni. Kila mmoja anajutia kivyake, hakuna upendo tena, hakuna kuaminiana tena, ni mwendo wa kutuhumiana na kuviziana. [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]Baba ana chumba chake, mama naye ana chake, ama la chumba ni kimoja lakini kila mmoja ana kitanda chake.
Hakuna upendo, hakuna sharing, hakuna majadiliano ya changamoto, ya maumivu ya kushinda na kushindwa, ya kutiana moyo na kufarijiana, kila mtu kivyake, kila mtu na lwake. [emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji24][emoji17][emoji17][emoji17]
Karibuni wanandoa wote, ni mada ya kupeana faraja na kushare maumivu. Itambueni nguvu ya kuongea, kuongea hupunguza maumivu mengi, kupitia mada hii utajiona hauko pekeyako na pengine utaona kuwa kumbe wewe una nafuu kubwa ukisikia ya mwenzako. Jisikie huru ufunguke.
Funguka kwenye ndoa yako iliyoumizwa na kujeruhiwa sana, iliyotiwa vidonda na makovu ya kila aina;
~ Ya usaliti,
~ Ya kuchapiwa,
~ Ya kusingiziwa,
~ Ya kunenewa mabaya,
~ Ya kudharauliwa kutukanwa na kudhalilishwa.
~ Funguka upate nafuu,
~ Funguka upate faraja,
~ Funguka upunguze sumu mwilini,
~ Funguka upate kupona sasa.
Karibuni wanandoa wote.
Jr[emoji769]