Mada maalum kwa wanandoa

Mada maalum kwa wanandoa

Unataka kuniambia kuwa hajioni kama anajiharibu mpaka mimi nimwambie? Ndani kuna vioo kila sehemu, chumbani, vyooni, bado tu mpaka mimi nimwelekeze what to do? Wanawake walivyo wa hajabu, mimi kama mumewe ninaweza kumuambia what to do ili asijiharibu shepu, yeye ataanza kufikiri labda nina nyumba ndogo au kuna mwanamke mtaani namtamani alingane naye, ndiyo maana unakuta sie wanaume hatuwaambii chochote wake zetu kuepuka malumbano ya kijinga. Unamwacha ajiharibu zaidi ili upate kisingizio ama kigezo cha kutafuta nyumba ndogo. Endeleeni kujiharibu tu na kutukata stimu ya kutowapenda.
[emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji851][emoji851][emoji851]wee jamaa mke wako anapata shida daaaah!

Yaan ni unamtaftia kila aina ya sababu haahaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika vitu ambavyo siwezi kuishi kwa kukosa Amani nmekubari matokeo siku nyingi ndoa imenishinda nmemuachia nyumba na mtt moja mwingine naishi nae mwenyewe bahati yngu nafanya kazi njee ya nchi nikija likizo kwa miaka 2 mara moja nafikia hotel mwenzi wngu moja nasepa kosea vyote ila ukikosea kuoa au kuolewa ni balaa kuliko kitu chchote duniani usije kbs kutoa lawama ukisikia mtu amejitoa Uhai ndoa zina mengi jamani...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmmh yako Kali asee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi suala la ruhusa ya kutoka hilo halipo na halitakuwepo...sijakuoa uje kuwa mlinzi wangu na kunipangia vitu vya kufanya na kutokufanya ati nirudi home saa 1
Ukienda hivyo hamtafika, ndoa ni maelewano na kuishi kwa amani na upendo. Pia kumbuka mumeoana. Lazima kila kitu kuwe na kiasi sio kufanya ili kumkomoa mwenzako. Ana haki ya kukuuliza ulikuwa wapi na pale unapochelewa kurudi nyumbani maana ni mkeo, nyie ni mwili mmoja mumekubali kuishi kama mke na mume hivyo kuna vitu lazima mukubaliane maana kila mtu ana mapungufu yake. Pia hamna sehemu niliyosema mume arudi saa 1 ila nimejitolea mfano mimi na mume wangu huwa tumepangiana kwamba awe anarudi saa 4.
 
Aisee...! Mi nna miezi miwili tu ya ndoa nafikiria kutoa Talaka nibaki maisha yangu ya usela maana kabla sijaoa nilikua na furaha lakini sa hv furaha ni asilimia tano tu
Pole mkuu, hizi ndoa sijui zina nin siku hizi, hapa Nina mwaka mmoja ndoani , lakini I wish nisingeoa, naona kama niliwahi sana kuoa, yaani I am cornerd, napenda kuwa ndoani, lakini sio na mwanamke huyo!
 
Pole mkuu, hizi ndoa sijui zina nin siku hizi, hapa Nina mwaka mmoja ndoani , lakini I wish nisingeoa, naona kama niliwahi sana kuoa, yaani I am cornerd, napenda kuwa ndoani, lakini sio na mwanamke huyo!
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji144][emoji144][emoji144][emoji87][emoji87][emoji87]

Jr[emoji769]
 
Jaman nimetengana na mume wangu baada ya kuona vipigo vimezidi ikabidi niondoke niende kwa kaka angu ambaye naye anafamilia yake,nilikuwa nafanya nya kazi katika kampuni Fulani lakini mume aliniachisha kutokana kazi iyo kuwa na shift za usiku na nilikuwa na mtoto mdogo,kwa sasa nilikuwa najishughulisha na biashara ndogondogo apo nyumbani ,ila tangu nimeondoka nipo mkoa mwingine kwa sasa sijasimama vizur kibiashara mana niliondoka pale bila chochote,uyu mwanaume anakomaa yeye atatuma laki 2 tu kwa ajili ya kumtunza mtoto kwa mwezi wakati yye kipato chake kwa mwezi haipungui 1.4milion je nisahihi iyo pesa kwa kipato chake

Jr[emoji769]
Copy n paste from JF post
 
Hahahahaaaa! Kuoa bila mipango au kulenga ishu moja tuu matokeo yake ndiyo hayo!!

Kabla ya kuoa ulipaswa kujua au kujifunza utaishi vipi na mkeo na hata baadae wanao! Yanayobaki muachie Mungu

Mie nina zaidi ya miaka 10 kwenye ndoa, mwanzoni nilipata ugumu flani coz kuna mmoja wetu kabadili dini so kufundishana na kuwekana sawa ilikuwa shida kidogo! Pia nilikiwa mnywaji, kurudi usiku hakuna muda na familia napo vilichangia kuweka gap kwenye ndoa yangu na wakati huo kipato kilikuwa chini, so tukawa na matamanio yasiyotimia matokeo yake ni stress na kugombana!

Kabla ya kuoa nilipanga kuwa na familia yenye furaha, outings na vacations na safari ni vitu napenda sana kiukweli!! Nilihitaji mtu wa kufanana nae!

Nilipoanza kazi na NGO moja hivii inadeal na maswala ya ndoa! Nilikuja kugundua visababishi vya vikubwa vya migogoro ya ndoa ni nini! Kimoja wapo ni kitendo cha kila siku kurudi nyumbani usiku wa manane, umelewa wanawake wanaumia sana ila basi tu! Yakimzidi ndipo nae hutafuta faraja kwa namna ingine au hubadilika tabia na ndipo hapo, migogoro inaanzia!

Niliamua kubadilika, pombe nikaacha na familia yangu ikawa ndiye rafiki zangu wakubwa!!

Naishi kwa amani na nafurahia maisha ya ndoa to maximum!! Sijutii kwa hakika na naamini hata mke wangu vile vile!!

Tunatoka outing wote, tunasafiri tunavyopenda tunafanya yanayotupasa yaan ni full furaha! Namshukuru Mungu kwa kweli.

Ndoa ya furaha inawezekana ila kwa jitihada za pande zote mbili!! Ukiona unaleta furaha ila upende mwingine hauhitaji uwe hivyo hilo ni tatizo na hapo inabidi kuchukia hatua!

Kikubwa tumia muda mwingi kuchunguza utayetaka kuoa au kuolewa nae. Kama ana tabia usiyoipenda jikatae mapemaaaa! Usitarajie atabadilika akishaingia kwenye ndoa, na hili ndiyo kosa la wengi!!
Hongera sana
 
Hatimaye nimesoma posts zote...wtf??

Ukisoma hivi kila siku lazima nyongo ijae mwilini, sitaki kusoma vitu hasi namna hii, havijengi ni kubomoa tu mwanzo mwisho, japo kuna funzo pia tunapata.

Tufanyie kazi mahusiano yetu, huwa naamini hakuna maisha marahisi, uwe single, umeoa/kuolewa, uwe mtawa, divorcee, ishi na dada/kaka zako. Maisha ni fumbo, haturidhiki sisi wanadamu.

Naishi jinsi nilivyochagua, najaribu kufanya compromise ili hata nisiyopenda niendane na mwenzangu. Life's too short to yell all the time!!
Thanx Mshana Jr, bango zuri...
Eliii
 
Back
Top Bottom