Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Katika barabara inahitaji umakini basi ni Dar hadi Morogoro, na kama hauna uzoefu ni bora ukatoka Dar saa nane usiku ili ufike Morogoro mapema kabla barabara haijawa busy sana.
2014 nilifanya kazi kati ya Kibaha na Chalinze yani hiyo barabara niliipita mara mbili kwa siku.. Kwa miezi 12 kama hakuna siku nilikutana na ajali basi hazizidi wiki mbili
 
Mitaa ya Mwanga kuelekea Same usiku wa saa saba au nane lazima ukutane na mbuzi au punda wanajichunga peke yao,

Ni mimi tu hukutana nao au ipo namna!!!
 
Ndo maana Matajiri wengi Wa magari ni makatili, Mjinga akiingiza Gari yangu mazingira kama haya lazima nimlambe makofi tu. Afu litalalamika limeonewa
Wewe ulipokuwa unapokea hela bila kudadisi hali ya njia, ulitegemea gari ikifika hapo ivukeje?

Tajiri anayethamini mali yake hawezi ruhusu gari iende popote tu bila kujua hali ya njia ikoje!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…