Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

TANGAZO TANGAZO MUHIMU.
Katika ajali Lori iliyotokea jumatatu Maeneo ya Soni Halmashauri ya Bumbuli Kuna mwili mmoja bado haujatambuliwa.
NI kijana mwenye katiba umri wa miaka 26 hivi na inasemekana alipandia hambalawei Kata ya shume wilayani Lushoto
Hivyo kwa yeyote mwenye kumtambua au kupotelewa na ndugu yake wa kiume afike ofisi ya Mganga mkuu Lushoto.
Simu 0626790182/0626757209/0789649777
Sambaza ujue huu.
 
Falcon ya Dar _ Tarime imeingia nyuma ya roli bovu usiku huu ambalo halikua na ishara yoyote ya kuashiria ubovu wake.
Nawasihi madereva kuendelea kuwa makini sana mtumiapo vyombo hvi vya moto barabaran, mnagharimu maisha ya ndugu, wapendwa, marafiki na wengineo waliowaamini na kuwapa dhamana ya nyie kuwa beba na kuwapeleka makwao salama
.
NB:ONGEZEN UMAKIN
 
Haka kamwez kamechangamka kwa ajari
 
Habari za muda huu kuna ajali ya gari imetokea hapa kwa Kipara Tuangoma karibu na Stainley Toyota R4 T332DFG nyeusi imegonga mnazi imekatika vipande viwili chanzo speed kubwa akitokea Kongowe kwenda Kigamboni wamefanikiwa kumtoa dereva alikua peke yake yupo hoi muda huu miguu yote imekatika.
 
Taarifa kama tulivyoipokea:

"Imetokea ajali mbaya sana eneo la Mwitikio kata ya Kiloli Sikonge iliyohusisha basi la Mkombozi na Sase Bosa zikifukuzana zikielekea Mbeya muda mfupi uliopita na watu kadhaa wamefariki dunia

Tunafatailia taarifa kamili

 
Hii taarifa siyo ya kweli mkuu!
 
AJALI YAUA POLISI NA MAHABUSU MWANZA

Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili - waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya kigaidi pamoja na mauaji, wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 katika Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Sengerema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la polisi aina ya Toyota Landcruise yenye namba za usajili PT 3798 lililokuwa likitokea mkoani Mwanza, kukata ‘sterling rod’ na kuhama kutoka upande wake na kwenda upande mwingine na kugongana na Lori aina ya Scania likiwa na tela namba. T.865 mali ya kampuni ya Nyanza Botling.

Ajali hiyo pia imejeruhi watu wanne na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita huku miili ya askari hao wawili ikihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

#AJaliYaGariGeita #PolisiWapataAjali #Ajali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…