Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

Mada Maalum ya Madereva: Changamoto, Uzoefu, Vituko na Connections

IMG-20220901-WA0012.jpg
 
VETA ina uwanja mpana zaidi wa kujifunza vingi zaidi nadhani hata gharama ziko chini kulingana na private sector
ila kwabushauri mtu asije somea veta ya dar es salaam utajuta bora ukapige mkoani kwanza kuna utulivu wake
 
Kuna yoyote anae weza kuwa na connection ya udereva it, kuna kijana anaulizia mishe hizo
 
TAHADHARI KWA ABIRIA WAISHIO DAR ES SALAAM
Ikifika jioni maeneo ya Mnazi Mmoja kwa sababu ya shida ya usafiri wa kutoka katikati ya jiji kwenda maeneo mbalimbali pembezoni mwa mji, kuna wapiga debe hutangaza usafiri kwa nauli ya shs Elfu Mbili, kwenye moja ya Magari Madogo na Noah. Hususani maeneo ya karibu na Benki ya CRDB Tawi la Lumumba.
Majuzi jamaa Mmoja alipanda hizo gari akiwa na wenzake ikidaiwa inaelekea Gongo la Mboto. Matokeo yake walitekwa na watu wenye silaha ambao awali walijifanya nao ni wasafiri na kuporwa kila kitu baada ya kupelekwa Pugu Mnadani Wakasachiwa huku wakitishiwa kupigwa risasi na kuchinjwa kwa visu walivyokuwa wamebeba.
"Ukiweza wajulishe wengine ili wapande usafiri huo kwa tahadhari au wakiweza waachane nao"
 
Back
Top Bottom