Machache ya kujifunza:
1. Uchaguzi huu umefuatiliwa kwa miezi miwili mfululizo. Hata CCM walipokua kwenye kitchen party yao Dom walikua wanachungulia simu kujua kinachoendela Chadema. Tuilinde imani kubwa Watanzania waliyoonesha kwetu.
2. Mchuano wa Freeman na Lissu umeifanya Chadema kupata promo kubwa na kujibrand bila wasanii wala celebrities.
3. Chadema imefundisha demokrasia kwa vitendo. Fomu ya Mwenyekiti haikutolewa moja kama hati ya kifo. Yeyote aliyejipima na kuona anaweza kuongoza, alipewa fomu, akiwemo rafiki yangu Odero aliyeambulia kura moja.
4. Uchaguzi umeendeshwa kwa uwazi na kura kuhesabiwa hadharani. Freeman amefundisha somo la demokrasia kwa vitendo. Kule Chama chakavu wasingekubali Mwenyekiti wao aondoke kwa kura 31 tu, wangepindua meza. Lakini Freeman ni muumini wa haki na ameheshimu demokrasia. Respect to him 🙏🏽.
5. Chadema tumeset golden standards kwenye viwango vya Free, Fair, Credible and Transparent election. Hakuna Chama chochote kimewahi kufikia kiwango hiki cha uwazi. Kwa sasa vyama vingine vikifanya chaguzi vitapimwa kwa viwango vyetu. Sisi ndio SI unit.
6. Mbunge mmoja amedai eti wajomba zake Wachagga wamepigwa kwenye huu uchaguzi. Hivi tunataja makabila kwani tunatambika? Acheni ufala. Kwenye uchaguzi wa kisiasa mtu apimwe kwa hoja zake sio kabila lake. Kama wachagga wamepigwa, je "Strategist" wa Lissu, Godbless Lema ni Mkikuyu? We "Mpwa" tunakuonya acha ushamba kutaja makabila kwenye mambo serious. Tulikua hatufanyi tambiko, bali uchaguzi. Au tukupe laana ya ujombani ukose jimbo?
7. Kwenye press yangu ya tar.12 nilisema watu waweke akiba ya maneno. Usinene ukamala. Nilisema baada ya uchaguzi kuna watu watatamani kuyameza maneno yao lakini haitawezekana.
8. Ni bahati mbaya wapambe waliongea mengi kipindi cha kampeni na kuifanya CCM ichukue notes ambazo wanaweza kuzitumia baadae dhidi yetu.
9. Kwenye press yangu nilishauri Mwenyekiti atakayechaguliwa aunde Post Election Mediation committee itakayotibu majeraha yaliyojitokeza wakati wa kampeni.
10. Watanzania wanatupenda, wanatuamini. Tukilinde chama chetu kwa wivu mkubwa. Kikifa itachukua miaka mingi kupata chama kingine kitakachoaminika kama hiki. #StrongerTogether 💪🏽