Hivi kwann malor huwa yanainua yale matair ya nyuma? Na huinuliwa kwa mfumo gani?
Idea nzima ya kunyanyua matairi ni kupunguza matumizi ya matairi hayo kipindi ambacho gari halijabeba mzigo, kumbuka malori yana matairi Mengi si kwa ajili ya urembo ,ni kutokana na mizigo mizito yanayobeba. ,ilikiwa tupu kunakuwa hakuna umuhimu wa kuyatembeza yote,
Mifumo ya kunyanyua matairi iko miwili , kutegemeana na aina ya suspension zilizotumika , kwa steel suspension mfumo unaotumika ni hydraulic , kwa air suspension mfumo unaotumika huwa ni wa electronic solenoid ambayo kimsingi huwa ni hewa . kwa bahati mbaya sina uwezo wa kuielezea humu jamvini, ila ni mifumo rahisi Sana Kama unaielezea kwa vitendo .
Kwa kuongezea tu , kuna aina mbili za kunyanyua matairi,mid lift na tag axle
mid lift , hii hunyangua tairi za mbele ya diff,
Tag axle ,hunyanyua tairi za nyuma ya diff,
Mid lift huwa inanyanyua tairi ikiwa empty tu, Tag axle huwa inanyanyua hata Kama Ina mzigo , idea ni kuongeza mkandamizo kwenye diff, Kama itatokea kuteleza .nk, na ndio sababu tag axle huwa zinatumika Sana kwenye rough roads.