Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

mkuu mshana naomba unijuze kuhusu ulaji wa mafuta kwa gari spacio old model maana gari yangu inatumia mafuta lita kumi kwa km 56,nimejaribu kubadilisha plug na kufanta service nyingine km kuchange oil filter na vingine ila bado inanichangana kwenye ulaji wa mafuta, ushauri wako mkuu, maana digital gauge inashuka jwenye red taa mpk inaniboa
 
Wakuu, Nina Toyota Premio ambayo ina miezi miwili tu tangu nimeichukua. Nimegundua muungurumo wake umekuwa mkubwa sana tofauti na ilivyokuwa awali, naomba kujua je kutakuwa na tatizo?
 
Wataalamu naombeni kujua aina ya injini na ulaji wa mafuta wa hz RAV 4 ambazo mbele ubavuni baada ya mlango zina nembo ya gx. Nawasilisha
 
Wakuu, Nina Toyota Premio ambayo ina miezi miwili tu tangu nimeichukua. Nimegundua muungurumo wake umekuwa mkubwa sana tofauti na ilivyokuwa awali, naomba kujua je kutakuwa na tatizo?

Mkuu pole sana, moja ya sababu us gari kubadili muungurumo yaweza kua wheel bearing kuharibika. Hizi zikiharibika gari hutoa muungurumo usio wa kawaida (wengi husema, Gari INAVUMA). Check na fundi, mimi si mtaalam sana. Lakini kama shida ni bearing ni ishu ndogo sana kwani ubadilishaji wake si gharama na zoezi la dakika chache tu
 
Habari wadau! Gari yangu inasumbua AC, ukiwasha inatoa baridi kwa muda kidogo then inatoa joto tena Kali tu. kwa wataalamu naomba ushauri Kama hii ni kitu naweza rekebisha mwenyewe Au Kama ni kitu serious basi naomba kuelekezwa wapi naweza pata fundi mzuri wa AC za magari. Mimi nipo Dar. Wasalaaaam!
 
Heshima kwenu wakuu
nilikuwa nauliza vipi kuhusu uimara na matumizi ya mafuta
fuel consumption kwa Suzuki grand vitara 2015 model? 2.4cc (2400cc)
4cylinder

Natanguliza shukrani.

Mkuu hizo gari ni nzuri sana, mm ninatumia Escudo ya 2006 V6 inatumia lita moja km7-8 ikiwa na ac! ya cc2400 huwenda inakula vzr zaid
 
Vipi kuhusu Audi a3, Nataka kuagiza, Msaada kwa anayezifahamu Please
 
mshana ujanijibu kuhusu spacio yangu kwa uzoefu lita moja kwa km ngapi please
 
Nijuzeni juu ya gari aina ya audi A4 ALT engine ya mwaka 2005 kama zina tatizo au uzuri wowote
 
Nashukuru mkuu Nguso,itabidi nifanye mpango nimchek fundi ili atizame tatizo nn kwa sababu kuna jamaa ameniambia leo kuwa huenda eksozi imetoboka ndo maana inatoa muungurumo mkubwa
 
Hongera Sana mleta mada. Ni Shule tosha na ninefahamu mambo mengi, zaidi nijuavyo kama wengine. ILA ombi langu kwa Invisible kuwa jukwa rasmi. Kwani itawapa wengi shida kurudi nyuma kufuatilia Uzi, pindi watakapo wasilisha maombi ya ushauri na Ku shauriwa kufanya hivyo. Na pia kwa wataalamu wetu kutorudia ten times kitu kile kile kama ilivyo sasa.
CC mshana j Invisible
 
Last edited by a moderator:
Thanks mkuu, naomba njia rahisi ya kujua gari inatumia lita 1 kwa km ngapi.

Njia ya kwanza ni kwa kuangalia manual book sehemu ya çc lakini bahati mbaya sana nyingi zimeandikwa kijapani

Njia ya pili ya kienyeji sana ni kureset km kwenye 0 kisha weka mafuta hata lita mbili tu endesha mpaka yaishe kisha angalia umbali wa km
Nb: zoezi hili inabidi mshale uwe chini kabisa
 

Mmh hii ni beyond abdormal kama tank halina leakage onana na fundi mahiri afanye computerized diagnosis
 

Inawezekana kabisa kuna leakage hivyo msukumo unapokuwa mkubwa gas huvuja lakini pia angalia knob ya kuadjust joto na baridi
 

Inawezekana kabisa kuna leakage hivyo msukumo unapokuwa mkubwa gas huvuja lakini pia angalia knob ya kuadjust joto na baridi
Lakini pia compressor yaweza kuwa na shida
 

Yaweza pia kuwa exhaust pipe imeachia kwenye joint ya muffler inategemea ni mlio wa aina gani kwakuwa hata engine oil ikipungua sana yaweza leta hilo tatizo
 

Thanks mkuu, ngoja nijaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…