Ansah Miles
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 392
- 175
jamani napenda kujua kuhusu suzuki jimmy wide juu ya upatikanaji wa spare, utumiaji wa mafuta pamoja na durability yake.
Mtoto ni kiumbe hai, zaidi ya hatari zinazoweza kumpata yeye binafsi hana madhara na anaelezeka kama ni keshapata akili, gari ni mashine haijitambui, utakachofanya ndio kitakachotokea
Yes, na mimi nimejadili issue, tena muhimu kuliko magari ya Gluga na Haria or what have you.
Nimeongelea tatizo sugu nchini, ukiona mtu anasema Toyota Gluga na Toyota Haria na jamii inaona ni sawa ujue kuna tatizo la msingi la kitaifa la semi literacy.
Kuna vizazi vizima, a whole litany of generations, ambavyo vilikwamishwa na kiunzi cha mtihani wa darasa la saba, na kwa walio wengi haukuwepo uwezo wa kujiendeleza kwenye shule binafsi. Ndio unapata kizazo cha Toyota Gluga.
Ukienda Ilala Shauri Moyo watu wanauza maduka ya spea za "Prado Mayai" "Rava fo new modeli" Ukiwatajia make and model hamuelewani. Wanakuuliza "Mayai sio Mayai"? Sijui kama ni mayai, haijaandikwa mayai kwenye tail end... please!
Kama taifa, tunatakiwa kushughulikia hili tatizo la watu wetu, semi-literacy, kwa vizazi vijavyo.
Unazo zote mbili Toyota Kluger na Toyota Gluga?
Yes, ulivyoandika ndivyo ulivyo! Utajitengaje na kituko kilichotoka kichwani mwako? Na hili sio suala la "ngeli," hili ni jina la kitu, Toyota Kluger, hakuna GLUGA!
Mnajadili magari gani, Toyota Gluga? Mtu hujui kuandika na kusoma utajadi magari utawezaje wakati hata user manual ya gari itakushinda? Eti unajadili issue nyeti, issue nyeti kwako ni elimu ya msingi huna, hakuna Toyota Gluga!Tunajadili magari sio lugha, we mpuuzi
Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.
Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.
Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake
Karibuni sana
Ushauri: Jinsi ya kununua gari iliotumika ndani ya Tanzania
View attachment 225786
Mshana Jr, Naomba ushauri wako nina gari aina ya Nissan primera ya UK hii gari hili gari linatoa alama ya chk engine kwenye dashboard hali ukiliwasha injini inakuwa haina nguvu halafu linapiga brake fire na miss nyingiii, nimewatafuta mafundi wa umeme lakini wengi wameshindwa, unaweza kunijulisha ni mtaalamu gani anaweza kuja kufanya diagnosis ili niweze kupata uvumbuzi ?
Nashukuru ila ungenipa details zaidi ninawapataje wataalamu wa computer diagnostics
Mmh hii ni beyond abdormal kama tank halina leakage onana na fundi mahiri afanye computerized diagnosis
Mkuu nina gari aina ya Toyota RAV4 nikiendesha mwendo mrefu gari ikachemka halafu nipaki, nikija kuweka D au R gari inashtuka ikiambatana na mlio "kuu"
Hapa tatizo laweza kuwa nini?