Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

nabjtaji kununua mimi kitambo laki i huwa naziogopa sana bei zake i think huu mwaka kabla haujaisha nitanunua nalenda zile ambazk sio kipanya kwa matumizi ya biashara napenda zile kama caravaan na muundo ule ila bei sasa
 
Habari wanaJF'
Naomba ushauri wenu kuhusu aina ya tairi gani nzuri na imara, na ufafanuzi zaidi kuhusu namba zinazokuwa pembezoni mwa matairi: mfano Saizi: 175 / 80 R16 91S, mbadala wake ni saizi ipi?
 
Za mda huu wadau nimeuliza zaidi ya mara 3 naomba kujua kuhusu pajero mini
Nina vitz nataka kushift kweny hyo gari
Ningependa mnisaidie kuhusu unywaj wa mafuta upatikanaji wa spea na pia mafundi wake wapo
Asanten sana
 
Jamani mbona mnalipotezea hilo tatizo langu. Au mpaka niwaite wakongwe wa uzi huu. Haya njooni hapa akina mshana jr Kaizer N'yadikwa Preta PRONDO lusungo OLESAIDIM Profesa na wengineo wote.
 
Last edited by a moderator:
Wadau, naomba uzoefu kwa alowahi kununua gari toka japan na kampuni ya autocom japan. Nataka kupata ufaham kama hawana longolongo na utapeli na ucheleweshaji wa mzigo. Nawasilisha
 
Za mda huu wadau nimeuliza zaidi ya mara 3 naomba kujua kuhusu pajero mini
Nina vitz nataka kushift kweny hyo gari
Ningependa mnisaidie kuhusu unywaj wa mafuta upatikanaji wa spea na pia mafundi wake wapo
Asanten sana

Mkuu........sijatumia Mitsubishi lakini......mmmmh.........kama pesa yako sio ya mawazo........ichukue........spea zake zipo juu kidogo na kama upo makini.......hizi gari zimeanza kutoweka mjini.........watu wengi wamezikimbia..........baki na vitz yako au ilishe vizuri ishibe ikuwe iwe IST.........
 
Habari wanaJF'
Naomba ushauri wenu kuhusu aina ya tairi gani nzuri na imara, na ufafanuzi zaidi kuhusu namba zinazokuwa pembezoni mwa matairi: mfano Saizi: 175 / 80 R16 91S, madala wake ni saizi ipi?
Mdau kwa hilo la namba ninekuwekea image ina maelezo kwa picha hope utaelewa.
 

Attachments

  • 1437150748172.jpg
    43.1 KB · Views: 265
Wazee poleni na majukumu, nimenunua gari toyota allion cc 1490, milleage 57000km, ya mwaka 2002, engine VVTI.gari imefika mwezi wa 6 mwaka huu..tatzo la gari hii ni kutumia mafuta mengi, yaani inakwenda wastani wa 1lita per less than 7km, nilienda kwa fundi mmoja wa mtaani akaniambia nibadilishe plug. Nimebadilisha plug tena pale kariakoo lile duka la kisangani nimeweka plug original lakini bado gari linakunywa sana mafuta tofauti na.cc zake na situmii hata AC. tatizo jingne ni.gari kutokuwa na.nguvu wakati wa kupanda mwinuko mdogo tu.
Najua jamii forum naweza pata ushauri wa nini kufanya hapa. Asanteni sana ndugu
 

Vipi engine oil inapungua mara kwa mara? yawezekana kabisa block ya engine ikawa imetanuka au piston rings zimekwisha na nadhani ndiyo maana mafuta yanatumika mengi kwa kuwa unaiendesha kwa kuilazimisha ikimbie kama awali kwahiyo mafuta yanakwenda mengi zaidi
 

Hahahahahahaha
Nahisi nimekuelewa vizuri sana mzazi
 
Aisee Geem nieleweshe vizuri hapa, oil nimemwaga mara moja, na hizi poston rings ndo enjector mozle au..nieleweahe vizuri hapa.maana mafundi wa.mtaa.kila.mtu anajibu lake
 
Mdau kwa hilo la namba ninekuwekea image ina maelezo kwa picha hope utaelewa.

...Asante sana mkuu kwa image! Sasa Nimeelewa maana ya hizo namba za pembezoni.

NB: Naomba ushauri: "gari ninayotumia ilikuja (imported from JP) na matairi yenye namba / saizi 175 / 80 / R16. Nimeenda Dukani kuulizia mpya wakaniambia kuwa hiyo saizi hawana, wakashauri kuwa ninaweza kuweka tairi yenye namba hizi: 215 / 70 / R16, Je hiyo saizi inakubalika kwenye RIM AMBAYO IMEKUJA NA TAIRI YENYE NAMBA 175/80/R16 ?"

Natanguliza shukurani.
 

Kama hilo gari total price (CIF) ni $1670 au chini ya hapo, ushuru ni 3.7mil. Bei uliyoweka hapo ni FOB, inabidi ujue CIF ni dola ngapi. Kama CIF itazidi hiyo $1670 basi ushuru utapanda na makadirio ya ushuru mpya yatafanywa upya na TRA. Pia ongeza milioni 1 kwa ajili ya gharama nyinginezo (change huenda ikabaki).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…