Wazee poleni na majukumu, nimenunua gari toyota allion cc 1490, milleage 57000km, ya mwaka 2002, engine VVTI.gari imefika mwezi wa 6 mwaka huu..tatzo la gari hii ni kutumia mafuta mengi, yaani inakwenda wastani wa 1lita per less than 7km, nilienda kwa fundi mmoja wa mtaani akaniambia nibadilishe plug. Nimebadilisha plug tena pale kariakoo lile duka la kisangani nimeweka plug original lakini bado gari linakunywa sana mafuta tofauti na.cc zake na situmii hata AC. tatizo jingne ni.gari kutokuwa na.nguvu wakati wa kupanda mwinuko mdogo tu.
Najua jamii forum naweza pata ushauri wa nini kufanya hapa. Asanteni sana ndugu