Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Hapo haina noma kama hakuna saizi hiyo..kinachobadilika hapo ni upana wa tairi utakuwa mkubwa kidogo ila aspect ratio itapungua na rim size ni ile ile
 
Kagua kwenye milango ya gari yako. Manufacture huwa wanaandika range ya size za tairi zinazokubalika kwa gari husika.
 
Jamani naombeni msaada juu ya Nissan March uimara wake, spea pamoja na ulaji wa mafuta maana nataka kuiagiza nimeipenda sana ila naogopa kuna watu wanadai spea zake hazipatikani na ni ghali sana, nataka kupata ukweli
 
Last edited by a moderator:
Za mda huu wadau nimeuliza zaidi ya mara 3 naomba kujua kuhusu pajero mini
Nina vitz nataka kushift kweny hyo gari
Ningependa mnisaidie kuhusu unywaj wa mafuta upatikanaji wa spea na pia mafundi wake wapo
Asanten sana

Ni gari nzuri ila hazitaki shida ndio maana watu wengi wanazikimbia na spare iko juu
 
Hapo haina noma kama hakuna saizi hiyo..kinachobadilika hapo ni upana wa tairi utakuwa mkubwa kidogo ila aspect ratio itapungua na rim size ni ile ile

Wakuu Asanteni kwa ushauri wenu.

cc: mzawahalisi
 
Jamani naombeni msaada juu ya Nissan March uimara wake, spea pamoja na ulaji wa mafuta maana nataka kuiagiza nimeipenda sana ila naogopa kuna watu wanadai spea zake hazipatikani na ni ghali sana, nataka kupata ukweli

Kitendo cha kutamka tu Nissan........kimenifanya nipate mawazo.........mbona Vitz na passo ni nzuri tu.......
hapa nataka kukueleza kuwa.........Toyota ni Friendly kwa watanzania ikifuatiwa na Suzuki............waliobaki hawataki mazoea na sisi...........
 
Asante nimekuelewa, lakn nataka kujua tatizo lake hasa ni nini? Nimetokea kuipenda tu hii gari.
 
Aisee Geem nieleweshe vizuri hapa, oil nimemwaga mara moja, na hizi poston rings ndo enjector mozle au..nieleweahe vizuri hapa.maana mafundi wa.mtaa.kila.mtu anajibu lake

Sielewi sana lakini naweza kukuelewesha...........piston rings ni tofauti kabisa na nozzle..........halafu idadi ya nozzle inategemea na gari yako ni ya cylinder ngapi.........na nozzle moja ikifa......inaweza kuleta kwikwi kwenye gari yako.........
eti Mshana Jr...... MANI....... RRONDO......... OLESAIDIMU......... Kaizer.......ni hivyo...........au nimechemka.........?....
 
Last edited by a moderator:
Asante nimekuelewa, lakn nataka kujua tatizo lake hasa ni nini? Nimetokea kuipenda tu hii gari.

Tatizo la Nissan ni spea.........ila kama hilo sio tatizo kwako.......why not bana..........kanaonekana ni kagumu na kanahimili vishindo...........
 
Tatizo la Nissan ni spea.........ila kama hilo sio tatizo kwako.......why not bana..........kanaonekana ni kagumu na kanahimili vishindo...........

Nashukuru sana kwan ushauri wako, ngoja tusubiri na wengne tuone wanasemaje, ila bado sijajua ulaji wake wa mafuta.
 
Tatizo la Nissan ni spea.........ila kama hilo sio tatizo kwako.......why not bana..........kanaonekana ni kagumu na kanahimili vishindo...........

mkuu spare tatizo kivipi??

kwani yupo wapi mpaka anakuwa na hofu na spea za nissan??

sema kama amezoea toyota huku lazima ataona kuwa anaonewa maana bei ya spea imesimama sana.ila uziri wake ni original ukifunga uhakika 100%
 
Asante sana kwa ushauri, kweli nasikia gari kama Nissan, Subaru, Mitsubishi nyingi spea zake ni ghali lakn orijino, hapa cha msingi kama zinapatikana hakuna shida, zingekuwa hazipatikani ingekuwa tabu.
 
Aisee hiyo ni gearbox hydraulic filter imechoka au imejaa uchafu hivyo inachelewa kuingia kwenye mzunguko wa gearing system

Ahsanteni sana. Nitapeleka kwa fundi wkend ijayo. Na hiko kifaa si hakina gharama kubwa na pia hakichukui muda mrefu kuki-replace.?!
 
Wakuu, nampango wa kuagiza Toyota Voltz... Mwenye uzoefu wa hii gari naomba ushauri.

Gari iko smart tuuu, wala haina shida, karibu Autocom Japan Inc, wauzaji wa magari used yenye ubora kabisa, office zetu zipo hapa Quality Center Dar es salaam almaarufu kama uchumi supermarket, 📞 0767328063 for more information
www2.autocj.co.jp
 
Wakuu salaam! Naomba kwa mwenye uzoefu wa Nissan March toleo la 2004 anijuze uzuri na ubaya wa gari hiyo. Natanguliza shukrani 🙏
 
Wakuu naombeni ushauri cha kufanya
Fungua za gari yangu ghafla zimegoma kufunga kwa remote, yaani badala yake nafunga manually sasa, nahisi betri sijui imeisha (ila sina uhakika kama inakuwa na betri ndani) maana nikibonyeza kitufe cha kufunga gari hakuna response yeyote. Sijui nifanyeje wakuu ili niweze tena kufunga kwa remote?

cc mshana jr
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…