Asante ila kwa sasa nikp dodoma..ningejua brand gani zina ubora huo nimunue huku. Tindi
Kuna njia mbili ya kwanza, jaribu kidia general spares kama hana muagizie mtu akununulie hapa dar. Ila kwa ushauri wangu gear box oil ndio uhai halisi wa gari yako. Ukikosea kuweka oil ambayo siyo sahihi basi matatizo ya gari hayatakwisha
Nina tatizo naomba mnisaidie.
Leo asbh wakati nataka kuwasha gari nimeweka Switch on haijaonyesha kitu.Baada ya muda kama dk 3 hv ndio ikaanza kuonesha switch on ila ikiwa imefifia.Baada ya dk 2 Nikaweka switch off, halafu nikaweka tena Switch on ndio nikaona imekubali ikiwa na full charge na gari likawaka.Nika anza safari ila nikiwa njiani ghafla nikaona gari limezima na dash board ikawa haioneshi kitu. nikapaki pembeni kabla hata sijafungua Boneti nikashangaa imeonesha switch on na nikapiga gari likawaka.
Naomba umnisaidie linaweza kuwa ni tatizo gani hilo??
Gari yangu ni premio New model ya 2003.
Wakuu mi nina tatizo hivi,gari yangu sijui ina tatizo gani maana nikitembea umbali fulani kwenye odometer/speedometer haionyeshi umbali sahihi kama unavyojulikana.
KWA MFANO
umbali toka Dar mpaka chalinze ni km 109 hii inajulikana lakini mi nikienda mpaka chalinze umbali hausomi 109km badala yake itasoma kama 97km na hapo safari yangu imeanzia Mbagala kuu maeneo ya mgeni nani.
Je hii hali usababishwa na nini?
Inaweza ikawa sawa tuu gari yako.Kwani ww unajua hizo 109km za Chalinze zomepimwa kutokea wapi??Inaweza ikawa ni kutoka posta au kkoo na wala sio Ubungo.Maana mm mwenyewe huwa nafuta km kutokea Sinza ila nikifika Morogoro Msamvu inasoma Km zizisizofika hata 180km wakati vibao vinasema Dar moro ni 193km
Kuna uzi hapa tena umekuwa "stick" una kila kitu kuhusu hayo magari nakushauri uutafute utakusaidia mengi.
Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.
Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.
Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake
Karibuni sana
Ushauri: Jinsi ya kununua gari iliotumika ndani ya Tanzania
View attachment 225786
Habari ya jumapil..
Napenda kutaka kujua kuhusu toyota ipsum.Hasa katika fuel consuption,,
uzuri na ubaya wa hili gari. Upatikanaji wa spare zake n.k
Habari ya jumapil..
Napenda kutaka kujua kuhusu toyota ipsum.Hasa katika fuel consuption,,
uzuri na ubaya wa hili gari. Upatikanaji wa spare zake n.k
Za old model ni vimeo fulani hivi kwa hapa kwetu new model ziko vizuri ila zinakunywa mafuta kutokana na ukubwa wake wa engine
Asante.. nilikua nazipenda kwa sababu zina seats za kutosha.
Vip alternative ni gari gan..ambayo nayo.ina seats 7
Gari nyingi hizi za kisasa kwa uimara sio kivile hizo Ipsum Uganda ni nyingi sana waweza ichukua lakini uitunze la sivyo Toyota wish lakini nayo haitofautiani sana na ipsum