Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Nzuri sana hasa ukipata RD5, inakamata road vizuri ngumu fuel consuption ni nzuri ndani kuna nafasi ya kutosha pia

Mkuu hizi gari ni super, ndio maana soko lake kubwa liko UK, ni gari nzuri nimeitumia kwa mda mrefu sana
 
Mr mshana naomb na wadau wengine wajuz mnisaidie kati y spacio old model n terious IPI nzuri mana Kazin napandisha mlim
 
Mr mshana na wadau wajuz naomben msaad kati ya spacio old model n terious IPI inafaa n haisumbui mana kazin napandisha mlima
 
Inaweza kuwa kweli, sijawahi kubadilisha nilishasoma kwenye kichwa cha dipstick ya gearbox hydraulic pameandikwa "Do not change under normal operation"

Mkuu Columbus umefanikiwa kutatua tatizo lako?

Naomba tuwe tunapeana mrejesho wa utatuzi wa matatizo kwa manufaa ya wanajukwaa.
 
Naomba kuuliza, kwann toyota passio znauzwa bei nafuu kdogo ukilinganisha na gar znazoendana nazo kama toyota ist. Nini siri ya hz kuuzwa bei nafuu au zna matatzo mengi ukilinganisha na ist? Wajuzi wa magar naomba msaada, nmevutiwa na mwonekano wa passio ila bei yake inanipa walakain kidogo
 
Naomba kuuliza, kwann toyota passio znauzwa bei nafuu kdogo ukilinganisha na gar znazoendana nazo kama toyota ist. Nini siri ya hz kuuzwa bei nafuu au zna matatzo mengi ukilinganisha na ist? Wajuzi wa magar naomba msaada, nmevutiwa na mwonekano wa passio ila bei yake inanipa walakain kidogo

spacio gari nzuri sema haitaki shida... sio gari ya kuendesha rough.kwa barabara zetu za kibongo.. wengi hawakai nazo muda kabla hazijaanza kugonga na kutoa milio.. kama ni mtumiaji mzuri wa gari uta enjoy spacio
 
Nisaidieni wadau jinsi ya kuwa naweka mafuta kwenye gari pale sheli kwa kutumia kadi nataka niachane na hii tabia ya kutoa pesa mfukoni

Mkuu, Tz hii au hiyo shell ni kampuni ya wapi? Nijuavyo hizo system kwa Tz ni km bado kabisa. Unazungumzia EFPOS si ndio? Kama zipo basi kunakua na mashine ambayo lazima awepo operator ukimaliza kuweka mafuta basi unaenda counter na kutaja pump ulojaza anakuomba kadi unalipa kwa kadi baada ya kumpa mhudumu. Sijajua km tumeelewana?!
 
Naomba kuuliza, kwann toyota passio znauzwa bei nafuu kdogo ukilinganisha na gar znazoendana nazo kama toyota ist. Nini siri ya hz kuuzwa bei nafuu au zna matatzo mengi ukilinganisha na ist? Wajuzi wa magar naomba msaada, nmevutiwa na mwonekano wa passio ila bei yake inanipa walakain kidogo

Una maanisha spacio au passo? Sijakusoma vzr
 
wakuu za jumapili...nina gari aina ya PASSO piston 3 inatatizo ambalo nimepeleka kwa mafundi wengi lakini wameshindwa kulikwamua.....

tatizo lenyewe ni kuwa wakati wa asubuhi nikiiwasha huwa haina nguvu nahapo hapo huzima so huwa narazimika kuiwasha kwa zaidi ya mara moja na ili nianze safari inanibid niiache iungurume kwanza kwa zaid ya dakika 5... pia tatizo hili hujitokeza kipindi ambacho gari haijawashwa kwa muda mrefu..jr tatizo lipoi hasa ...je ni sencors tu na je ni ipi?

n.b. gari imefanyiwa service yote pamoja na kuwekwa plag mpya
 
wakuu za jumapili...nina garua aina ya PASSO piston 3 inatatizo amabalo nmepeleka kwa mafundi wengi lakini wameshindwa kulikwamua.....

tatizo lenyewe ni kuwa wakati wa asubuhi nikiiwasha huwa haina nguvu nahapo hapo huzima so huwa narazimika kuiwasha kwa zaidi ya mara moja na ili nianze safari inanibid niiache iungurume kwanza kwa zaid ya dakika 5... pia tatizo hili hujitokeza kipindi ambacho gari haijawashwa kwa muda mrefu..jr tatizo lipoi hasa ...je ni sencors tu na je ni ipi?

n.b. gari imefanyiwa service yote pamoja na kuwekwa plag mpya

Pole sana mkuu, unaposema nguvu una maanisha 'compression' ya engine au ni kuwa ukiweka gear na kuongeza fuel haiondoki? I pity u brother hope utapata solution tu
 
wakuu naomba kuuliza ubora wa toyota probox van, engine code 1NZ, 1490cc ya mwaka 2009.. nataka kuitumia kwa ajili ya kubeba mizogo midogo midogo ya dukani. maana nimeona ina space kubwa na pia ukikunja kiti cha nyuma ina nafasi ya kutosha kuweka mzigo.. mnanishaurije wakuu kuhusu engine na maintenance yake???
 
Na corolla yangu nayo ina tatizo kama hilo ndugu yangu msaada tafadhali
 
Mhana kwa kuongeza more knowldge kuhusu magari,, usisahau namba hii pia to connect to whatsap group 0713535363,
 
UMEWAHI KUKAMATWA NA POLISI BARABARANI?

Je, umewahi kukamatwa na polisi wakati ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?
zijue haki na wajibu wako !

Bila kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani kutakuwa na vurugu katika barabara zetu.
Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za Barabara ? iwapo kila mmoja atazifuata sote tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama zaidi. Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao, isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.

Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati gani anakusimamisha uwapo barabarani.

Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako ? kama atakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani ? pia anaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).

Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari ? anaweza kukataa fotokopi ? hata hivyo, unaweza kuamua kupeleka leseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa. Ili kuepuka matatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).

Hati ya usajili:

Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili ? gari lazima liendane na maelezo ya kwenye kibandiko, lakini vitu vidogo kama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).

Leseni ya barabarani, na bima ya gari:

Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani na kibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).

Kunyang?anywa:

Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.

Mikanda ya kiti ya usalama:

Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) ? unatenda kosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.

Kuendesha baada ya kunywa pombe
:

Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi cha pombe kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatia ya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).

Kutumia simu ya mkononi wakati unaendesha:
Ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la ?kuendesha kwa uzembe? (RTA, s.42, s. 50).

Mwendo kasi:

Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) ? ofisa wa polisi anaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).

Kustahili kuwepo barabarani
:

Ofisa WA polisi ana haki ya kukagua Kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri ?unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.

KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA: Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwa ofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezo kwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini ? kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda Na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIA YOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisi anakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishi kwa Ofisa Msimamizi Mkuu ? ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu ?usitoe rushwa na usipokee rushwa.

Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na kuyaweka kwenye gari lako ? lakini kumbuka kwamba ni mwongozo tu.

Noted!
 
wadau mwenye uzoefu na gari aina ya mitsubish GDI au io please maana natamani kununua kwa mtu
 
Back
Top Bottom